Diamond Ana Funguo za Nyumba Anaweza Kuja Muda Wowote

Mama wa mwana dada Hamisa Mobeto amethibitisha kuwa nnyumba ambayo amenunuliwa mtoto wa hamisa mabae ni mjukuu wake ni ya mjukuu wake na wala sio ya Hamisa kama watu wanavyotangaza katika mitandao kuwa Hamisa amenunuliwa nyumba.

Katika mitandao ya kijamii kumekuwa na maneno mengi yakisema kuwa mwana dada Hamisa maenunuliwa nyumba na Diamond tena hasa baada ya kuonekana kwa comments katika ukurasa wa hamisa wa instagram akiulizwa na Diamond kama wameipenda nyumba hiyo.

Mama wa Hamisa alisema kuwa pamja na kwamba  nyumba imenunuliwa lakini sio ya hamisa ni ya deedaylan na kwamba Diamond anao funguo za nyumba hiyo kwaio muda wowote anaweza kuja katika nyumba hiyo.

 

Nyumba Sio ya Hamisa, ni Nyumba ya Deedaylan;-Mama Mobeto

Mama mzazi wa mwanadada Hamisa Mobeto amefunguka na kusema kuwa Pamoja na kwamba ni kweli Diamond amemnunulia nyumba hamisa lakini nyumba hiyo sio ya hamisa kama watu walivyokuwa wakisema bali nyumba hiyo ni ya mtoto wao Abdul na amemshukuru sana mtoto huyo asie na mwaka hata mmoja kwa kuwafanya wakapewa nyumba.

Hamisa hajanunuliwa nyumba, kanunuliwa  daylaan, huyu ndio mwenye nyumba na kwanza namshukuru mjukuu wangu kwa kuja katika maisha yetu.bila daylan tusingekuwa hapa 

Hata hivyo Mama mobeto anasema kuwa anajua kuwa watu wanamchukia sana mtoto wake lakini waache na kwamba anajua kuwa ipo siku watakuja kumpenda kwa sababu swala la mwanaume kumchagua mwanamke wa kuona ilo ni swala la Diamond kuamua.

Najua kuwa mwanangu wanamchukia lakini ipo siku watampenda tu , naomba wamuache mwanangu wasimsakame wamuache swala la kuoa anajua kuchagua ni mwanaume.

Mama Mobeto Achoshwa na Skendo za Diamond.

Mama wa video queen maarufu nchini Mama Mobeto amefunguka na kusema kuwa amechoshwa na tabia ya waandishi kuwa wanamuliza maswaka yanayomuhusu diamond wakati wao sasa hivi wako busy na kufanya kazi na sio kuzungumziwa katika mitandao ya kijamii.

Mama Mobeto amsema hataki kabisa kusikia habari zinazomuhusu Diamond kwa sababu kila mtu sasa hivi ana maisha yake hivyo waache kumfatilia.

jamani sisi mambo hayo ya kwenye mitandao hatuna kabisa,hata mtoto wangu ameshayasahu hayo mambo kabisa sas hivi, badala yake yupo kabisa na mambo yake mengine sasa hivi.michakato  yetu sasa hivi ni kutafuta pesa na wala sio kitu kingne kabisa.muda wa kuchokoana katika mitandao hatuna tena sasa hivi michakato yetu ni kutafuta pesa tu sasa hivi .tukiwa tunaongelea hivyo hatuwezi kupiga hatua kabisa kwaio kama kuna watu wana weza kufanya hivy acha wao wafanye tulishajivua kabisa na hayo mambo na hata huyo Diamond hatutaki kusikia mamneno yake tena.

Wakati Mama Mobeto akisema hayo kuhusu diamond na maisha yao mpaya huku  mtoto wake Hamisa alipost maneno katika mtandao wa snapchat kuwa amemmsi mwanaume wake ambao inasemekana kuwa mwanaume huyo ni diamond platinumz.

Mama Mobeto Amtupia Mama Diamond Dongo Gizani

Ilivyoanza ilikuwa ni vita kati ya Zari na Hamisa lakini sasa inaonekana kama vita hii inaelekea kuathiri hadi familia nzima kwa zande wote, mama mzazi wa Hamisa Mobeto ametupa dongo kali kwa mama mzazi wa Diamond Platinumz kutokana kile kuwa mama huyo ameolewa na mwanaume aliyechini ya umri wake.

Mama huyo amesema kuwa pamoja na kwamba hata yeye ana mume kwa sasa lakini kama anataka kuolewa basi ataolewa na mwanaume aliyemzidi umri au ambae wapo sawa nae ili basi watoto wake na wajukuu wapate baba watakae kuwa wana uhuru wa kumuita babu.

Mama Mobeto amesema kuwa kwa umri alionao sasa hivi yeye ameshakuwa mtu mzima kwaiyo kitendo cha kuolewa na kijana au mwanaume aliye chini ya umri wake ni kujishusha hadhi akiwa kama mama na bibi pia.

jamani mimi kama ni kuolewa ntaolewa na mtu mzima mwenzangu, kwa sababu serengeti boys kwangu haitawezekana kabisa,nahitaji kuolewa kweli ila itabidi niolewa na mtu mzima mwenzangu ili wajukuu nao wapate babu.

Hata hivyo maneno hayo inawezekana yamesemwa na mama huyo kutokana na kitendo cha mama mzazi mwenzie upande wa pili(mama yake na Diamond) kuolewa na kijana mdogo zaidi yake hivi karibuni.hii ni dhahiri kuwa kutokuelewana kwa hamisa na diamond kunasababisha kuenea kwa chuki mpaka kwa familia zao.