Video Queen Agnes Akumbwa na Skendo Ya Wizi

Video Queen aliyejizolea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kukaa utupu Agnes Mmasi amekumbwa na skendo nzito ya wizi na kupelekea kuswekwa rumande.

Globa Publishers wanaripoti stori hii kutoka Kwenye chanzo cha kuaminika ambaye amedai mrembo huyo amekuwa akisota Kwenye kituo cha polisi cha Mabatini tangu Jumatano.

Mnahabari kamba Agness amedakwa kisa kutapeli nguo maeneo ya Kijitonyama? Kama hamjazidaka ni kamba alichukua kwa mkopo, baadaye akawa anamzungusha mwenye mzigo, mara amtukane hapo ndipo alipodakwa na mpaka sasa anasota nyuma ya nondo”.

Gazeti hilo lilimsaka mwanamama ambaye ndiye aliyeibiwa na Agnes ambaye alifunguka haya:

Ni kweli alichukua mzigo wa nguo, jinsi sita zenye thamani ya shilingi 90,000. Alichukua akidai anakwenda kuzijaribu na siku iliyofuata angetoa pesa, lakini aliingia mitini. Nilipokuwa nikimtafuta baadaye alikuwa akitukana na kudai hakuna ambacho ninaweza kumfanya.

Ndipo nilipomfungulia mashitaka kwenye Kituo cha Polisi Mabatini kwa jalada namba KJN/ RB/3851/I6L (matusi), akatafutwa na kutiwa mbaroni”.

Kwa muda wote huu  Agness alikuwa nyuma ya nondo, kwa hiyo hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hili.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.