Bond:Wastara Alitaka Mafanikio ya Haraka

Aliyekuwa meneja wa msanii wabongo movies Wastara Sajuki amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimtuhumu kuwa alijiingiza kwenye mapenzi na wastara baaadae kumtelekeza sio kweli kwasababu kuna mapungufu mengi yaliyokuwepo na kushindwa kuendelea na penzi hilo.

Bond anasema kuwa  aliamua kumuacha Wastara kwa hiari yake kabisa kwa sababu Wastara alikuwa akitaka mafanikio ya haraka haraka wakati yeye kwa wakati huo alikuwa ana kitu cha kumpa.Lakini pia alichukua uamuzi wa kumuacha baada ya kuona kuwa  Wastara hana fuaraha na penzi hilo hivyo aliona ni bora ampe furaha yake kwa kuachana nae.

Mimi ndie niliemuacha Wastara na kumaua kuondoka na kwenda kutafuta maisha yangu  mengine  baada ya kuona kuwa  namkosesha amani na bado Wastara alikuwa akitaka mafanikio ya haraka haraka sana  wakati mimi uchumi wangu ulikuwa umeyumba. Alifunguka Bond.

Wastara alijiingiza katika mapenzi na meneja wake huyo baada ya kufiwa na mumewe marehemu Juma Sajuki na kuzua maneno mengi katika mitandao kutokana na ukaribu wa mwanaume huyo na familia ya Sajuki kipindi cha uhai wake, hata hivyo penzi hilo halikuchukua muda lilivunjika.

Akiongelea kuhusu swala ya yeye kuhusishwa na ujambazi nakukaa selo kwa zaidi ya siku 20, Bond anasema kuwa anashukuru Mungu kuwa polisi walifatilia na kuona kuwa hakuwa na hatia yoyote ile ingawa mwaka 2017 kwake umekuwa mgumu sana kutokana na misukosuko hiyo.

Kuhusu ishu ya kuhusihwa katika ujambazi imenitesa sana kwakweli, kwani nilikaa selo kwa siku 20 lakini nashukuru Mungu polisi  waliujua ukweli hivyo kuniachia huru. Alimalizia Bond alipokuwa akiongea na GPL

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.