Zari Amshauri Diamond Atumie Kinga

Mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda Zarinah Hassan Zari The Bosslady ambaye pia ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amemtaka Ex wake huyo kutumia kinga.

Zari alishaweka wazi siku za nyuma kuwa alimshindwa Diamond kwa sababu ya Michepuko yake na kupelekea kumtosa siku ya wapendanao Miezi michache iliyopita.

Kupitia Citizen TV, Zari alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe kwa wanaume wote wasaliti kutumia kinga ili kutowahatarishia maisha wapenzi wao. Zari alisema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa la sababu hasa iliyomfanya kutangaza kummwaga Diamond.

Zari alieleza kwamba, mwanamke hawezi kumzuia mwanaume kusaliti, lakini kama mwanaume ameshindwa kujizuia na anapaswa au ameamua kufanya hivyo, basi angalau atumie kondomu katika tendo la ndoa.

Kwa wanaume, sisemi kwamba wawe wasaliti kadiri wawezavyo, hapana, lakini kama wanataka kufanya hivyo, wajaribu kutumia kondomu kwa sababu siyo kwamba watapata watoto wasiotarajiwa tu, lakini pia wataishia kupata HIV na magonjwa mengine ya kuambukiza (STD’s).“Siyo hayo tu, lakini pia wasipotumia kondomu watawapelekea magonjwa wengine (wapenzi wao) wanaowasubiria nyumbani”.

Zari alikazia mkazi sana kwenye suala la kutumia kinga unapoenda kuchepuka kwa sababu Diamond hakutumia kinga yoyote ambayo ilisababisha kumpa mimba Hamisa wakati yupo na Zari.

Zari Ampa Za Uso Mwanaume Aliyetaka Kumuhonga Gari

Mwanamama mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amempa makavu ya Uso msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya Ringtone Apoko.

Tangu Zari aachane na Diamond Msanii huyo amekuwa akiyuka mtandao wa kijamii kueleza kuwa anampenda sana Zari na yupo tayari kwenda kutoa mahari Uganda ili amuoe.

Lakini wikiendi iliyopita aliibuka na jipya baada ya kusikia Zari anaenda Kenya aliwatuhumu ajili ya Tamasha kwani alidai ameamua kumnunulia gari aina ya Range Rover Sport ambalo alienda nalo mpaka kituo cha redio alipokuwepo lakini alimkosa.

Baada ya kumkosa Kwenye studio hizo Ringtone aliandika Kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa Zari akachukue zawadi yake hiyo aliyomnunulia.

Baada ya taarifa hizo kusambaa sana Kwenye mitandao ya kijamii Zari alifunguka Kwenye mahojiano na Kiss Fm na kusema hamfahamu mtu huyo na hajawahi kuwasiliana naye hivyo hawezi kupokea kitu chochote kutoka kwake:

Simfahamu huyo Ringtone na sijawahi kukutana naye, ndio mara ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Nina watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wananifuatilia, siwezi kujua nani kunifuata na kwa wakati upi”.

Lakini pia Zari aliweka wazi kuwa hana shida ya Range Rover maana wiki iliyopita ametoka kujinunulia Range Rover Sport mpyaa hivyo yuko vizuri.

Zari- Nilimpenda Sana Diamond Lakini Alinivunjia Heshima

Mwanamama na mfanyabiashara maarufu sana Kwenye mitandao ya kijamii Zarinah Hassan maarufu kama Zari The Bosslady  amefunguka kuhusu uhusiano wake na Ex wake Diamond na kudai alimpenda sana lakini dharau zilizidi.

Zari alifunguka hayo alipokuwa nchini Kenya kwa ajili ya Tamasha lake la The color purple concert aliloenda kuhudhuria mwishoni mwa wiki iliyopita.

Zari alipohojiwa na Kiss Fm ya nchini Kenya kuhusu uhusiano wake na Diamond aliweka wazi kuwa alimpenda sana kijana huyo lakini alikuwa anafanya vitendo vingi vya kumkosea heshima.

Nilimpenda sana Diamond na kila mtu anajua kuwa Nilimpenda na tukapata watoto wawili wazuri lakini mwanaume anapoanza kuchepuka na wanawake wengine ipo hiyo lakini anapoanza kufanya vitendo vya kukukosea heshima hapo ndipo niliposema basi inatosha”.

Lakini pia Zari aliweka wazi kuwa moja kat ya vitu vilvyisababisha yeye kuchoshwa kabisa ni alivyoanza vitendo vibaya Kwenye mitandao ya kijamii kama kuonekana na wanawake wengine na kusababisha yeye na watoto wake kutukanwa na kudharaulika.

