Wema Sepetu Amjia Juu Soudy Brown Kisa Mama Yake

Muigizaji wa Bongo Movie Mrembo Wema Sepetu amemjia juu mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu Soudy Brown baada ya kumrekodi Mama yake.

Siku ya Jumanne kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM Soudy alimpigia Mama Wema Simu kwaajili ya mahojiano baada ya kumkosa Wema kwa Simu, Kitendo hicho cha kumpigia Simu na kumhoji Mama yake kilimkera Wema na kumjia juu Soudy.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema alimtolea povu Soudy;

“There is limits to everything…Sipendi kabisa when people involve my mother kwenye mambo ambayo hata hayamhusu…Niachie Mama yangu Soudy I don’t like when you bother her like dat only kumrecord alafu uje kumuanika like that…Hivi Soudy huna mama wa kumfanyia like that?sasa basis like da way huwezi kumfanyia mama ako basi usiwafanyie mama wa wenzako..Have some respect at least”.

Baada ya povu hilo la Wema, Soudy Brown alimuomba Wema msamaha na kukiri kosa hilo na mashabiki wa Wema pia walionesha kukerwa na kitendo hicho.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.