Asha Baraka Awajia Juu Wasanii Wenye Asili Ya Kongo

Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka amegeuka mwiba mkali kwa kuwachamba wanamuziki Raia wa DR Congo wanaofanya shughuli ya muziki nchini kwa tabia zao za kutohudhuria misiba ya wanamuziki wenzao wasio raia wa nchi yao.

Asha Baraka aliwachamba raia hao waliofurika Ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni jijini Dar, Jumatano iliyopita kwenye msiba wa mwenzao, Erick Cantona ‘Mugogo wa Mazizini Msanii wa Bei Kali’ aliyefariki Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar.

Mkurugenzi huyo aliwatolea mfano wa kifo cha mwanamuziki na kiongozi wa Bendi ya Vijana Jazz, Abdallah Mgonahazeru ambaye msiba huo walifurika wanamuziki na wasanii wa filamu lakini hakukuwa na mkongomani hata mmoja.

Asha Baraka Atuma Maombi Kwa Mh Rais Magufuli.

Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ inatarajia kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.
Katika maadhimisho hayo bendi hiyo imeandaa tamasha kubwa la muziki wa dansi litakalofanyika 29 Septemba Ukumbi wa Club Legend (zamani Nyumbani Lounge).
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, amewaambia waandishi wa habari kwamba katika maadhimisho hayo bendi ya Twanga Pepeta itafanya shughuli mbalimbali za kijamii kama ishara ya kuwashukuru mashabiki zake.
“Tunakusudia kutembelea Hospitali ya Mwananyamala, tutatoa pia majaketi nakishi (Jacket reflectors) kwa madereva wa pikipiki, hii ni maalum kwa kumuenzi muimbaji wetu, Abdul Semwando aliyefariki kwa ajali ya pikipiki pia tutatembelea vituo kadhaa vya watoto yatima,” amesema Asha.
Mkurugenzi huyo pia ametuma maombi kwa Rais John Magufuli ili aruhusu wanamuziki wa dansi wapige muziki kama zamani zaidi ya saa sita usiku kwa kuwa muziki ndiyo ajira ya vijana wengi.
Naye kiongozi wa bendi, Luiza Mbutu amesema bendi hiyo imezuia baadhi ya waliokuwa wanamuziki wake kurudi katika bendi hiyo kwa kuwa wataua bendi walizopo.
Hata hivyo, Asha Baraka ametoa onyo kwa watu wanaoiba na kuweka nyimbo za bendi ya Twanga Pepeta kwenye mitandao yao bila ridhaa yao huku akionya pia wasanii  wanaocheza nyimbo zao mikoani  kwa kuwa wanakiuka sheria ya haki miliki.
Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.