“Mnaochonga Kuhusu Ndoa Yangu Hayawahusu”-Ben Kinyaiya

Mtangazaji wa Channel Ten na muigizaji wa Tamthilia ya Huba, Ben Kinyaiya ameibuka na kuwatolea Povu zito watu wanaoendelea kuichokonoa ndoa yake.

Jumamosi iliyopita  Ben  alifunga ndoa ya kiserikali na mwanamke wake huyo ambaye anatajwa kuwa mchumba wake wa siku nyingi, baada ya picha zao kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Ben Kinyaiya na Mpenzi Wake

Mara baada ya picha hizo za harusi kusambaa, mara moja maneno yaliibuka kutokana na muonekano wa bibi harusi ambapo wapo waliodai kuwa mwanamke huyo ni mtu mzima kuliko Ben ‘Shuga Mama’.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Ben amewajia juu watu ambao wanaiponda ndoa yake na kuwataka waache kumfuatilia kwani huo ni uamuzi wake binafsi na wala hakulazimishwa na mtu.

Wale ambao wananisema kuhusu ndoa yangu hayawahusu, maana wanaongea sana. Wapo wanaosema mara nimefuata pesa, mara ni kwa sababu nataka kwenda kuishi Uingereza, mimi hayo siyaelewi kwa kuwa wao ndiyo wanayaongea.

Mimi ninasisitiza tu kuwa wanaweza kuzungumza mambo mengi, lakini ukweli ni kwamba hayawahusu”.

 

Ndugu Wamwaga Povu Siku 7 Baada Ya Ndoa Ben Kinyaiya

Ikiwa  zimepita siku chache tangu Mtangazaji mkongwe Ben Kinyaiya Afungukia ndoa ambayo ilizua gumzo kwenye Mitandao ya kijami, mapya yameibuka kuhusu sakata hilo huku familia ikihusishwa.

Gazeti la Risasi Jumamosi linaripoti kuwa Ben Kinyaiya amejikuta akicharukiwa na ndugu wa mwanamke kwa kushindwa kumtetea ubavu wake huyo.

Kwa mujibu wa mmoja wa ndugu wa mwanamke aliyefunga ndoa na Ben aliyezungumza na gazeti hili kwa niaba ya ndugu wengine, wamechukizwa ile mbaya na kitendo cha Ben kulikalia kimya suala hilo huku kukiwa na mjadala kila kona. Alisema kibaya zaidi kwenye huo mjadala, ndugu yao amekuwa akitukanwa na kuambiwa maneno mengi ya shombo, lakini Ben amekuwa hataki kujitokeza na kueleza ukweli wa ndoa yao.

Ndugu huyo alifunguka kwamba, anaamini kuwa kama Ben angetaka ndugu yao asitukanwe kwenye mitandao ya kijamii kila kukicha, basi angejitokeza na kuanika ukweli kuhusiana na kile kinachosemwa juu ya ndugu yao.

Yaani mkeo kabisa anasimangwa kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii halafu unanyamaza?  Kama kweli mtu una mapenzi ya dhati kwake, kwa nini ufichefiche? Kwa nini asiweke kila kitu wazi maana angeweka wazi, watu wangeheshimu uamuzi wake maana inavyoonekana ni kama anataka kujifanya siyo kweli bali ni filamu”.

Ndugu huyo alisisitiza kuwa ni kweli Ben amemuoa mchumba wake huyo wa siku nyingi.

Ndoa ilifungwa pale kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Boma) jijini Dar hivyo siyo kitu cha kusema kwamba ni filamu bali ni jambo linalotambulika kiserikali. Ukweli ni kwamba Ben alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na ndugu yetu kwa takriban miaka miwili sasa.

Cha msingi yeye atuambie kama hakumpenda ili tujue kabisa maana wanaume wa siku hizi ni shida sana. Inawezekana amemuona ndugu yetu yupo kwenye maisha mazuri, akatamani maisha zaidi kuliko mapenzi”.

 

Bibi Harusi Wa Ben Kinyaiya Azua Kizaazaa

Siku ya jumamosi Mtangazaji mkongwe wa televisheni Ben Kinyaiya alifunga ndoa na ya kiserikali na mwanamke ambaye anatajwa kuwa mchumba wake wa siku nyingi baada ya picha zao kuonekano katika mtandao wa kijamii siku ya jana.

Mara Baada ya picha hizo za hatusi kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii mara moja maneno yaliibuka kutokana na muonekano wa bibiharusi ambapo wapo waliodai kuwa mwanamke huyo ni mtu mzima kuliko Ben Kinyaiya ‘Shuga Mama’.

Lakini pia kuna maneno yaliyosambaa kuwa huenda harusi hiyo ilikuwa ni muvi kwani mashabiki hawakuamini kuwa mwanamke yule Ndiye mke mtarajiwa wa staa huyo.

Hizi ni baadhi ya picha za harusi zinzaowaonyesha maharusi hao wakifurahia siku yao maalumu:

.
.
.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.