Zari Amtolea Nje Msanii Kutoka Kenya Aliyejitolea Kumuoa

Mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda aliyeweka makazi yake nchini South Africa Zarinah Hassan ‘Zari the Bosslady’ ambaye pia ni baby mama wa msanii Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanaume wowote kwa hivi sasa.

Zari amefunguka hayo alipokuwa anafanya mahojiano na BBC Swahili London, Uingereza ambapo alifunguka mengi kuhusiana na mahusiano yake na Diamond lakini pia aliongelea mipango yake ya mbeleni kimapenzi hasa.

Wiki iliyopita msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya anayejulikana kama Ringtone alifunguka na kuweka hisia zake hadharani juu ya Zari baada ya kusema anataka kumuoa na hata kuongeza kuwa yupo tayari kupeleka ng’ombe 42 nchini Uganda kama mahari baada ya Diamond kumzalisha watoto na kushindwa kumuoa.

Tangu Zari aachane na Diamond kumekuwa na tetesi nyingi kuwa anatoka na wanaume kadhaa hasa kumekuwa na mwaname anayeitwa Mr. X ambaye ilisemekana kuwa alichukua nafasi ya Diamond lakini Zari amezima tetesi hizo zote baada ya kusema hana mpenzi na hahitaji kuwa na mtu yoyote kwa sasa:

Hapana sitafuti huwa na mahusiano, mapenzi yakitokea yanatokea kwa hivyo siwezi kusema sitakuwepo kwenye mahusiano tena ila kwa sasa najiangalia mwenyewe na maisha yangu na watoto wangu kwaiyo ntapumzika kwa sasa”.

Lakini Zari alifunguka na kusema kuwa ni ngumu kwake kuwa na mahusiano kwa sasa kwani hataki kuwachanganya watoto wake kwa kumuona na mwanaume tofauti kila siku. Hivyo wale wote waliokuwa wanategemea kupata nafasi ikiwemo Ringtone wakajaribu kwingine kwani Zari kasema hataki mahusiano kwa sasa.

“Sitaki Kusikia Kuhusu Diamond Wala Mama Yake”. Amesisitiza Zari Kuwa Amemuacha Diamond Kweli Sio Kiki

Zari amerudi tena Kwenye headlines za mitandao ya kijamii baada ya kutoa povu zito baada kuulizwa kuhusu uhusiano wake na Baba watoto wake Diamond Platnumz.

Uhusiano wa Zari na Diamond umekuwa gumzo kila kona tangu wiki iliyopita siku ya Valentine’s ambapo Zari alitangaza kuwa amemuacha Diamond kwa sababu ya kuendekeza michepuko.

Siku ya jana kupitia Instalive ya Instagram Zari alitoa povu kali pale alipoulizwa swali kuhusu Diamond na shabiki wake.

Zari alizungumza haya kuhusu Diamond na familia yake:

Kuna mtu kaniuliza kuwa kosa gani la mwisho ambalo Diamond alikufanyia mpaka ukaamua kumuacha? Naomba niseme mara ya mwisho kuanzia sahivi huu ukurasa ni wangu na nitaongelea kuhusu mambo yangu binafsi yaani mambo ya Zari haihusiani na Diamond wala Mama yake wala sitaongelea alichokifanya au wanawake wake malaya wake waliochoka hapana kwaiyo hapa mnaniongelea mimi na watoto wangu”.

Lakini pia Zari amefunguka na kusisitiza ni kweli amemuacha Diamond na taarifa zote kuwa ni Kiki zinazoendelea kusambaa mtandaoni sio za kweli.

Huddah Amchana Zari na Kamwambia Hana Ubosi Wowote

Socialite maarufu kabisa nchini Kenya, Huddah Monroe ameingia kwenye vita ya maneno mtandaoni tena na Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Huddah amempanga Zari na kudai anajifanya Bosslady wakati hana lolote hii imetokana baada ya Zari kuweka video mtandaoni inayomuonyesha akionyesha simu zake tatu ambazo anatumia hivi sasa ambazo ni Samsung galaxy s8, Note 5 na IPhone X.

