Uwoya- Hakuna Wa Kuziba Pengo La Kanumba

Muogizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kudai bado hajaona msanii mwingine anayeweza kuvivaa viatu vya staa wa Bongo movie marehemu Steven Kanumba.

Uwoya amesema ameangalia sana mwenendo Kwenye tasnia hii kwa kipindi kirefu na Mpaka sasa hajaona bado msanii anayeweza kuwa hata nusu ya alivyokuwa marehemu Kanumba.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Uwoya amedai Kanumba ni staa aliyekuwa anajitoa ili kuifikisha Bongo Movies mbali, jambo ambalo hakuna anayelifanya kwa

Wakati mwingine alikuwa anatoa pesa yake mwenyewe mfukoni ili tu kufanya jambo la kuipeleka Bongo Movies mbali na kweli alikuwa ameanza kufanikiwa kuitangaza Tanzania duniani”.

Uwoya ameshawahi kucheza filamu nyingi sana na Marehemu Kanumba ambazo pia zimeweza kufanya vizuri zaidi.

Wasanii wengi wamekuwa wakidai tangu Kanumba sage dunia basi na tasnia hii nayo imelega kabisa kwani jitihada zake Kwenye tasnia zilikuwa za kweli kabisa.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.