Nimeshaumizwa Sana na Mapenzi Kwa Sasa Nipo Single-Aslay

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kudai kuwa kutokana na kuumizwa sana na mapenzi kipindi cha nyuma amechukua maamuzi ya kuwa Single kwa sasa.

Hitmaker huyo wa goma la ‘Natamba’ ameweka wazi kuwa hataki kukurupuka na kuingia Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kutokana na matukio aliyopitia kipindi cha nyuma.

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha Leo ten cha Clouds Fm, Aslay ambaye amezaa mtoto mmoja na mama watoto anayejulikana kama Tessy Chocolate, ametiririka haya.

Nilishawahi kuumia kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini mahusiano hayo hayakuwa kati yangu na mama mtoto wangu Tessy ni ya mwanamke mwingine, ndio maana kwa sasa nipo single“.

Sitaki kukurupuka kutafuta mahusino mapya kwa sababu wanawake wengine wanakupenda kwa kuwa ni msanii na wengine wana tamaa”.

Hivi sasa Aslay anafanya vyema na ngoma yake ya Kwatu ambayo inaendelea kufanya vyema Kwenye Media mbali mbali.

Aslay Apiga Show Ukumbi Ukiwa Mtupu London (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amejikuta akipatwa na fedheha baada ya shoo yake aliyopiga nchini Uingereza kukosa mashabiki.

Aslay ambaye alisafiri kwenda nchini Uingereza mwezi uliopita mwishoni ambapo alienda kupiga shoo yake.

Kupitia ukurasa  wake wa Instagram Aslay aliitangaza shoo hiyo kwa kuweka picha hii:

Kwa kuwa Aslay ni mmoja kati ya mastaa ambao wanafanya vizuri sana Kwenye Bongo fleva alitegemewa kupata mapokezi makubwa nchini humo Lakini cha kushangaza ni shoo viti aliyoipiga.

Aslay sio Msanii wa kwanza kutoka Bongo aliyepiga shoo tupu nchini Uingereza kwani mapema mwezi huu Msanii mkongwe Ray C naye alisemekana kukosa mashabiki katika shoo yake nchini humo.

Wasanii ambao wamekuwa wakijulikana kwa kujaza sana shoo zao za nje ya nchi ni pamoja na Ali Kiba na Diamond.

Aslay Atangaza Kubadilisha Staili Ya Kutoa Nyimbo

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kudai kuanzia sasa anataka kuanza kubadilisha staili aliyokuwa anatumia kutoa nyimbo zake.

Tangu Aslay atoke Yamoto Band alikuwa msanii wa kwanza kupata mafanikio makubwa hasa baada ya kuanzisha trend ya kutoa nyimbo kwa mfulululizo ambapo alitoa nyimbo mara kwa mara.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Enews cha East Africa Tv, Aslay amedai hivi sasa ameamua kubadilisha mtindo huo na kuamua kuzipa nyimbo muda anapotoa kwa sababu kuna wasanii wameiga mtindo huo.

Siwezi nikawa nafanya kitu ambacho naona watu wengi wanang’ang’ania kufanya hivyo sahivi kilichobaki nimeamua natoa wimbo halafu nasikilizia mashabiki wameupokeaje”.

Aslay amesema pia sababu nyingine ya kubadilika ni uongozi wake mpya;

Lakini pia nimebadilika kwa sababu nipo Kwenye management mpya kwaiyo nawasikiliza wanasemaje halafu siwezi nikakurupuka kama zamani kwa sababu nataka muziki wangu uende kimataifa zaidi”.

Wasanii kadhaa walionekana kuiga mtindo wa Aslay wa kutoa nyimbo mfulululizo mfulululizo ingawa wasanii hao walikiri kuwa hakufanikiwa mfano ni Msami Baby.

Aslay Akiri Kupigana Chini na Mama Watoto Wake

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amekiri kupigana chini na aliyekuwa mpenzi wake na Mama watoto wake Tessy Chocolate.

Siku chache zilizopita kuna tetesi zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wapendanao hao wameachana baada ya Tessy kufuta Tatoo aliyokuwa amechora jina la Aslay mkononi.

Hatimaye Aslay amethibitisha tetesi hizo Kwenye Interview na Bongo 5 ambapo ameweka wazi kuwa yeye na Tessy wamepigana chini na kila mtu anaendelea na maisha yake.

Ni kweli tumezinguana mimi na mama watoto wangu sahivi kidogo kila mtu anaangalia maisha yake ila mimi na yule ni ndugu tumezaa tuna mtoto wetu tunashukuru mtoto wetu anaendelea vizuri hilo ndo la maana”.

Ingawa Aslay hajaweka wazi sababu ya kuachana lakini inasemekana kuwa alichepuka kwani Tessy alishawahi kudokeza hilo kwa maneno ya mafumbo aliyoposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.