Baada ya kuonyesha simu hizo Zari alidai kuwa yeye ni tajiri na ndio maana amenunua simu zote kali kwa wakati huu huku akionyesha saa yake aliyodai ni Rolex. Baada ya video hiyo kusambaa mtandaoni Huddah alimjibu kuwa yeye amekuwa anatumia IPhone X tangu ilivyotoka mwaka jana hivyo yeye ndio Boss.

Kupitia ukurasa wake wa SnapChat Huddah aliandika maneno yafuatayo:

Funny how people buy iPhone X after it came out long ago and social media can’t sleep…some of us have been using iPhone Z from the day it came out and we don’t flaunt small things like that because we’re used to it! Act like a boss! Tumia pesa ikuzoee”.

Zari na Huddah ni maadui wakubwa na sio mara ya kwanza kwa wawili hawa kurushiana maneno mtandaoni wamekuwa wakitofautiana mara kwa mara lakini ustajaabu kujua kuwa mara ya kwanza walikuwa marafiki wakubwa.

Zari na Huddah Enzi za Urafiki wao.

 

Zari na Hamisa Wajibu Tuhuma za Kupata Umaarufu Kupitia Kuzaa na Diamond

Wazazi wenza wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Mfanyabiashara Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ na muigizaji Hamisa Mobetto wameongelea tuhuma walizorushiwa kuwa wanapata umaarufu zaidi kupitia kuzaa na Diamond.

Hamisa na Zari wana ufanano wa kitu kimoja tu nacho ni kuwa wote wamezaa na Diamond lakini zaidi ya hapo ni maadui wakubwa kupita kiasi hilo lilidhihirika mwezi uliopita pale wote walipokuwa na shoo nchini Uganda ambapo waliishia kurushiana maneno ya kashfa mtandaoni hadi kufikia hatua ya kutukanana.

Diamond ni msanii mkubwa sana sio tu Tanzania bali hata nje ya Tanzania kwenye nchi nyingi za Africa hata nje ya bara la Africa kumekuwa na maneno mengi yanayosemwa huku watu wakidai kuwa warembo hawa wanafurahia hizi kiki za kuwa na Diamond kwani na wao wanapata umaarufu wakujulikana.

Kuna maneno yamekuwa yanasemwa kuwa Zari yupo na Diamond sio kwa ajili ya pesa bali ya umaarufu kwani inasemekana kuwa anapenda sana fame na kiki.

Zari ali[ohojiwa na Millard Ayo Tv alifunguka kuhusu tuhuma hizo kama ifuatavyo;

Naweza kusem ndiyo na hapana, ndiyo kwa sababu sahivi tumekuwa couple yenye nguvu (power couple) watu wanapenda kutuongelea sana na vitu kama hivyo hata hivyo kabla kulikuwa kuna watu walikuwa wanamjua Diamond mimi hawanijua na kuna watu walikuwa wananijua mimi na Diamond hawamjui kwaiyo nahisi tumesaidiana kujulikana”.

Hamisa naye alifunguka tuhuma hizo kwani tangu amezaa na Diamond amekuwa akisafiri nchi kama Kenya, Uganda, na Nigeria, Dubai kwenda kufanya shughuli mbali mbali:

Habari hiyo ni ya kweli kwani Diamond ni mwanamuziki mkubwa lakini mwanzo nilivyokuwa na mimba nilikuwa sijui nini kitatokea lakini tangia hapo sijapata jina kubwa tu au umaarufu lakini pia changamoto ambazo zinanilazimisha nipambane maana maisha nayo magumu”.

 

Zari Kwa Hamisa “Ulijua Kuwa Diamond Ana Familia Lakini Bado Ulimpanulia Miguu Yako”.

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ameendelea kutawala tena headlines baada ya bifu lake na Hamisa kuendelea kupamba moto mtandaoni.

