Yusuph Mlela Amtolea Povu Zito Steve Nyerere Kisa Mzee Majuto

Muigizaji wa Bongo movie Yusuph Mlela amemjibu muigizaji mwenzake na mwanasiasa Steve Nyerere baada ya kumtuhumu yeye na wasanii wenzake kwa kutafuta kiki Kupitia Mzee Majuto.

Steve Nyerere aliwajia juu wasanii wote walipoenda hospitali kumuona Mzee Majuto na kupiga naye picha kisha kuweka Kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutafuta kiki.

Lakini pia Steve aliwatuhumu wasanii hao kwa kuenda kumtembelea hospitalini hapo lakini hawa cha hii chochote Kwenye kitabu chake cha matibabu mwisho wa siku wanaishia kupata tu kiki.

Baada ya Tuhuma hizo, Yusuph Mlela akiwa ni miongoni mwa wasanii walioenda kumuona Mzee Majuto na kisha kupiga naye picha amemtolea povu zito Steve Kupitia kipindi cha Enews ya EATV:

Steve Nyerere ni Steve Nyerere sasa sijui alitaka akamuone mwenyewe ili hili tatizo lionekane lake peke yake sijui wakati hilo suala ni la kwetu sote lakini sijajua yeye mwenyewe alimaanisha nini maana siwezi kukaa nikaanza kulumbana naye maana nina vitu vingi sana vya kufanya lakini mimi nilifanya kwa ajili ya upendo na mzee”.

Mzee Majuto anasafirishwa wiki hii kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.