Ruby Akiri Kutengeneza Picha Za Shepu Feki Ili Kutafuta ‘Kiki’

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ruby amefunguka na kukiri kuwa mbinu nyingi za kupata kiki mtandaoni kwa wasanii bila kukaa uchi mojawapo ni njia yake aliyoitumia wiki chache zilizopita ya kutengeneza picha za shepu feki.

Wiki iliyopita Ruby alizua gumzo mtandaoni baada ya kurusha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na makalio makubwa kupita kiasi tofauti na umbo dogo la Ruby lililozoeleka na watu.

Baada ya picha hizo kusambaa maneno Mengi yalizuka huku wengine wakidai pica zile ni za kutengeneza huku wengine wakidai kuwa Ruby amekunywa dawa za kichina kuongeza msambwanda use mkubwa tofauti na zamani.

Kwenye interview aliyofanya siku chache zilizopita Ruby amesema zipo njia nyingi za wasanii kupata kiki kuliko kupiga picha za utupu na kudhalilishana na badala yake wanaweza kutumia njia aliyofanya yeye kwa kutengeneza umbo lake.

Ruby amedai kuwa kwa kupitia simu yako mtu unaweza ukajiremba kwa jinsi ambavyo utaweza kusababisha mashabiki zake waendelee kumfatilia na hata kumjadili:

Zile picha zenye kunionyesha umbo kwanza alinitengenezea shabiki yangu akanitumia kisha mimi nikaona niiweke mtandaoni kama somo new wasanii wenzangu ili kuwaonyesha kuwa unaweza ukafanya kitu kama kile na ukapata attention uliyokuwa unaitaka. Badala ya kupiga picha za utupu na sasa serikali ipo macho siyo vizuri napenda tuwe wabunifu”.

Hivi sasa imekuwa kawaida kwa wasanii Wa Bongo fleva na Bongo movie kufanya matukio mbali mbali ili wapate attention ya watu mitandaoni ili waendelee kukaa kwenye chati kitendo hicho kinaitwa ‘Kiki’.

Ruby Ajisifu Kuwa Nandy Mamuwezi Katika Muziki

Ruby ni moja ya wasanii waliokuja na kufanya vizuri sana katika tasnia ya muziki lakini ndoto zake zilizimika baada ya kukosana na menejimenti yake na kushindwa kuendelea na muziki kwa kipindi cha muda mrefu kidogo , lakini moja ya wasanii wa kike wenye kipaji cha kuimba na anaweza kufanya vizuri kama atapewa nafasi nyingine ya kufanya muziki.

Hivi karibuni msanii Ruby amekuja na nyimbo yake mpya iliyokwenda kwa jina la ‘are  you ready’, ambayo ni ya kwanza tangu kukaa kwake kimya kwa kipindi kirefu kidogo.

Aliipoulizwa kuhusu kimya chake cha muda mrefu Ruby aliibu kuwa sababu  moja wapo ya kukaa kimya ni kumpa nafasi msanii mwenzie Nandy ili aweze kujulikana katika muziki kwa sababu endapo na yeye angeendelea kufanya kazi basi Nandy asingeweza kufanya vizuri katika muziki kama ilivyo sasa.

Ruby anasema kuwa ujio wa Nandy haukuksumbua sana kwa sababu ana amini kuwa Nandy ni msanii mzuri lakini hakutaka kuanza kujishindanisha nae,lakini pia anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakisema kuwa ujio  wa Nandy ulikuwa ni wa kuziba pengo aliloliacha lakini ukweli ni kwamba yeye na Nandy wote wanafanya muziki wa aina moja lakini bado kuna tofauti kubwa kati yao hasa upande wa TONE  na SCALES zao katika muziki wanaoimba.

Hata hivyo Ruby ameomba kutokushindwanishwa na mtu yoote kwa sababu hapendi kushindana na mtu katikamaisha yake zaidi ya yeye mwenyewe tu, na hata kama wanafanya muziki wa aina moja  haimaanishi kuwa wanafanana hata kidogo.

Ruby anatangaza kurudi tena katika muziki na kusema kuwa wakati yupo kimya alikuwa akiumia sana pale alipokuwa akiona mashabiki zake wanalalamika na kumuomba arudi na kwamba walikuwa wakim-miss sana.

