“Wasanii Waache Unafiki”- Professor Jay

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva man mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amefunguka na kuwachana wasanii waache unafiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari katika siku za hivi karibuni, Professor Jay amesema kuwa unafiki kwa wasanii wengi Kwenye Bongo fleva ndio unapelekea wengi wao kukosa mafanikio mapema:

Nomba niwaombe sana Wasanii wa Watanzania, Unafiki ndio unatufikisha hapa tulipo, ukiona msanii mwenzako anaandaa kitu msapoti kwa njia zozote unazoweza kumsapoti ili kesho na wewe ukiwa na cha kwako na yeye aweze kukusapoti ingawa wasanii wa Bongo unaweza ukamsapoti ikifika zangu yako anakausha anasubiri mpaka anapokuja Tena anaomba umsapoti Tena sasa huo ni Unafiki “.

Lakini pia Professor Jay amezungumzia wimbo wake mpya aliomshirikisha Harmonize unaoitwa ‘Yatapita’ ambao una uhalisia wa maisha ya wengi ikiwemo Harmonize ambaye ameshapitia maisha magumu ikiwemo kuuza mitumba mpaka kukataliwa Kwenye BSS na sasa staa mkubwa Bongo.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.