Nandy Amtaja Aslay Kama Moja ya Wasanii Wenye Fedha Tanzania

mwanadada nandy amefunguka na kusema kuwa miongoni wa wasanii wenye fedha nyingi sana tanzania basi huwezi kumsahau msanii mwenzake aslay ambae aliwahi kufanya nae kazi zaidi ya mbili za muziki.Akiongea na Times Fm katika kipindi cha the playlist, Nandy alisea kuwa huwezi kumuacha Aslay pale unapotaka kuwataja wasanii wachache tanzania wenye fedha nyingi.

Katika top five ninaweza kumuweka katika namba tatu,ingawa siwezi kutaja namba mbili au namba tatu lakini yeye namuweka katika namba tatu.

Hata hivyo alipokuwa akiendelea Nandy alisema kuwa ukiachan na Aslay kuwa namba tatu lakini ukweli ni kwamba yeye ndio namba nne inayofuata kwa wasanii wenye pesa bongo, ikumbukwe kwamba katika list ya wasanii wenye fedha iliyowahi kutolewa mwaka jana wasanii waliokuwa wakiongoza ni pamoja na Diamond Platinumz. Lady Jay dee, Dy, na Alikiba.

Aslay na Nandy Wazungumzia Wimbo Wao Uliorudiwa Zaidi ya Mara Moja.

Wasanii wanaofanya vizuri pamoja tangu walipoanza kuimba kwa kushirikiana wimbo wa kwanza wa Mahabuba na sasa wametoa wimbo mpya wa Subral kheri mpenzi Nandy na Aslay leo wamezungumzia wimbo huo ambao umetoka jana katika ofisi za Clouds Media.

Wasanii hao wawili waliamua kutoa wimbo huo kwa kuurudia kwa mara ya pila ambapo mara ya kwanza wimbo huo uliimbwa na bi  nasma hamis kidogo .na  wazo la kuurudi lilitolewa na boss wao.

Akiongea katika Power Breakfast Aslay anasema kuwa ‘huu wimbo wa subral kheri  ni mali ya culture Group  lakini huko nyuma kidogo ulishawahi kuimbwa na msanii wa taarabu bi nasma hamis kidogo , hivyo sisi tumeurudia kwa mara ya pili.

Lakini pia Nandy aliweza kuiongelea video ya wimbo huo ambayo imetoka ikiwa local sana “idea ya kutoa nyimbo katika mazingira yale alinipa aslay hata katika wimbo wangu wa kivuruge, hii ni kwa sababu nimepata majibu amzuri ya wimbo wa kivuruge ndio maana hata hii nilikubali kuifanya katika mazingira yael ingawa ilinipa ugumu katika kuuvaa uhalisia.”

Kwa upande wa Aslay yeye anasema kuwa alipokuwa Ya Moto Band alikuwa chini ya watu hivyo ilikuwa rahisi kusema anataka kufanyiwa sehemu yoyote video lakini sasa hivi anafanya mwenyewe ndio maana ameamua kurudi kule uswahilini ambapo yeye mwenyewe ametoka na anashukuru sana kwa sababu watu wanazipokea vizuri, endapo watapata ela kwa kujichanga changa wataaenda kutoa video nje.

Akiongeleaa  kuhusu  maneno yanayosambaa kuhusu bifu lake na msanii mwenzake Ruby, andy amekanusha maneno hayo na kusema kuwa watu wamekuwa wakiongea vitu vya uongo kuhusu wao lakini ukweli ni kwamba wao wako vizuri na kwa sababu wote wanafanya kazi sehemu moja ni vigumu sana kugombana.

Hata hivyo Nandy anasema kuwa wanaweza kutoa wimbo na Ruby siku yoyote ile kwa sababu wote ni watoto wa nyumba moja, na kitendo cha kuwafananisha au kuwagombanisha sio kitu kizuri na hakiwezekani. hivyo watu wasikae wakitangaza na kuzusha vitu ambavyo havina ukweli.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.