Mwanadada Wolper amevunja rekodi kwa kununua album ya msanii Barnaba iliyotoka hivi karibuni inayojulikana kwa jina la Gold kwa dola 3000 sawa na milion 7 za kitanzania.
Hata hivyo Wolper anasema kuwa amemua kufanya hivyo kwa sababu Barnaba amekuwa akimsapoti sana yeye kipindi cha nyuma na hata kufanya show zake bure , hivyo kwake kufanya hivyo ni furaha kubwa kwa sababu naona kuwa anamsapoti mtu ambae ni kama ndugu yake.
kabla ya mimi kuwa bossy lady alikuwa ankuja na kukesha katika sho zangu bure, kwahio kwangu mimi ni mtu muhimu sana hata kununua album hiyo kwa dola 3000 ni kumsapoti mtu muhimu sana kwangu.
Katika hafla hiyo wadau mbalimbali walihudhuria kwa ajili ya kumsapoti msanii huyo.