Zari alimpiga kibuti Diamond mapema mwaka huu siku ya Valentine’s Day Kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya video za Diamond na Wema kusambaa wakikumbatiana.

Diamond Asisitiza Kuwa Nillan Ni Mtoto Wake Sio Wa Ivan

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kuuanika ukweli wazi kabisa kuwa Nillan ni mtoto wake na sio mtoto wa Marehemu Ivan Semwanga kama wengi wanavyodai.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi zinazodai kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond ambapo ilidaiwa kuwa Zari alichepuka na Ivan kipindi yuko na Diamond ndio akamzaa Nillan.

Diamond ameamua kuzima kabisa tetesi hizo na kuanika kuwa Nillan ni mtoto wake na kuwataka mashabiki wasilete uchonganishi Kwenye familia yake hasa kwa wanaye.

Siku ya jana Mama Diamond aliposti picha ya Baba Diamond akiwa amembeba Diamond wakati mdogo na Diamond alikomenti kwenye picha hiyo kuwa anataka aonganishe picha hiyo na ya Nillan ili watu waone jinsi walivyofanana na kuacha kusema yule sio mtoto wake.

 

Dah hii picha nilikuwa naitafuta sana…kuna picha moja nimembeba Nillan kama hivyo nilikuwa nazimix niwawekee maboya wanaokazana kusema Nillan sio mwanangu…mxiew”.

Lakini pia Diamond alimtolea povu zito shabiki na kumta asimgombanishe na watoto wake:

Usiniletee uchanganishi na matimu yenu kwa wanangu…watoto wote ni wangu Tiffah, Nillan, Dylan… hivyo yaani”.

 

Msanii Ringtone Azidi Kumlilia Zari Atangaza Kumnunulia Range Rover

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya Ringtone Apoko amezidi kulilia penzi la Zari The Bosslady ambapo siku ya jana ametangaza kumnunulia gari aina ya Range Rover.

Siku za nyuma Ringtone alishawahi kutangaza penzi lake kwa Zari na hata kuhahidi kumuoa huku akidai anahitaji mwanaume ambaye ni mcha Mungu na aachane na Diamond.

Siku ya jana Zari alitua nchini Kenya tayari kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la hisani linaloitwa Colour Purple Concert lililoandaliwa na litakalofanyika tarehe 12.

Baada ya Ringtone kupata taarifa kuwa Zari anatua nchini Kenya mara moja alimjulisha akifika atakuta gari lake Range Rover limeshanunuliwa na linamsubiri.

Siku chache zilizopita Zari alijinunulia Range Rover Sport lenye thamani ya shilingi milioni 175 lakini pia aliweka wazi kuwa kuna msururu mrefu wa wanaume wanaotaka kuwa naye.

Zari- Kuna Foleni Ya Wanaume Wanaonitaka Lakini Mimi Sipo Tayari

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amefunguka na kudai kuna wanaume kibao wamepanga foleni wako tayari kuwa naye lakini yeye mwenyewe ndio hayuko tayari.

Zari alitokwa na povu hilo siku chache zilizopita baada ya kudaiwa amenunua gari lile ili amrushe roho Diamond na hata kudaiwa upweke alionao ndio unamsumbua na hata kudaiwa kuwa amekosa mwanaume wa kumhonga na kuwa naye.

Siku chache zilizopita Zari aliweka wazi kuwa amenunua gari jipya aina ya Range Rover Lakini mara tu baada ya hapo timu za Instagram zilimjia juu na kumsema kuwa ameazima tu gari lile ili amrushe roho Baba watoto wake na kudai hapo alipo ana upweke wa ajabu.

Zari alitumia mtandao wa Snapchat kuandika  ujumbe ambapo aliweka wazi kuwa hana upweke na wala hana shida ya  kuwa na mwanaume kwa sasa maana wapo wengi wanaomtaka:

Oooh anajinunilisha magari kwa sababu hana raha, Hapana sio kweli Nipo Single kwa sababu nimeamua kuwa hivyo kwa sasa foleni ya wanaume wanaotaka kuwa na mimi ni kinda sana lakini kwa sasa sitaki mtu nikiwa tayari nitakuwa na Mahusiano lakini kwa sasa ni mimi na watoto wangu tu”.

 

Zari Anunua Ndinga Lenye Thamani Ya shilingi Milioni 172

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan amethibitisha kuwa yeye ni Bosslady kweli baada ya kuweka wazi kuwa amenunua gari aina ya Range Rover lenye thamani ya shilingi milioni 171,337,500.