Mnaukosea Heshima Mziki Wangu Mkinifananisha na Ruby -Nandy

Mwanamuziki wa bongo fleva, Nandy amefunguka na kudai kuwa amechoshwa na kufananishwa na mwanamuziki mwenzie Ruby.

Kwa muda mrefu sasa Ruby na Nandy wamekuwa kwenye aina ya ushindani ambao unatokana na watu kuwafananisha kutokana na aina ya muziki wanaofanya.

Kwenye mahojiano na Extra Showbiz, Nandy amesema kwa muda mrefu mashabiki wake wamekuwa wakimfananisha na mwanamuziki mwenzake Ruby hivyo amewataka wanao mfananisha na Ruby waache mara moja kwani miziki yao Ina ladha zilizo tofauti sana pia.

Namheshimu Ruby ni mwanamuziki mzuri, lakini kumfananisha na mimi ni kunikosea heshima mziki wangu ladha ya mziki wangu ni tofauti kabisa na Ruby kutokana na utofauti wangu wa mziki ninaofanya na pia kama unaufahamu mziki wa Ruby anaofanya utagundua ni mziki tofauti”.

Alisema Nandy ambaye hakufafanua kwa undani zaidi alimaanisha nini kwa kusema hayo. Ingawa kila mmoja amesema kuwa hana bifu na mwenzake lakini inasemekana ni kama paka na chui yaani hawaivi katika chungu kimoja hata kidogo.

Ruby: Nimechoka Kusikia Habari za Nandy Kila Siku

Msanii wa Bongo fleva Ruby amechoshwa na kile alichodai ni kuulizwa habari za Nandy kila siku anapohojiwa.

Ruby na Mwanamuziki mwenziye Nandy wanasemekana kuwa wana bifu la chinichini kwa kile kinachodaiwa wamegombania bwana, ingawa wawili hao wameziki kukana kuwa kila mmoja hana tatizo na mwenziye lakini habari chini ya kapeti zinadai kuwa wawili hao ni panya na paka (hawapatani).

Ruby alifunguka hayo kwenye kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na stesheni moja ya redio na kudai kuwa amechoshwa na watangazaji wa media mbali mbali badala ya kumuuliza maswali ya maana kila siku wamekalia kumuuliza habari za Nandy ambazo kwa sasa zimeshamchosha na ni kitu kinachotengeneza ugomvi baina yao hata kama hakuna ugomvi.

Nachukia sana swali la kufananishwa na Nandy Kwa sababu honestly I am tired of that question! ni kama vile watangazaji wanashindwa ni maswali gani ya kuuliza , maswali ni yale yale nimeshayajibu sana ! I love Nandy she is a good artist, she is a good singer but don’t ask me too much questions about her, it’s like mnataka kutengeneza ugomvi sasa nashindwa kuelewa hata watu wa media mnatengeneza ugomvi sasa kwasababu swali lilishajibiwa mara Mia moja sasa kwa nini lijirudie kila siku?”.

Nandy na yeye alipoulizwa mara ya mwisho kama ana ugomvi na Ruby alikana kata kata ingawa wambea wa mjini wanadai eti kuwa wawili hao walikuwa marafiki walipokuwa wote THT lakini Ruby alipoondoka tu Nandy akajiweka kwa jamaa/ sponsor wa Ruby hivyo kusababisha ugomvi (habari hazijathibitishwa)

Kumbe Ruby Hakuwa Na Mimba

Miezi kadhaa ya nyuma kulikuwa na habari karibia kila kona zikiongelea habari ya msanii wa kike aliyekuwa akitambaa sana katika muziki wa Bongo Fleva  Hellen George kuwa ni mjamzito lakini kumbe habari zile hazikuwa za kweli, tetesi izo ambazo zilikaa kwa muda kidogo mitandaoni mpaka aliyempa ujauzito kujulikana kuwa ni kijana mmoja kutoka Arusha zimekanushwa na Ruby mweneyewe na kusema kuwa habari za yeye kuwa ni mimba ni uongo ilikuwa ni mimba feki.

Hata hivyo tetesi izo zimekuja baada ya yeye mwenyewe kuweka picha yake katiaka mitandao  akionyesha tumbo lake kuwa kubwa ivyo kama kawaida ya mitandao na mihemko ya mishabikaia walianza kuongea kuhusu kuwepo kwa ujauzito huo, hata hivyo Ruby mwenyewe hakutaka kubisha kuhusu maneno ya mashabiki akaendelea kuwapa moyo kuwa kweli yeye ni mjamzito kweli.

