Mdogo Wa Ndikumana Kuiponda Bongo Movies

Mdogo  wak maraehem Hamad Ndikumana anajulikana kama Laddy  Ndikumana  amefunguka na kuwatukana  wasanii wa bongo movies kwa kuwaita wanafiki kutokana  na kutoonekana katika msiba wa kaka yake wakati kipindi yupo hai wengi walikuwa wakionekana  kuwa karibu nae

Hamad Ndikumana ambae alikuwa mume wa msanii Irene Uwoya awa ndoa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja alifariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa moyo na kuzikwa huku kwao nchin Rwanda.Irene Uwoya alifanikiwa kwenda kuzuru karibu la mzazi mwenzie huyo ingawa hakupata bahati ya kuzika mwili wa marehemu.

Akiongea na Big Chawa wa Planet Bongo  ya East Afrika Laddy Ndikumana alisema kuwa  wasanii hao wamekuwa wajinga na wanafiki sana  kwa kuwa wameshindwa kufika katika msiba  wakati kipindi yupo hai wengi walikuwa marafiki zake na walikuwa karibu nae kwa kipindi chote.laddy anasema kuwa kipindi kaka yake alipokwa na hela walikuwa wanakula nae bata kila kukicha.

Wapo baadhi ya wasanii walionyeshwa kuguswa na msiba huo na kufika nyumbani kwa Irene ambapo familia ya mwanadada huyo ilikuwa ikiombeleza  msiba huo kabla ya kupanga safari ya kwenda rwanda kwa ajili ya mazishi ya mwanasoka huyo ingawa hawakuweza kuwahi, hata hivyo wapo baadhi ya watu kutoka bongo movies ambao waliongozana na mwanadada Irene katika kuhani msiba huo akiwepo Mike Sangu ambae alitumwa kama mwakilishi wa bongo movies.

 

 

Aliekuwa Mume Wa Irene Uwoya Afariki Dunia

Aliekuwa mume wa msanii wa bongo movie Irene Uwoya  maaarufu kama Ndikumana afariki Dunia jana usiku.Ndikumana alikuwa maarufu kutokana na umahiri wake katika soka na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akichezea timu ya  APOP  Kinyras Peyias ya  nchini Cyprus.

Hamad Ndikumana alikuwa na umri wa miaka 39 kutoka nchini Rwanda alifariki usiku wa kuamkia leo ikisemekana kuwa alikuwa na matatizo ya moyo lakini alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida.

Ndikumana na Irene Uwoya hawakuwahi kutengana kisheria lakini hawakuwa pamoja kwa takribani zaidi ya miaka mitatu nyuma  lakini walikuwa wamebahatika kupta mtoto mmoja wa kiume.

Mpaka mauti yanamfika Ndikumana na Irene Uwoya walikuwa katika mafarakano na kutupiana maneno katika mtandao kutokana na irene uwoya kufunga ndoa na msanii mwenzie upande wa bongo fleva Dogo Janja .

Irene uwoya akiwa na Ndikumana siku ya harusi yao

Marehemu ndikumana akiwa na mtoto wake aliezaa na Irene Uwoya

 

Ndoa Ya Irene Na Ndikumana Haijavunjika

Baada ya kusambaa kwa picha nyingi za harusi kati ya msanii wa bongo fleva Dogo Janja na msanii wa bongo movie , mwanadaada mlimbwende katika tasnia hiyo Irene Uwoya  na hata baadae watu hao kuamua kuthibitisha ndoa iyo ingawa baadhi ya mashabiki na watu wao wa karibu bado wakiona ni kama kitendawili kilichokosa majibu kwa wawili hao kuoana.

Hata baada ya kusambaa kwa picha hizo , mume wa kwanza wa Irene Uwoya  anaefahamika kama Ndikumana ambae walifunga nae ndoa ya kikristo kanisani pia alijibu mapigo kwa kuweka post akiwa na mwanamke mwingine inaesemekana kuwa ni wa nchini kwao.Wawili hao walitengena bila idhini ya imani yao iliyowaunganisha kukubali wao kutengana .

Akizungumza na moja ya waandishi wa habari wa gazeti pendwa hapa nchini moja ya waasisi wa dini ya kikristo ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa hata kama Irene Uwoya ameamua kuolewa na mwanaume mwingine lakini bado ndoa yake na mumuwe wa kwanza aliefunga nae  kanisani bado inatambulika palepale kwa sababu kanisa lilichukua jukumu la kuwaunganisha kwa makubaliano na pia ilitakiwa warudi tena kanisani kupata ushuruhishi wa matatizo yao.

Ndoa yao bado ipo hai kabisa kanisani kwa sababu kanisani kwetu hauna talaka,talaka itatoka pale kumegundulika tatizo kubwa kama mmoja atakuwa anazini na ushahidi ukawepo kabisa au kutokee  tatizo la kinyumba  ambalo haliwezi kutatulika ndio kibali cha talaka kitatolewa na ndoa itabatilishwa  lakini kimsingi kabisa kanisa halitambui talaka.

Hata hivyo kiongozi huyo alisema kuwa kwa kile anachokifanya Irene na muwe wake huyo wa ndoa kwa kubadilsha wanawake kila siku ni dhambi ya kizini ambayo kanisa pi inaikataza.

Kanisa linakataza kabisa uzinzi na wanachokifanya wao kwa sasa ni uzinzi,kitendo hicho hakimpendezi mungu kabisa, kwa sababu ni kinyume na biblia inavyosema na imani ya kikristo.wanatakiwa wabadilike wakae  wamalize tofauti zao.

Irene Uwoya na Ndikumana walifanikwa kufunga ndoa na kuzaa mtoto mmoja ambae , kwa sasa Irene ameolewa ndoa ya kiislamu na kuachana na ndoa ya kikristo aliyokuwa nao kwanza.