Zari alitangaza mpango wake wa kununua gari hilo wiki chache zilizopita na hatimaye wikiendi hii alilianika gari hilo jipya na kuliweka Kwenye mitandao ya kijamii.

Mara baada ya kuweka gari hilo kuna habari zilizuka kuwa amenunuliwa gari hilo na mpenzi wake taarifa alizozikana na kuweka wazi kuwa amenunua gari lile kwa hela zake mwenyewe.

Lakini pia Zari ameweka wazi mipango yake ya kuanzisha Food franchise kama vile KFC au McDonalds.

Zari Amkumbuka Agness Masogange Amefunguka Haya Kuhusu Kifo Chake

Kifo cha Video Vixen na msanii wa Bongo movie Agnes Gerald maarufu kama Masogange kimewagusa wengi hasa kwa sababu alikuwa mrembo mdogo tu.

Moja kati ya watu walioguswa na kifo hiko ni Baby mama wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ambaye amemlilia marehemu Agnes Masogange.

Zari ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambao ameonesha kuguswa na msiba huo ambao amekiri kuwa alikuwa anafahamiana na marehemu ingawa hawakuwa marafiki sana lakini alikuwa mtu wa kumsalimia na kumjulia hali.

 

Zari Adai Hawezi Kudate Mtanzania Tena, Adai Mwanaye Sio wa Tandale

Mfanyabiashara maarufu na baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameibuka na kuapa kuwa hataweza kutembea na mwanaume wa Kitanzania tena.

Zari ameyasema hayo baada ya Kupitia kipindi Kigumu na Ex wake Diamond ambaye alichepuka sana kipindi cha Mahusiano yao ya miaka minne hadi kufikia hatua ya kuzaa nje.

Zari alimwaga Diamond mapema mwaka huu siku ya wapendanao baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Lakini pia Zari ameibuka na kudai kuwa mtoto wake  Tiffah sio wa Tandale hii iliyokea siku chache zilizopita wakati Zari na marafiki zake walipokuwa Kwenye Instagram live.

Zari alifunguka na kusema mtoto wake Tiffah anashindwa kutofautisha kati ya R na L tabia ambayo ameirithi kutoka kwa Upande wa Baba yake kwani Watanzania wengi hawawezi kutofautisha R na L na wengi wao wanamuita Zali badala ya zari.

Ndipo mmoja kati ya marafiki wa Zari alisema Tiffah ni wa Tandale Lakini mara moja Zari alikataa na kusema mwanaye sio wa Tandale.

Tandale ndipo Diamond na familia yake walipokulia na hajawahi hata mara moja kukataa asili yake na hata albamu yake inaitwa ‘A boy From Tandale’.

Dj Rasta Bob Wa Uganda Adai Zari Alikuwa Mpenzi Wake Kabla Hajamuacha na Kukimbilia Wanaume Matajiri

Dj na mtangazaji maarufu nchini Uganda Robert Ogwel maarufu kama Dj Rasta Bob Mc amefunguka na kudai Ex wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari alikuwa mpenzi wake kabla hajamuacha na kwenda kwa Ivan.

Dj Rasta Bob alimwaga ubuyu huo Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kituo cha Spark Tv nchini Uganda ambapo alidai yeye ndio alikuwa mwanaume wa kwanza kuwa na Zari.

Dj huyo amefunguka na kudai kuwa yeye ndio alimtoa Zari kwao Jinja na kumleta jijini Kampala nchini Uganda kutokana na kuvutiwa na urembo wake lakini pia amedai kuwa yeye ndio alimfunza mambo mengi Zari kuhusu ustaa kwani kipindi hiko alikuwa maarufu sana.

Lakini pia amedai muda mfupi baada ya kuwa wa mjini na kupendeza ndipo Zari alivyomtosa na kuanza kutoka kimapenzi na mwanaume tajiri ambaye ni Ivan na kumwambia anaweza kuishi mwenyewe mjini na kumuacha solemba.

Dj Rasta ambaye ni mkongwe nchini Uganda katika sekta ya burudani amekiri pamoja kuwa Zari amefanikiwa kimaisha na kutoka na wanaume matajiri lakini watambue kuwa yeye ndio alimtoa kijijini na kumfundisha kila kitu kuhusu kuishi mjini.

Irene Paul Azidi Kumwagia Sifa Zari

Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul amezidi kumiminia sifa Zarinah Hassan ‘Zari’ na kudai mrembo huyo anajua kutengeneza jina lake na pia anajua kufanya biashara.

