Penzi La Vanessa Mdee na Jux Lazidi Kuwachanganya Mashabiki

Wasanii wa kizazi kipya Juma Jux na Vanessa Mdee wamezidi kushika vichwa vya habari na kuwazingua mashabiki zao kila siku kwa matendo yao wanayofanya wakiwa stejini.

Wasanii hawa ambao walikuwa wapenzi siku za nyuma wamezidi kushika vichwa vya habari kila siku huku kila mmoja akijiuliza kama wako wote au hawako wote. Jux na Vanessa walikuwa kwenye uhusiano kwa miaka minne kabla hawajaachana mapema mwaka kwa sababu zisizojulikana. Wote wawili waliweka wazi kuwa pamoja na kuwa ameachana lakini kila mmoja bado anampenda mwenzie, huku Jux akisisitiza kuwa amejaribu kurudiana na Vanessa lakini amekataa kwa kile alichodai kuwa akiachana na mtu hawezi kurudi nyuma.

Wakati tamasha la Fiesta likiwa bado linaendelea wawili hawa wamezidi kuwa kivutio kwa mashabiki zao ambao wanahudhuria tamasha hilo ambapo Jux na Vanessa wanaonekana wakibambiana kuimbiana kimahaba na hata kupigiana magoti. Walipokuwa kwenye Fiesta mkoani Morogoro baada ya Jux kutumia zaidi ya dakika tatu kumuimbia Vanessa alipewa masharti magumu ambayo aliambiwa endapo angeyatimiza basi angepokelewa tena.

Baada ya Jux kuimba kwa hisia hadi kupiga magoti, Vanessa ambaye alionesha kutokuridhika alimwambia masharti yake:

Huyu brother msimu wote wa Fiesta amekuwa akiniimbia sijui anauawa, sijui analia sielewi mimi, sasa sikilizeni nyie wote hapa ni mashahidi bado siamini kama anataka kurudiana na mimi nampa dakika kumi na tano tu tukikutana fiesta Dar es Salaam nyie ni mashahidi, akiweza fresh kama vipi aendelee kuuawa au sio?”.

Jux naye alijibu atazifanyia kazi hizo dakika kumi na tano ili ampate tena mrembo huyo. Mshabiki wamekuwa wakichanganyikiwa kwa kutoelewa kama ni kweli wawili hao wameachana au wapo woye maana inasemekana huko mikoani wanaonekana wakiwa na ukaribu wa ajabu.

Mimi Mars Aweka Wazi Uhusiano Wake na Mpenzi Wa Dada Yake Jux

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘siamini’ Mimi Mars ambaye pia ni dada wa damu wa mwanamuziki Vanessa Mdee amefunguka na kuongelea habari zilizoenea kuhusiana na uhusiano wake na Jux.

Siku chache zilizopita Mimi Mars na Jux waliweka picha mtandaoni wakiwa pamoja kitu kilichopelekea mashabiki kuanza kuhoji ukaribu wao ukitegemea kuwa Jux ni/ alikuwa shemeji yake kwa dada yake Vanessa.

Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Clouds, Mimi Mars amefunguka kuwa alikerwa na tuhuma hizo kwani zilikuwa tu ni picha walipiga na hawana uhusiano wowote;

Kwanza taarifa zile zilinikasirisha kwa sababu huko ni kukoseana heshima kwa kweli inamaanisha watu wananionaje na mnanichukuliaje kuona kwamba mimi naweza kufanya kitendo kama hicho na mpenzi wa dada yangu lakini haileti maana kabisa lakini niliipuzzia habari ile ndio maana sijaiongelea wala sijaandika chochote maana najua ukibishana na watu ambao hawana akili vizuri huwezi shinda”.

Pia Mimi alifunguka kuhusu uhusiano wa Jux na Vanessa  kwa sasa kwani kumekuwa na tetesi mbali mbali kuwa wawili hao wamerudiana kutokana na ukaribu waliokuwa nao huko fiesta:

Kwangu mimi naona ni kama marafiki wawili kama walivyotuamba wenyewe ni marafiki ambao wanaendelea kuwa na uhusiano mzuri kwani tumejiwekea kuwa watu wakiachana lazima wawe maadui lakini sio lazima iwe hivyo kwaiyo wao wanatuenyesha njia tofauti ya kwamba watu mkiachana pia bado mnaweza mkawa marafiki kwa sababu sanasana hata ukikaa ukasikiliza maongezi yao wanayoongea ni jinsi ya kujengana kwenye shoo na mafanikio kwenye shoo”.

Pia Mimi Mars amefunguka kuwa anatamani dada yake Vanessa arudiana na Jux kwani ni mtu mcheshi na mkarimu na pia walivyokuwa pamoja walikuwa poa sana na pia Jux ana mapenzi ya dhati kabisa kwa Vanessa.