Hamisa na Zari waliingia vitani wiki iliyopita baada ya kukutana nchini Uganda ambapo kila mmoja alikuwa ameenda kuhost party. Tangu wiki iliyopita wawili hao wameendelea kirushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya jana kupitia mtandao wake wa snapchat Zari amemrushia dongo jingine Hamisa huku akimtaka aachane na Diamond kwani wameshasamehana na wanapendana sana:

Ulijua wazi kabisa kuwa alikuwa ni mwanaume wa mtu  na ana familia na watoto lakini bado ukaenda kumpanulia miguu yako na kuzaa naye unafikiri hilo gundu litanipata mimi? Kwa kipi nilichofanya hilo linakurudia mwenyewe. Ukitaka rusha picha video zote za zamani hamna shida sisi tumesha sameheana tumesahau ya nyuma sahivi tunaangalia mbele  ule uchawi wote uliokuwa unamwekea unaisha sahivi amerudi katika akili zake za kawaida. Eti unajiita mtoto mdogo mimi nauzee wangu ndo namridhisha na kanikubali. Mpaka sahivi una watoto wawilo kila mmoja na baba yake hivi ukifikisha umri kama wangu utakuwa na watoto wangapi na kila baba wa mtoto anakukataa? Kwa nini unamng’ang’ania  Baba Tigfah na Nillan kwa nini sio Baba Fancy? Una wazimu”.

Zari ameendelea kumpa madongo Hamisa kwenye mitandao ya kijamii huku akimuonyesha kuwa yuko na Diamond nchini South Africa ambapo wanakula bata.

Siku Nikimchoka Diamond Namuacha Kwasababu Mimi Ni Tajiri Sihitaji Pesa Zake- Zari

Mfanyabiashara na Mzazi mwenza wa Mwanamuziki Diamond, Zari the Bosslady amekuja tena na nyingine kali akidai kuwa yeye ni mwanamke tajiri na pesa zake ivyo hahitaji pesa za mwanaume yoyote hasa Diamond kwani tayari anajiweza na endapo siku ikifika akichoshwa na matendo ya Diamond basi atamuacha na hatahitaji hata senti yake kwani yeye mwenyewe ni bosi.

Tangu mpenzi wake Diamond alipom-cheat na kuzaa na Hamisa Zari ametumia muda wake mwingi kugombana na Hamisa na kumrushia vijembe mtandaoni jambo ambalo watu wengi wameshangazwa kuwa ni kwa nini agombane na Hamisa wakati Diamnd ndio aliyemsaliti lakini jana Zari alijibu kuwa hana muda na mtu ye anaongea anachoongea kikikuuma basi ujue lako hilo.

Zari alimwaga povu hilo jana kenye mtandao wa Instagram ambapo Zari aliongelea watu ambao wanamfuata na kumuita mdhaifu kwa kitendo chake cha kumsamehe  Diamond sio kwa kutembea na mwanamke mwingine bali kwa kuzaa na mwanamke mwingine. Zari alizidi kufunguka kuwa yeye yupo na diamond sio kwa sababu ya umaarufu na pesa kama watu wengi wanavyosema bali yuko naye kwa sababu ya mapenzi aliyonayo juu yake na kudai kuwa iwapo kuna siku ambayo Diamond atamuuzi basi hatakuwa na budu bali kumuacha.

Pia Zari alimrushia dongo Hamisa kwa kitendo chake cha kuomba pesa ya matunzo ya mtoto na kudai kuwa hata siku moja hatakaaa aje ampelekee mahakamani mwanaume kwa sababu amekataa kulea mtoto wake bali ataondoka na kuenda kulea mtoto wake bila kuhitaji huduma kutoka kwa mwanaume kwa sababu ana uwezo huo. Zari aliongelea mambo ya peasa ya malezi ya mtoto kwa sababu Hamisa kampeleka mahakamani Diamond kwa sababu amekataaa kumlea mwanae aliyezaa naye anayejulikana kama Dylan.

Baba Diamond Amshauri Zari Amvumilie Diamond Kwa Mapungufu yake

Baba mzazi wa Mwanamuziki Diamond Platnumz Mzee Abdul ameibuka na kumshauri Zari aendelee tu kumvumilia Diamond kwa makosa aliyoyafanya.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Mllard Ayo Baba Diamond alipoulizwa akikutana na Zari atamshauri nini kuhusu mtoto wake ndipo aliposema kuwa atamshauri awe mvumilivu.

Baba Diamond amesema;

“Kwanza awe mvumilivu kwani mtoto wa kiume anakua mtu wa kudanganywa, mpotofu na ilimradi kashaambiwa kuna mke mwenzie basi awe mvumilivu ila kikubwa tu kuwe na heshima na adabu Zari kama Zari na Hamisa kama Hamisa waheshimiane wawe pamoja waangalie maisha tu yanaenda kama kawaida”.

