Vera Sidika na Otile Brown Mapenzi Hadharani

Socialite maarufu kutoka nchini Kenya Vera Sidika amejikuta akimwagiwa mahaba na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki pia kutoka nchini humo anayeitwa Otike Brown.

Vera Sidika alijizolea umaarufu Afrika Mashariki kutokana na umbo  lake matata amejikuta akidondoka Kwenye penzi la kijana huyo.

Wawili hao wamekuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa muda sasa na wameonyeshana mapenzi katika sehemu mbali mbali za hadhara Ikiwa ni pamoja na kuweka picha zao za kimahaba Kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini hivi karibuni Otile alianika kuuwambia ulimwengu mzima kuwa anampenda Vera kwani alimuoa Kwenye moja ya shoo zake na kumpa maneno matamu mrembo:

Nakupenda sana wewe mwanamke (Vera)… wewe ni kila kitu kwangu… na kinachonivutia zaidi kwako ni jinsi ulivyoumbika… niamini, nimewaona wanawake wengi lakini upo tofauti nao sana, wewe mvumilivu, una busara na mtu spesho”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.