Wastara: Milioni 43 Nilizochangiwa za Matibabu Hazijatosha na Nina Mpasuko wa Fuvu

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma ‘Wastara Sajuki’ amedai kuwa pesa ambazo wananchi na serikali ilimchangia kwa ajili ya matibabu jumla ya kiasi cha shilingi milioni 43 hazijatosha.

Wastara ambaye anasumbuliwa na matatizo ya mguu ambaye alikatwa mguu mmoja miaka kadhaa iliyopita baada ya ajali ya gari aliomba msaada mapema mwaka huu wa matibabu ambapo alichangiwa jumla ya shilingi milioni 43.

Alisafiri wiki chache zilizopita kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu na alirudi siku ya jana ambapo alipokelewa na wasanii wenzake wa Bongo movie uwanja wa ndege.

Baada ya kuwasili jana Wastara aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa pesa alizochangiwa kiasi cha shilingi milioni 43 hazikutosha hivyo amelazimika kuuza mali zake ili pesa zitimie kwa kudai madaktari wamemwambia ana matatizo zaidi ya miguu na mgongo.

Lakini pia Wastara amedai baada ya kufanyiwa vipimo kwa kina amegundulika ana tatizo kwenye fuvu lake la kichwa ambalo hilo ndilo lilikuwa likimfanya asipate usingizi bila yeye mwenyewe kujitambua.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.