Akiongea katika mahojiano  na gazeti moja nchini Ruby ameamua kuelezea ukweli kuhusu ukweli wa mimba hiyo.Ruby anasema kuwa ni kweli alipost picha ya tumbo kubwa katika mtandao lakini siku iyo alikuwa ametoka kula pilau kwa mama yake aliloandaliwa na mama yake huyo , hata hivYo baada ya yeye kushiba akaamua kutunisha tumbo kama utani na kupost katika mtandao wake Instagram , picha ambayo ilifanya mashabiki  waweke maamuzi  ya moja kwa moja kuwa Ruby  ni mjamzito.

“Kwa kuwa  watu walinianzishia hilo na mimi nikawa ninaitikia kuwa ni kweli lakini sikuwa na mimba  ingawa hata nilipoulizwa na baaadhi ya watu nilijibu kuwa ni kweli nina mimba  na nilimtaja mpaka baba wa watoto wangu ambae alihusika na mimba hiyo  na kumuonesha katika mitandao  lakini kwa sasa sitaki kumzungumzia kabisa’ alisema Ruby.

Msanii huyo wa kike aliyekuwa akilelewa kumuziki kutoka jumba la muziki la THT , kwa sasa yupo kimya kutokana na yeye kutokuwana maelewano mazuri na menejimenti yake , lakini alipokuwa akifanya mahojiano katika vyombo mbalimbali vya habari Ruby alisema kuwa kwa sasa anajiandaa vvyema na yupo karibu kurudi katika muziki hivyo mashabiki wake wakaae wakimsubiri kwa nyimbo nyingi nzuri.

Ruby Aongelea Menejimenti Yake Na Muziki Kwa Ujumla

Msanii wa Bongo Fleva ambae alikuwa ameiteka tasnia ya muziki kwa muda kidogo siku za nyuma ambae pia kipaji chake kimekuzwa kutoka THT,  Ruby, amefunguka na kuongelea swala  la muziki na  maisha yake kwa ujumla.Ruby  anasema kuwa  kukaa kimya hakuathiri kipaji chake kabisa na wala hakuwezi kufanya  kipaji chake kipotee.

Ruby anasema kuwa  muziki wa sasa si muziki mzuri tena,wasanii wamekuwa wakifanya muziki biashara hivyo muziki unapotea kabisa.Ruby anakumbuka kuwa alipokuwa akiimba gospel alikuwa akifanya mazoezi wa wenzake kwa pamoja lakini kwa Bongo Fleva kitu icho hakipo badala yake wasanii wa bongo wanajikubali sana.

Alipoulizwa kuhusu menejiment yake Ruby anasema kuwa watu wa mitandao wamekuwa ni watu wa kusema vitu bila kujua ukweli wa kile kinachoongelewa,kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitaja kiwango alichopewa na menejinenti yake ili kufanya tamasha la Fiesta kuwa ni dogo ndio maana yeye akakataa kufanya show iyo na kuwa iyo ndio sababu ya yeye kugombana na menejimenti yake. Ruby anakataa maneno hayo na anasema yeye hakuwahi kuzungumza hivyo, kitu nilichokiongelea kuhusu menejiment yangu ni swala la maslahi,na hata  alipoongelea maslahi haikuwa kwamba ni ela ,maslahi ina mambo mengi.

“Sijui kama nilikosea ila kwa kipindi kile ni maamuzi yaliyokuja kwa sababu ya situation ya kipindi kile”anasema Ruby,Ruby anaendelea kusema kuwa endapo atapewa nafasi ya kumwambia Ruge chochote atamwambia tu “nakupenda” kwa sababu ni bosi wake na atabaki kuwa bosi wake.Ruby anamchukulia Ruge kama baba kwa sababu yeye ndie aliemtoa katika muziki na sio bosi wake tu .

“Mimi sina tatizo na Ruge , hata hataa.. kama ningekuwa na shida na Ruge wala hata nisingeongea , watu wanaona nina tatizo na Ruge kutokana na matatizo yaliyotokea, lakini matatizo yanatokea na haina haja ya kujenga bifu na mzazi” anasema Ruby

Ruby anasema kuwa ukipata shida ndio muda wa kuwajua marafiki zako, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimsema kutokana na kusimama kwake kimuziki lakini ukweli ni kwamba ana nyimbo nyingi na anadhani sasa ni muda wa yeye kuzitoa kwa sababu mashabiki wanamuhitaji.

