Mi Peter Sijawahi Kumuona,Nilikuwa Namuona Casto :-Sholo Mwamba.

Msanii wa singeli nchini, Sholo Mwamba ambae hapo awali aliwahi kufanya kazi na muna love ameongea na waandishi wa habari na kusema kuwa amesikia habari za muna kufiwa na mtoto wke na amesikitishwa sana lakini yeye na muna hawana mawasiliano yoyote hivyo anatuma salamu zake za pole.

Sholo anasema kuwa hata katika akaunti zake za instagram alishamblock kwaio hana namna ya kuwaisliana nae lakini hajawahi kujua habari zozte za peter lakini ameshawahi kuonana na casto mara nyingi sana na hata hospitali mtoto alipokuwa akiumwa walikuwa wakiangaika na casto hospitali.

Muna ameniblock instagram , lakini habari za msiba wa mtoto ninazo.nampa pole sana .kuhusu huyu peter mimi sijawahi kumuona kabisa ila nilishawahi kunuona casto mara nyingi sana lunc na hata mtoto alikuwa akiumwa tulikuwa tunaenda na casto hospitali  na kila sehemu .

nimeondoka kwa muna kwa sababu ya maswala hayo hayo  ambayo sasa hivi ambayo sasa hivi yanamtokea puani sasa hivi, niliondoka pale kwa sababu siwezi kuwa nawaita wakina dogo janja baba.

 

Sholo Mwamba Mbaroni Kwa Utapeli.

Msanii mkubwa na maarufu wa muziki wa singeli  nchini Seif Mwinyijuma  maarufu kama Sholo Mwamba  asakwa na polisi kwa tuhuma za  utapeli baada kutanguliziwa pesa kwa ajili ya kufanya shoo  katika mkesha wa mwaka mpya  katika ukumbi wa Dar Live lakini msanii huyo aliingia mitini na kutokomea na kusababisha fujo kwa mashabiki wake.

Akizungumza  kuhusu tukio ilo meneja wa Dar Live, Rajab Mteta  maarufu kama KP Mjomba  alithibitisha kuwa alimlipa fedha nusu msanii huyo  lakini hakutokea na hakutoa tarifa yoyote kuhusu kutokuja kwake katika tamasha hilo, na huku simu yake na simu ya meneja wake zikiwa hazipatikani.

Nilikubaliana na sholo mwamba afanye shoo  afanye shoo katika mkesha wa mwaka  mpya  na hata mkataba wa fedha alizochukua nusu upo,lakini hakutokea kwa ajili ya kufanya shoo , hali hiyo imezua tafrani sana kwa mashabiki wake na kufanya tuonekane matapeli.

Mashabiki walipoona kuwa Sholo Mwamba hajatokea wakaanza kuzua tafrani, ambapo walianza kufanya fuja na kufanya uharibifu wa baadhi ya vifaa.Kitendo alichafanya sholo mwamba sio kizuri kabisa matangazo yote yalikuwa yanaonyesha kuwa atakuwepo katika shoo kama alipata matatizo alitakiwa awasiline na mimi lakini kwa ivho alichofanya ni utapeli mkubwa.

Tayari meneja huyio alishafungua kesi polisi yenye rn namba KJN/RB/12/2018

 

Bifu La Young Dee Na Dogo Janja,Chanzo ni Muna

Kwa muda sasa kumekuwa na chokochoko kati ya wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva yaani Young Dee na Dogo Janja ambapo katika kufatilia sababu inaonekana ni yale maneno ambayo Young Dee aliyaongea yaliyokuwa yanamuhusu Dogo Janja na Young Killer Msodoki kuwa yeye (Young Dee) ni mkubwa kimuziki hivyo hataki kabisa kusikia watu wakimfanisha na wasanii hao wawili ambao kwake anawaona bado wachanga hawajamfikia kiwango chake. Young Killer alinyamzaza na hajaonekana kuongea chochote kuhusu ili lakini Dogo Janja hakuweza kuvumilia na kuamua kujibu maneno ya Young Dee na kumwambia kuwa hata yeye hawezi kulinganishawa  msanii kama yeye ambae anavuta unga, kabisa hawezi kuongea na ‘mteja’.

Bifu limeendelea na kuwa kubwa mpaka baadhi ya wasanii waliamua kuingia nakuwashauri kuyamaliza mambo hayo, kati ya wasanii hao ni pamoja na Nikki wa Pili.Lakini jana msanii wa muziki wa singeli Sholo Mwamba nae aliamua kufunguka kuhusu bifu ilo huku akiamua kumwaga ubuyu hadharani kuhusu sababu ya wasanii hao kugombana ni mwanamke.

Akiongea na eNews ,Sholo Mwamba ambae alikuwa chini ya menejiment ya Muna Entertainment alifunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye na Muna hawafanyi kazi pamoja na sababu sio kwamba yeye alichokwa na Muna bali yeye alimchoka Muna, alipoulizwa sababau ya yeye kumchoka meneja wake alijibu “Kitu ambacho mimi kiliniuzi na nilikichoka kwa Muda ni kitendo cha sisi wanaume kufanya kazi na kutafuta ela  afu tukienda pale  kwa muna tunakuta madogo wengune wamekaa kwenye makochi wamejiachia, sisi wahuni tunaenda kuimba visingeli vijijini tunaleta mpunga kwa bosi alafu bosi anatumia na wajinga”aliongea Sholo Mwamba

hapo wote vingasti tu, tunawakuta pale kwa bimkubwa wanajiachia achia tu, Dogo Janja, Young Dee, wanagombana wanagombania demu, ila sisi tunakuja kwa bosi tunawakuta hayo mambo ya kugombana ni miyeyusho tu” aliongezea Sholo Mwamba

Hata hivyo Sholo pia anaonekana ana wivu wa mapenzi kwa Muna Love na kufikia hatua ya kusema ” namshangaa bosi si angenipa hata mimi, akinipa sisemi, tunakula kimyakimya”