Young Killer Akanusha Kumtukana Uwoya

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Young Killer ameibuka na kukana tetesi zilizosambaa kuwa alimdhihaki Msanii wa Bongo movie Irene Uwoya kwenye moja ya nyimbo zake.

Tetesi hizo zilisambaa Baada ya maneno aliyoimba  kwenye moja ya nyimbo yake kuzua utata ambapo alinukuliwa akiimba “Sishangai Hawa pimbi wakinitukana ni kawaida Kama bibi na vijana”.

Kufuatia maneno hayo kwenye verse ya nyimbo yake mashabiki wengi walidhani amemtupia dongo Dogo Janja ambaye kwa kipindi hiko alikuwa kwenye ndoa na Uwoya na walikuwa Kama na Bifu na Young Killer.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Young Killer amekanusha dongo hilo kumlenga Uwoya na kuweka wazi kuwa vijana waliooa Vibibi ni wengi sana kwenye mitandao ya kijamii.

Sikumaanisha hivyo na sidhani kama Uwoya ni bibi kwa kweli Mimi kwanza sidhani kama Irene Uwoya ni bibi wapo wengi waliooa watu ambao ni mabibi wapo wengi hata mitandaoni tunawaona usimchukulie tu Dogo Janja au namna gani vipi hebu mtoe kuna watu wengine kibao”.

Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja ilipigwa sana vita kutokana na tofauti ya kiumri iliyokuwepo baina yao ambapo Uwoya alidaiwa kuwa mkubwa kuliko Dogo Janja.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.