Nandy afungukia bifu lake na Ruby

Msanii wa Bongo fleva, Faustina Charles maarufu kama Nandy amesema japo watu wengi wamekuwa wakihoji kuhusu ukaribu wake na msanii wa zamani wa zao la Jumba la kuibua vipaji la THT (Tanzania House of Talent), Ruby kwa madai kuwa kwa sasa hawapikiki chungu kimoja kutokana na ushindani uliopo baina yao, ishu ambayo ameikataa na sio kweli kwani hana bifu na mwanadada huyo.
Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni alisema anawashangaa wanavyosema hapatani na Ruby kwa madai kuwa anahukiwa kwa sababu amemfunika mwenzake kimuziki

“Ukiniuliza mimi na Ruby nani anaimba vizuri, nitakujibu wote, yeye ana muziki wake nami nina muziki wangu sina ugomvi wala mazoea naye ila tukikutana tunasalimiana tu kama washkaji”,

Kumekuwa na tetesi mbalimbali za kuwepo kwa bifu kati ya warembo hawa wawili kutokana na ufanano wa muziki wanaofanya japo wamekuwa wakikana kwamba hawana tatizo na ni washkaji tu.

Ruby afunguka kwa nini alimtema Soudy Brown wa Cloud FM

Ruby alikua mpenzi wa Soudy Brown (mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds FM) kwa muda wa miaka mbili. Mrembo huyo amefunguka kuhusu mahusiano yake na mtangazaji huyo.

Ruby alisema kuwa Soudy Brown ndiye mwanaume pekee kutoka kwenye industry ya muziki ambaye yeye amewai kuingia kimapenzi naye.

Ruby

Mrembo huyo alifunguka na kusema kuwa aliamua kumwacha Soudy Brown kwa sababu aliona mtangazaji huyo hakuwa na msimamo.

“Nikisema nitoke na mastaa wenzangu sio kwamba hawanisumbui wananisumbua sana lakini nawajua tayari the way walivyo. Lakini vitu vingi ambavyo naona wanafanyiwa wasanii wenzangu na mimi kweli nikawe na msanii? Hapana siwasemi kwa sifa mbaya wasanii lakini mimi siwezi kuisha nao kutokana na tabia zao kwa sababu mimi ni mwepesi sana kuumia. Mimi mwanaume ambaye nimetoka naye kwenye mapenzi na yupo kwenye industry yetu only ni Soudy Brown, na nimeishi naye kwa mwaka mmoja na miezi sita,” Ruby aliuambia mtandao wa Spin Tanzania.

 

 

Ruby aonyesha ujauzito wake (Picha)

Kunyamaza kwa Ruby kuna sababu, mrembo huyo hajatoa wimbo wowote hivi karibuni na pia hajakua akijadiliana na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii.

Mrembo huyo sasa amezua mdahalo katika mitandao ya kijamii baada ya yeye kuweka picha inayoonyesha tumbo lake.

Picha hilo linaonyesha kuwa Ruby ako na ujauzito ingawa mrembo huyo hukuandika chochote kudhibitisha kama anatarajia mtoto hivi karibuni.

Picha ambayo Ruby aliweka mtandaoni inayoonyesha ujauzito

 

 

 

Ruby amkana Ali Kiba

Hellen George maarufu kama Ruby amefunguka na kuweka wazi uhusiono wake na staa wa Bongofleva Ali Kiba. Uvumi mitendao ulikuwa unasema kuwa Ruby na Ali Kiba ni wapenzi.

Akiongea na Swaggaz, Ruby alisema hana ukaribu wowote na hit make huyo wa ‘Aje’. Mrembo huyo alisema hata hajawahi kuwa na mawasiliano na Kiba.

Ruby

Rubi alipuuza uvumi mitendaoni kuhusi uhusiano wake na Ali Kiba, alisema kuwa watu walishawahi sema yupo karibu sana na Diamond Platnumz .

“Na mimi taarifa hizo nimekuwa nikiziona kama wewe ulivyoziona, sioni jipya kwasababu walishawahi kusema kuwa nipo karibu sana na Diamond, sasa wamegeukia kwa Kiba ambaye hata mawasiliano yake sijawahi kuwa nayo,” Ruby alisema.