Baby J Atangaza Mapinduzi Kwenye Bongo Fleva

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika visiwa  wa Zanzibar Jamilah Abdullah maarufu kama Babu J ametangaza kufanya mapinduzi makubwa pindi atakaporudi kwenye Sanaa.

Baby J ambaye ameshawahi kutengeza nyimbo kali katika kipindi cha nyuma amekuwa kimya sana katika miaka ya karibuni.

Baby J amevunja ukimya Wake na kuweka wazi kuwa kwa sasa yupo mafichoni lakini Ana mpango wa kuibuka tena na anaamini endapo atarudi atafanya mapinduzi makubwa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  Baby J alisema kuwa ni kweli yuko kimya lakini kuna vitu anavipanga akimaliza ataibuka na kuwa vizuri kabisa.

Najua watu wengi wanajiuliza nipo wapi lakini nashukuru sana Mungu nilipojificha ni kwa ajili ya mambo mazuri na si vinginevyo”.

 

Mashabiki Wamtolea Povu Kiba, Baada ya Kumpost Baby J Badala ya Jokate

mwanadada  kutoka zanzibar amejikuta akiingia midomoni mwa mashabiki na kusemwa kuwa amekuwa akitoka kimapenzi na msani wmenzak alikiba baada ya msanii huyo alikiba kupost Baby Jay katika siku yake ya kuzaliwa na kuacha kumpost Jokate ambae alikuwa nae katika mahusiano.

Mashabiki walianza kumshutumu Alikiba na kumwambia kuwa kwanini ameweza kumpost Baby Jay na kumuacha Jokate ambae pia ilikuwa siku yake ya kuzaliwa na ndie aliyekuwa mpezni wake hata kama kwa sasa wameachana.

Katika siku hiyo wa kuzaliwa ya Jokate, watu wengi walimpost na ikitegemewa kuwa Alikiba atakuwa ni mmoja kati ya wengi watakaoweka picha na kupost kitu kuhusu siku yake ya kuzaliwa lakini haikuwa kama hivyo.

Hata hivyo katika baaadhi ya comments za mashabiki wamesma kuwa Alikiba na Baby j wamekuwa wapenzi tangu zamanikwaio inawezekana kuwa wawili hao wamerudiana na ndio maana nafasi ya jokate imechukuliwa.

 

 

 

Baby J aongelea kuhusu ndoa yake kwa mara ya kwanza

Baby J kwa mara ya kwanza ameongelea ndoa yake ambayo ilikuwa ikuzungumziwa sana mitandaoni.

Leo akiwa kwenye Clouds FM alieleza kwa nini hakuwa akiishi na muwewe baada ya kufunga ndoa.

”Wakati najiandaa kusafiri kwenda New York aliko ambako tulipanga mimi na yeye tukaishi, ilitakiwa iwe siku ya 15. Lakini ilipofika siku ya 10 mwenzangu akakamatwa huko aliko. Japo aliniambia kuwa atakamatwa, sijajua nini kilisababisha.

“Wakati anakamatwa ilikuwa saa 10 jioni baada ya muda ule sikumpata tena kwenye simu. Halafu bahati mbaya, mama yake mume wangua alikuwa amakuja Afrika kwa ajili ya harusi, so, nilikuwa niko naye. Bahati mbaya akafariki kwa mshtuko mida ya kama saa 12, na baada ya siku ya pili ndio akanipigia kujua juu ya msiba wa mama yake. Hivi na yeye alikuwa jela ikawa mtihani.

“Tunawasiliana kwa sasa hivi, ila ni mwaka wa tano toka ameshikiliwa. Halafu kipindi mwenzangu anakamatwa, mimi nipo kwenye msiba. Watu wakaanza kunitumia sms wakinisema kuwa tulikuambia, tutaendelea kupishana hapa hapa. Bahati nzuri, mwenzangua alikuwa ameniachia ujauzito mchanga, lakini bahati mbaya uliharibika kutokana na hiyo hali.

“Ninavyowasiliana na mwenzangu, ananisihi sana nivumilie. Nina matumaini japo sitaki kulizungumzia hilo.” Alisema.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.