Zabibu Kiba Afunguka Mahusiano Yake na Star wa Taifa Stars

Dada wa wasanii alikiba na abdul kiba, zabibu kiba amefunguka mahusiano yake ya kimapezni na mwanasoka kutoka katika kikosi cha timu ya taifa, Abdi Banda na kusema kuwa wamekuwa katika mahusiano kwa muda wa miaka minne sasa kwa hiyo kama mwanasoka huyo ameamua kumtambulisha hadharani basi kwake haina shida kabisa.

Akielezea kukutana kwao, Zabibu kiba anasema kuwa walivyoanza mapenzi , Abdi Banda ndio alianza kumtafuta yeye kwa njia ya simu bila hata yeye kujua amepata wapi namba yake lakini alimpigia na kumuomba wazungumze kwa kuwa alikuwa na shida.

Yeye ndo alinitafuta mimi sasa sijui aliniona wapi,au nani alimuunganisha lakini alianza kunipigia simu.

Akiongelea kuhusu mwanaume huyo kufanya makala katika moja ya magazeti pendwa hapa nchini na kumtaja yeye kama mpezni wake, zabibu alisema kuwa kwake ni jambo la kherikama aliamua kuweka wazi swala a mahusiano yake na kwake halina shida lakini hawezi kwa sasa kuzngumzia swala la ndoa kwa kuwa hilo anajua yeye.

kama alinitaja sawa lakini kuhusu swala landoa siwezi kuliongelea,kwa sababu banda bado hajaja nyumbani kutoa posa.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.