Black Pass Apata Kigugumizi Kufanya Kazi na Ebitoke.

Msanii wa vichekesho maarufu kama Black Pass ambae amepata umaarufu mkubwa kutokana na kuigiza kwake akiwa kama kiziwi na bubu amepata kigugumizi kujibu swali alilokuwa ameuliza na watangazaji wa Times Fm kuhusu yeye  kumjua ebitoke na kama anaweza kufanya nae kazi ya vichekesho  kwa sababu wote wapo katika tasnia moja.

Black Pass ambae alionekana kuwa na kigugumizi huku akijifanya ajaelewa swala aliloulizwa baadae alijibu na kusema kuwa  anaweza kufanya nae kazi lakini kwanza ni lazima apewe ruhusa kutoka kwa uongozi wake anaofanya kazi.

Mimi nafanya kazi na kampuni na kama kampuni itaniruhusu mimi nafanya kazi  na mtu yoyote na ikitokea   kama  uongozi unakubali na kuniambia nifanye nae kazi mimi nitafanya.

Ebitoke na Black Pass wamekuwa wakifananishwa  na kushindanishwa sana katika mitandao ya kijamii kwa sababu ya kazi zao , huku wengine wakisema kuwa Ebitoke ameshushwaa kiwango kutokana na uwepo wa mwanadada huyo ambae ana kipaji kikubwa katika vichekesho kuliko Ebitoke.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.