Wolper:Sio Kila Msanii Atapenda Ukifanya Biashara

Wasanii wengi bongo wamekuwa wakijiingiza katika biashara hasa ya mavazi na urembo kwa ujumla, Jackline Wolper nae ni mmoja wapo ambapo amekuwa akiuza nguo na urembo kwa watu mbalimbali lakini kitu anacholalamika Wolper ni kwamba wasanii wamekuwa sio watu wanaokuja sana katika duka lake kwa ajili ya kupata huduma anazotoa wakati alikuwa akitemegea kuwa wasanii ni moja ya watu wake wa karibu ambao walitakiwa kuwa  wateja wake wakubwa katika biashara hiyo.

Jackiline anasema kuwa wasanii ni watu wenye wivu sana ni bora wakanunue kitu kwa gharama kubwa zaidi kuliko kwenda kwa wasanii wenzao wakati wakijua kabisa kuwa wanakuwa wanawafaidisha wasanii hao, na anachokisema Jacky ni kuwa wengi wao wanakuwa wanawakomoa.

Wolper aliendelea kwa kusema kuwa tangu ameanza kuwa na biashara hiyo ni wasanii watatu au wanne tu ndo wamekuwa wakienda kwake kwa ajili ya kuhudmiwa , ilhali biashara kama yake haifanywi na wasanii wengi .

Unapofanya jambo lolote la maendeleo kwa sisi mastaa sio kwamba kila mtu atakuwa anapenda au anafurahi unavyofanikia.Wengi wananuna na kwaio ndio maana hawaji kukusapoti. Alifunguka Jacky

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.