Pia Mzee Abdul aliendelea kusema:

“Zari mi namwambia asipende kuwasikiliza waswahili ilimradi aangalie yake yanamwendea vizuri na Hamisa naye asipende kusikiliza ya Waswahili akae aangalie yake aendelee vizuri maana sisi waswahili kila neno linakuwa baya kwetu hamna neno zuri na mara nyingi tunakuwa hatupendani kupendeana mema mtu anapenda mwengine haaribikiwe asemwe tu, ila wakae pamoja tu waangalie haya maisha leo tupo kesho hatupo”.

Baba Diamond pia alimuomba Zari kama kuna uwezekano basi apewe nafasi awaone wajukuu zake akimaanisha Latiffah na Nilllan ambao amekiri hajawahi kuwaona kutokana na kutokuwa na  uhusiano mbovu na mtoto wake Diamond.

Baba Diamond aliongeza;

“Mi napenda kumwambia Zari nikiwa mimi kama mimi Baba Diamond aniletee wajukuu zangu kwanza niwaone au sio lazima nianiletee anaweza hata akaniambia sehemu gani naweza niweze kuenda kuwaona wajukuu zangu”.

Zari Amsamehe Diamond,Wamerudiana (picha ndani)

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu sakata la Diamond na Zari lichukue nafasi, baada Diamond kuwa na mahusiano ya siri na Hamisa kufikia hatua ya kumzalisha mtoto na kumkubali mtoto na Zari kutumia mitandao ya kijamii kudai kuwa hajamsamehe hatimaye Zari amemsamehe mpenzi wake.

Tarehe 23 jumamosi ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Zari  ambapo Diamond kwa kupitia ukurasa wake wa instagram aliweka ujumbe huu:

“Uzuri na urembo pengine ningetembea baadhi wanao pia. Lakini akili hekima pamoja na roho yako ya kwenye shida na raha kwangu ndio kitu pekee kinachonifanay nikupende na kukuthamini zaidi kadri siku zinavyozidi kuenda…wanaposema kwenye kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke imara hawamaanishsi anapika na kuosha vyombo hapaana ni mwanamke mwenyekuwa bega kwa bega na mpenziwe kwenye shida na raha…Happy birthday General”.

Siku hiyo kimya kimya Diamond alisafiri mpaka Afrika ya kusini ambako Zari yupo na kuweka picha mtandaoni akicheza na watoto wao Latifah na Nillan. Baada ya muda waliweka video na picha mbalimbali wakiwaonyesha wapendanao hao wakikumbatiana na kuweka wazi kuwa wamerudiana.

Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwa Diamond na Zari:

1. Diamond na Zari wakienda kwenye sherehe ya Zari (Birthday dinner)
2. Diamond akiwa amelala na binti yake Latifah
3. Diamond akiwa anacheza na mtoto wake Nillan (Daddy son moments)

Pamoja na hayo yote yaliyotokea Zari amekiri kuwa ameamua kumsamehe Diamond ili waendelee kulea familia yao ikiwemo watoto wa Ivan, kwani Diamond ameshakuwa baba kwao na pia Diamond alikiri kutorudia kosa tena.

Shilole Amponda Hamisa na Kumsifia Zari

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole Kiuno amefungukia suala la Hamisa na Zari na kuweka neno lake. Kama ilivyokuwa kwa wasanii wengi wametoa maoni yao juu ya jambo hili Shilole pia amefunguka na kuonyesha wazi yupo upande wa Zari na kumponda Hamisa.

Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole amefunguka kuwa kitendo alichofanya Hamisa kimewadhalilisha wanawake wote kwani  amemtumia mtoto wake kutafuta kiki.