Irene Paul amewataka wasanii wenzake waache kumuonea wivu Zari kwa Dili alilolipata la Softcare na badala yake wajiulize wanafanya nini ili hata kampuni kubwa ziwaangalie wao wanawake Kwanza.

Lakini pia Irene amedai kuwa Zari ni staa mkubwa sio tu nje ya Bongo bali hata nchini kwetu na kudai hajaona bado hajamfikia kwa uwezo wake wa kuweza kuwa kiwango cha juu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Irene alizidi kumiminia sifa hizo Zari na kusema yafuatayo:

Ni staa mkubwa, anajua kumaintain jina lake, simuoni staa wa kumshinda yeye Bongo”.

Wiki iliyopita Zari alipata dili na kampuni ya Softcare kwa ajili ya kuwa balozi wa bidhaa zao za pampasi kitendo kilichowakera watu wengi baada ya kampuni hiyo kumpa dili hilo Mganda wakati kuna Madura staa wa kibongo kibao wangeweza kuwa mabalozi.

Natafuta Pesa Sina Muda wa Kutafuta Mpenzi Mpya- Zari

Zari ameibuka na jipya tena huku safari hii akisisitiza kuwa wale wanaume wakware wote waliopanga foleni kusubiri penzi la Zari hawana nafasi kwani hana muda wa kuwa na mpenzi kwa sasa.

Zari alitangaza kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, mwezi uliopita lakini tangu hapo Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya Zari kupata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi ya Diamond.

Kupitia kurasa yake ya SnapChat siku ya jana Zari ameweka wazi kuwa haitaji mpenzi kwa sasa baada ya marafiki zake kumtumia ujumbe uliosema “Kama mwanaume wako akienda kutafuta vimada  wenye msambwanda mpya inabidi umkumbushe kuwa na wewe msambwanda wako mpya kwa mwanaume mpya”.

 

Zari amedai kuwa marafiki zake wanamtumia meme hizo kama vijembe kwa EX wake lakini amejibu kuwa hataki mwanaume mpya kwa sasa:

Marafiki zangu siwawezi hivi kwanini wamekazana kunionyesha hizi Mambo lakini hazinifai mimi….. Nahitaji kutafuta pesa mpya na sihitaji mwanaume kwa muda huu samahani!!!!”.

 

“Naenda South Africa Kama Kazi Hawezi Kunikataza Mtu”- Mama Diamond

Mama mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra ametoa povu zito na kusema anaweza kwenda South Africa muda wowote akitaka kwenda kuwaona wajukuu zake na hawezi kukatazwa na mtu.

Mapema mwaka huu Zari the Bosslady alimpiga kibuti cha maana aliyekuwa mpenzi wake na  Baba watoto wake supastaa wa Bongo fleva Diamond siku ya Valentine’s baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Baada ya kuachana Diamond alienda South Africa kwa ajili ya maandalizi ya Albamu yake lakini cha ajabu ni kwamba hakufika kwenye nyumba aliyonunua aliyokuwa anaishi na Zari na watoto na Tena hakufika hata kwenda kuwaangalia watoto wake.

Baada ya sakata hilo kutokea habari zilianza kusikika kuwa Diamond na familia yake na mama yake mzazi hawatakaribishwa tena kwenye nyumba ya South Africa hasa kwa sababu wamejenga ukaribu na adui namba moja wa Zari, Wema Sepetu.

Siku ya jana Bi. Sandra alitoleana povu na shabiki baada ya kumuuliza kwanini hapendi kumposti mjukuu wake wa Hamisa au anamuogopa Zari kwa sababu hataruhusiwa tena kwenda South Africa kuwaona wajukuu wake? Basi bwana povu la Mama Diamond lilikuwa hivi:

South Africa naenda kama kazi kwa taarifa yako na siwezi kukatazwa na mtu yoyote”.

Zari alishasema Kwenye Interview aliyofanya na BBC Swahili kuwa hana tatizo na familia ya Diamond kwani muda wowote wakitaka kuona watoto wao wanakaribishwa hata Diamond akitaka kuona wanaye.

Wema: Zari Alimuacha Diamond Kwa Mambo Aliyomfanyia Huko Nyuma Sio Kisa Mimi

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema anaamini Zari alimuacha Diamond kwa mambo yao waliyotofautiana kipindi cha nyuma lakini sio kisa yeye alimkumbatia.

