Zari Amshauri Diamond Atumie Kinga

Mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda Zarinah Hassan Zari The Bosslady ambaye pia ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amemtaka Ex wake huyo kutumia kinga.

Zari alishaweka wazi siku za nyuma kuwa alimshindwa Diamond kwa sababu ya Michepuko yake na kupelekea kumtosa siku ya wapendanao Miezi michache iliyopita.

Kupitia Citizen TV, Zari alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe kwa wanaume wote wasaliti kutumia kinga ili kutowahatarishia maisha wapenzi wao. Zari alisema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa la sababu hasa iliyomfanya kutangaza kummwaga Diamond.

Zari alieleza kwamba, mwanamke hawezi kumzuia mwanaume kusaliti, lakini kama mwanaume ameshindwa kujizuia na anapaswa au ameamua kufanya hivyo, basi angalau atumie kondomu katika tendo la ndoa.

Kwa wanaume, sisemi kwamba wawe wasaliti kadiri wawezavyo, hapana, lakini kama wanataka kufanya hivyo, wajaribu kutumia kondomu kwa sababu siyo kwamba watapata watoto wasiotarajiwa tu, lakini pia wataishia kupata HIV na magonjwa mengine ya kuambukiza (STD’s).“Siyo hayo tu, lakini pia wasipotumia kondomu watawapelekea magonjwa wengine (wapenzi wao) wanaowasubiria nyumbani”.

Zari alikazia mkazi sana kwenye suala la kutumia kinga unapoenda kuchepuka kwa sababu Diamond hakutumia kinga yoyote ambayo ilisababisha kumpa mimba Hamisa wakati yupo na Zari.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.