Shilole amefunguka;

“Mwanamke asiyejielewa ndio hutumia mwili wake kujidhalilisha na kuwatumia watoto malaika wasi na kosa kutafuta kiki. Mwanaume akikupenda atakuweka ndani atakuthamini. Kinyume na hapo mtatumiana kwa maslahi yenu binafsi. Ukiwa mwizi unakuwa hata na heshima kwa mwenye mali yake ya nini mpaka udhalilishwe na mwanaume ijulikane hupendwi ila umetumiwa tu. Vinginevyo hata huduma unayopata kwa wiki utaisikia bombani. Kwani haiwezekani mwanamke kufight na kutulia na watoto wako mpaka utengeneze drama? Hebu tubadilikeni jamani huu ni u GOLD DIGGER unatudhalilisha tu. Aggh mi nakereka tu hebu niendelee na umama ntilie wangu au sijui na mimi nitafute wababa wa watoto wangu tuanza drama”.

Kwa upande mwingine Shilole amemposti Zari na kumuonyesha yuko upande wake na anamkubali yeye. Shilole kaweka picha ya zari na maandishi “Ijumaa Kareem! Mashallah umependeza wifi”.

Zari na Hamisa Wazidi Kuvurugana Kisa Diamond

Baada ya kumalizika kwa utata wa muda mrefu baada Diamond kukiri kuwa ni baba  wa mtoto wa Hamisa, mashabiki walidhani sakata hilo limeisha na halitasikika tena lakini imekuwa tofauti na matarajio ya wengi kwani picha ndo kwanza kama linaanza kwani sakata hilo limechukua sura mpya.

Zari na Hamisa ambao kwa sasa wote ni mama watoto wa Diamond wameonyeshana chuki kwa kupitia mtandao wa kijamii Snapchat,huku wakiweka wazi  kuwa tusitegemee kuwaona wakiwa marafiki mda wowote kuanzia sasa. Hamisa kwa kudhani kuwa mtoto wake Dylan ameshakuwa na undugu na watoto wa Zari na Diamond Nillan na Tiffah akaamua kuwafata (follow) kwenye instagram kwakutumia ukurasa wa Dyla lakini Zari hakufuraishwa hivo kwa kupitia Snapchat akamwambia Hamisa amuachie watoto wake na wazimu wake unahitaji kupelekwa hodi ya machizi

Kupitia Snapchat Zari aliandika;

“Laki 2 stop following my kids lol, Your obsession needs a mental institution. Like hell?”.

Baada ya kuona hivyo Hamisa ilibidi awa-unfollow watoto wa Zari na kuandika haya kwenye Snapchat;

“Na kama kuna mwanamke mwingine unampenda zaidi yangu…….Bai mwambie mzaa chema shkamoo”.

“Waambie waliopanga mwenye nyumba kaja ndani……Ana meremeta”.

Ingawa watu wengi wangependa kuwaona wanawake hawa wanapatana kwa sababu tu ya watoto wao kwani wote baba yao ni mmoja hivyo wakiwa na maelewano angalau watoto watakua wakijuana kama ni ndugu.

Zari: Majizzo ni baba wa mtoto wa Hamisa sio Diamond

Kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki  wanajiuIiza  maswali je Diamond ni  baba halisi wa mtoto wa Hamisa?Ingawa Diamond amekataa tangu mwanzoni kuwa mtoto yule sio wa kwake licha ya Hamisa kumpa mtoto jina la baba ake na  Diamond “Abdul Naseeb”.

Katika mahojiano aliyofanya Zari  nchini Uganda amedai kuwa Diamond sio baba wa mtoto wa Hamisa na amekataa mara nyingi bali baba wa mtoto ni Majizzo,  ambaye tayari ni baba wa mtoto wa hamisa, amedai kuwa sababu pekee inayomfanya majizzo  akatae mtoto ni kwasababu  anamuogopa Lulu Michael ambaye ni mpenzi wake, na pia amedai kuwa Majizzo ndiye anayemlipia  kodi ya nyumba na kumuhudumia kila kitu. Lakini  Zari amefunguka kuwa amekwisha mwambia Diamond kama mtoto atatokea akawa  wake {za diamond} basi itabidi amuhudumie na amkubali ingawa hawezi kumlazimisha kama akikataa mwenyewe.

Diamond amekuwa akihusishwa kimapenzi na Hamisa kwa muda mrefu licha ya yeye kuendelea kukataa. Hamisa  hajamuweka wazi mpaka sasa baba wa mtoto wake, licha ya kuwa kutangaza arobaini ya mtoto itakayofanyika hivi karibu ambapo bila shaka baba wa mtoto atajulikana.