Baada ya Zari kutangaza kumuacha Diamond alifanya Interview na BBC Swahili na aliweka wazi kuwa amemuacha aliyekuwa mpenzi wake supastaa wa Bongo fleva Diamond kwa sababu ya yeye kukumbatiana na Wema kwenye party.

Wema na Diamond walikuwa pamoja kwa miaka kadhaa huko nyuma na wamekuwa na tabia ya kuachana na kurudiana hata Diamond amedaiwa kuchepuka kwa wapenzi wake wapya na Wema hivyo alivyoonekana tu Wema wanakumbatiana ikaonekana tayari.

Lakini Wema amekataa tuhuma za Zari kuwa amemuacha kisa yeye Kwenye Interview aliyofanya wikiendi iliyopita na Bongo 5 Wema Alitalia maneno haya juu ya suala hilo:

Zari alikuwa ana sababu nyingi sana za kupanick za nyuma za Diamond za mambo yao wenyewe lakini sio hiyo ya juzi ya mimi kumkumbatia Diamond kama rafiki atakuwa ana jingine”.

Lakini pia Wema aliweka wazi kuwa pamoja na yeye na Diamond wameachana kipindi kirefu kilichopita lakini bado wana chemistry ambayo haiwezi kuisha.

Wema alipotakiwa kumshauri kitu chochote Zari alifunguka na kusema kuwa hawezi kuwa mshauri wa Zari kuhusu Mahusiano yake na Diamond.

Zari Kuja na Reality Show Yake Itakayoitwa ‘The Life Of ZaritheBosslady’

Socialite na Mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari the Bosslady’ Zari ameongelea mipango yake ya kuja na Show yake mpya itakayohusu maisha yake ya kila siku itakayoitwa Life Of ZaritheBosslady.

Hii sio mara ya kwanza kwa Zari kufanya reality show aliwahi kuwa na reality show kipindi cha nyuma wakati yupo na Ivan iliitwa Boss lady na ilirushwa katika kituo cha televisheni cha nchini Uganda UBC.

Mara ya kwanza Zari alidokeza ujio wa Show yake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

Its coming #Yellowdot…Soon you will be able to watch mini videos of me. All you have to do is to click the link on my bio I will be posting life of Zari the Bosslady m…. you can subscribe yearly or monthly…stay tuned”.

Lakini pia Zari aliongelea Show yake hiyo kwenye mahojiano aliyofanya na BBC Swahili ambapo alifunguka kuwa tangu ameachana na Diamond amekuwa busy sana na Show yake kiasi ya kwamba hajajua kumfikiria.

Siku ya jana pia Zari aliwaambia mashabiki zake kuwa Kupitia kipindi hiko atawafundisha jinsi ya mpango wa kando wa mwanaume kwa miak tisa ambayo lilikuwa wazi ni dongo kwa Hamisa.

“Unajiona Mzuri na Mdogo Lakini Huwezi Kupata Mwanaume Wako” Zari Amrushia Hamisa Dongo

Mfanyabiashara na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amerudi tena kwenye headlines baada ya kumua kufumua bifu lake na baby mama mwingine wa Diamond, Hamisa Mobetto.

Inaelekea bifu la wazazi wenza wa Diamond  limerudi upyaaa kwani Zari kaamua kulianzisha tena baada ya kimya kirefu juu ya suala hilo na tofauti tulivyodhani kuwa huenda wamemaliza tofauti zao kama ambavyo Diamond na Hamisa walivyomaliza mahakamani.

Siku ya jana Zari kutumia mtandao wa SnapChat alimrushia Hamisa madongo upya kama ilivyokuwa siku za nyuma ambapo ameongelea kuhusu suala la Hamisa kuzaa na Diamond na pia taarifa za Hamisa kuchumbiwa na Diamond.

Siku za nyumba Hamisa ameshawahi kudokeza kuwa aliwahi kuchumbiwa au kuvalishwa Pete ya uchumba na Diamond na hata kuna taarifa zilienea kuwa huenda Diamond na Hamisa walifunga ndoa habari ambazo hazijawahi kuthibitishwa.

Mzuri, Mdogo lakini pamoja na hayo yote huwezi kupata mwanaume wa peke yako…..Eti amekuvalisha pete ya uchumba lakini hajawahi kukubali wala kukukubali hadharani! Dada jiangalie sana ….Anafanya Interview redioni eti mwenye mimba atoke blah blah”.

 

Lakini ni pia Zari ametangaza ujio wa kipindi chake kitakachoonyesha maisha yake halisia (reality show)  kitakachoitwa Life of Zarithebosslady ambacho mashabiki wake watapata kuona kila kitu kuhusu maisha yake.