Tundaman- Bob Junior Ni Mtoto Mdogo Sana Kwangu

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Tundaman ameibuka na kumtolea povu zito msanii mwenzake Lakini pia producer wa muziki Bob Junior na kudai ni mtoto mdogo sana.

Tunda man ni moja kati ya wasanii ambaye ameshawahi kufanya vizuri sana siku za nyuma na kazi zake lakini kwa muda mrefu amekuwa kimya na hajasikika akitoa ngoma na Ametaja Sababu kuwa ni ndoa yake na mtoto wake.

Baada ya kimya kingi Tunda amerudi kwa kasi ya ajabu kwani wiki iliyopita aliachia ngoma zake tatu mfululizo pamoja na video zake kwenye kipindi cha Friday Night Live.

Lakini baada ya tukio hilo Bob Junior ameibuka na kudai kitendo cha Tundaman kutoa video tatu kwa mkupuo mmoja ni kukurupuka bila kuangalia hali ikoje.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Tunda man amemjia juu Bob junior na kumuita bwana mdogo sana kwake kwaiyo hawezi kumwambia kitu:

Mimi na Bob Junior ni vitu viwili tofauti Kwanza mimi nimeanza kufanya Muziki muda mrefu Bob Junior kaja juzi juzi tu hapa 2009 sijui 2010 kwaiyo Kwenye muziki hawezi kunishauri kitu chochote kikaendana na mziki wangu ni bwana mdogo sana kwangu”.

 

 

Tunda Man Akumbwa na Kashfa ya Utapeli

Msanii wa kizazi kipya akitokea tip-top amekumbwa na tuhuma za utapeli baada ya msanii mmoja chipukizi kudai kuwa alimpa ela zake za urithi na kujikuta akikosa faida ya ela hizo alizokuwa nataka kuziwekeza katika muziki.

Chipukizi huyo anaejulikana kwa jina la Asala, amesema kuwa wakati anakutana na Tunda ,Man alikuwa na ela za urithi alizokuwa amepewa na familia yake baada ya wazazi wake kufariki  na kutaka kuwekeza katika muziki hivyo aliamua kumfata  Tunda Man ili aweze kumsaidia kuwekeza katika musiki.Asala anasema kuwa hata baada ya kumkabithi Tunda Man ela walitoa nyimbo moja tu iliyokwend kwa jina la subiri na baada ya hapo hakuna kilichoendelea.

Sitaki kabisa kumsikia kwa kile alichonifanyia, kanipiga sana ela zangu za urithi  kwa kujifanya meneja wangu lakini kumbe alikuwa amepanga kunitapeli.

Kuna pesa milion 3 nilimpatia  kwa ajili ya muziki wangu  lakini mpaka sasa sielewi chochote   hata nikimpigia simu utasikia subiri, subiri tuu.

Hata hivyo baada ya kuongea na Asala, waandishi waliamua kumtafuta Tunda Man mwenyewe ili aweze kujibu mashtaka hayo ambapo alionyesha kushtushwa na habari hizo na kusema hajui chochote kuhusu hicho.”hilo swala ndio nalisikia kwako,wala mimi sijamtapeli mtu hiyo milioni 30″.