“Vanessa Mdee ananipa stress” Lulu Diva afunguka

Mwanamziki Lulu Diva ambaye anaonekana kutamba Afrika Mashariki kupitia wimbo wake Wa utamu amedai kuwa Vanessa Mdee ni mwanamke anayempa stress kila kukicha.

Vanessa Mdee

Mrembo huyu alisema haya katika mahojiano yake na Uwazi Showbiz. Kulingana na Lulu Diva, Vanessa Mdee ndiye ni mwanamziki ambaye ameweza kupenya kwenye muziki haraka huku akipata kollabo na wasanii wa kutoka inje – kitu ambacho wasanii wa kike bado hawajaweza kufanya. Lulu alisema:

“Bongo kwa wanamuziki wa kike kiukweli anayenipa stress ni Vee, kila mtu anafahamu kuwa ni mkali na anajituma kwenye muziki wake, sasa mimi malengo yangu ni kufanya kazi kwa juhudi ili kufika mbali, kwanza kuwa hapo alipo yeye na baadaye kupita zaidi,“

Hata hivyo Lulu Diva alisema kuwa anandoto za
kufanya muziki wa kimataifa siku moja.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.