Irene Uwoya Achoshwa na Maswali kuhusiana na Uhusiano Wake na Dogo Janja

Mwigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka kuwa amechoshwa na watu wanamuuliza kuhusiana na uhusiano wake na Mwanamuziki Dogo Janja.

Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Irene Uwoya na Dogo Janja wana uhusiano wa kimapenzi, uhusiano huu umekuwa ukileta gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tofauti kubwa ya kiumri iliyopo baina yao. Dogo Janja ana umri wa miaka ishirini na mbili (22) na Mrembo Uwoya andaiwa kuwa na umri wa miaka ishirini na tisa (29), Huku bado kukiwa hamna uthibitisho Kama wawili hao ni wapenzi maneno hayo yamebaki kuwa ni tetesi tu.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha ‘over the weekend’ Irene alifunguka kuwa amechoshwa na kuulizwa maswali juu ya yeye kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dogo Janja ni suala lake  binafsi na hahitaji kuulizwa na haijalishi atakuwa na mtu anayemtaka.

“Sitaki na sihitaji kumzungumzia Dogo Janja na nimechoshwa na maswali kuhusu kuwa kwenye mahusiano naye hayo ni mambo yangu binafsi na ninaomba niachwe kwa kweli”.

Warembo wengi wa Bongo movie wanasifika kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana wenye umri mdogo kuliko wao huku wakijulikana kwa majina  kama Serengeti boys, ben-10.

 

Uwoya Abainisha Sifa za Mwanaume Anayemtaka

Muigizaji wa Bongo movies maarufu na mrembo Irene Uwoya ambaye pia amewahi kuolewa na mcheza mpira maarufu kutoka Rwanda, amesema anataka mwanaume atakaye kuwa naye awe na ngeu nyingi mwilini za kuchanwa na visu!

Irene amesema watu kama hao ndo anawataka yeye kwani inaonyesha kuwa ni uanaume halisi, na sio mwanaume anakuwa laini kama mtoto wa kike.

Irene alinukuliwa akisema:

“Sijasema napenda mwanaume mwenye sura mbaya nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume,  mwanaume uwe na ngeu, mimi bwana wangu ana ngeu, kachanwa visu yaani”.

Irene kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake mapya tangu kuwe na tetesi za kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Msami Baby na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi wazi kwa watu.

Ingawa kumekuwa na tetesi mitandaoni kuwa Uwoya anatoka kimapenzi na mwanamuziki kijana mdogo Dogo Janja ingawa Uwoya ameshakataa kwamba hakuna chochote kinachoendelea baina yao.

Irene Uwoya adhihirisha, kutokuchuja kwa ubora wake

Mwanadada aliyewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania  mwaka 2006 ambae pia kwa sasa ni msanii mkubwa katika tasnia ya filamu Irene Uwoya  amefunguka na kujipa sifa kubwa kuhusu kazi zake za sanaa.irene  anasema kuwa kipaji chake ni kipaji ambacho akiwezi kulinganishwa na mtyu yaani ni cha kipekee licha ya kuwa yeye ni mmoja kati ya wakongwe katika tasnia hii,kwa sasa hivi tasnia ya filamu imegubikwa na chipukizi la waigizaji lakini yeye bado anajiona kuwa ni mwamba hata kama kuna vitu vipya vinaibuka.

Irene anaongezea kuwa pamoja na udogo na uchipukizi aliokuwa nao kipindi hicho cha  mwaka 2008 lakini bado aliweza kutwaa tuzo ya  mwigizaji bora wa kike wakati ndio alikuwa bado mpya katika fani ya uigizaji kitu hicho  kinachozidi kumuongezea ubora wake katika kazi zake.”ubora wangu umedumu kutoka kuingia kwenye game  hadi sasa na hii yote ni kutokana na misimamo katika kazi,”aelezea Irene

Lakini pia irene anasema kuwa sio kwamba anaigiza kila filamu tu ilimradi ameigiza , na bado anaona kuwa yeye ndio msanii wa kike aliingia kwenye fani na kutwaa tuzo ya ubora.

Kuhusu yeye kuwa kimya ,Irene amesema kuwa kwa sasa ameigiza filamu moja tena imemlipa ela nyingi ivyo anasubiri iyo itoke ndipo aweze  kucheza filamu nyingine.

Hata hivyo, pamoja na uwepo wa skendo za mitandaoni kuhusu ugomvi wa yeye na baba mtoto wake ,na pia habari zilizokuwa zikisambaa kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na msanii mdogo wa Bongo Fleva  Dongo Janja ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha ngalenaro bado msanii huyo anaonekana kutokuteteleka na manen ya kwenye mitandao na bado anapeta na kujiamini zaidi.

Lakini pia kwa sasa hivi Irene uwoya amekula dili nono la kutangaza simu za kampuni ya Itel

Irene  Uwoya ni mama wa mtoto mmoja wa kiume  anaitwa ‘Krish’, mtoto ambae amezaa na aliyekuwa mume wake wa ndoa mcheza soka  Ndikumana lakini baadae walikuja kutengana.