Bifu Za Wasanii Zinazoendelea Bongo Zinaua Muziki

Kumekuwa na mifarakano mingi inayoendelea katika tasnia ya muziki tanzania, mara nyingine ugomvi unaokuwa unatokea unaweza kusababishwa na kitu kidogo tu ambacho inawezekana wasanii wenyewe wangekaa bila kufuata hisia za mashabiki wasimgefikia hatua ya kugombana kwa muda mrefu, wapo wanaogombana kwa sababu ya mambo binafsi yasiyohusiana na muziki.Kwa mwaka 2016-2017 zimezuka bifu nyingi na zingine zikiendelea kuongezea kadri siku zinavyozidi kwenda.Na hizi ni baadhi ya bifu za wasanii kwa mwaka 2016-2017.

1.Alikiba na Diamond Platinumz

Hakuna anaeweza kukujibu chanzo cha ugomvi wao ambao kila kukicha unachukua sura  mpya, ni ugomvi mkubwa ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kuumaliza wangeweza kukusanya mashabiki wengi kwa pamoja.

2.Diamond na Ommy dimpoz

Ni moja kati ya watu walikuwa na umoja sana walipoanza muziki, baade walikuja kutengana.Lakini bifu lilizidi kuw akubwa baada ya ommy kuungana na alikiba katika kazi hivyo Ommy akaanza kuwa upande wa Alikiba.bifu hili limeingiza hadi watu wa familia ya Diamond na inasemekana kuna kesi mahakamani kutokana na ugomvi wa wasanii hawa.

3.Young Dee,Young killer na Dogo Janja

Bifu lilianza kiutani utani lakini likazidi kukua, wasanii hao wanaona kuwa kila mmoja ni bora zaidi ya mwingine,kila mmoja hataki kufananishwa na mwingine, lakini kama wasanii wadogo wanaofanya vizuri katika sanaa walitakiwa kuungana ili kuendelea kuongeza idadi ya mashabiki.

4.Bob Junior na Diamond Platinumz

Kumekuwa tu na malalmiko ya upande wa Bob Junior kuhusu wawili hao kutokuwa na ushirikiano, ingawa anasema kuna mengi yanaendelea hapo katikati ikiwemo la wao kushindwa kukaa pamoja na kutatua tofauti zao kutokana na Diamond kutokuwa tayari, Diamond amekuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu ili ingawa Bob Juniour ndie amekuwa akifunguka kila mara kuhusu Diamond.

5.Man Fongo na Sholo Mwamba

Bifu lilianza pale man fongo alipomtuhumu Sholo Mwamba kufiksha habari za umbea kuhusu Wema Sepetu, ni mambo flani binafsi ambayo yaliwezekana kutatuliwa kimya kimya.Singeli ni muziki unaoshikakwa kasi kwa sasa Tanzania hivyo wasanii hawa walipaswa kuwa ndugu ili kukuza muziki huu.

Fahamu Warembo Waliofanikiwa Zaidi Katika Nyanja Mbalimbali Tanzania

1.Jokate mwegelo

Safari yake ya mafanikio ilianza kwa kushiriki mashindano ya u-miss .Ni mrembo  mjasiriamali anayeingia katika kundi la watu waliofanikwa hasa kupitia kampuni yake ya Kidoti,amekuwa akirudisha fadhila katika jamii kupitia sekta mbalimbali, kwanza alianza na kutoa misaada kwa wasusu mitaani, lakini pia alikuja na kampeni ya kusaidia utoaji wa vifaa vya shule kwa wasichana wanaoishi katika mazingira magumu.Jokate pia alishawahi kutoa msaada wa kujenga kiwanja cha mpira katika shule ya Jangwani.

2.Faraja Nyalandu

Amekuwa ni mfano wa kuigwa wa wasichana wengi katika jamii, Faraja ametoa mchango mkubwa sana katika sekta ya elimu kupitia project yake ya Shule Direct

3.Doris mollel

Amekuwa akitoa msaada mkubwa sana katika sekta ya afya hasa kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya umri wao(NJITI), chini ya Dorris Mollel Foundation, ameweza kutoa mashine pamoja na vitanda kwa wahitaji hao.Alianza kama Miss Singida mwaka 2014, na baadae Miss Tanzania namba tatu.

4.Flaviana matata

Mwanamitindo anayeishi nje ya nchi, safari yake ya mafanikio ilianza pale aliposhiriki Miss Universr mwaka 2007,amekuwa akisaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu chini ya Flaviana Matata Foundation.

5.Jenniffer Bash

Mrembo aliyeamua kuangalia fursa katika sekta ya kilimo, wengi wanamjua kaka mama Alaska, ikiwa Alaska ni jina la kampuni yake.aliona ni bora kushirikianana wakulima wa mashambani ili kuweza kuagawana faida na kunufaisha jamii pia.Kwa sasa kampuni yake inauza mayai, mchele na mafuta.

6.Nasreen Kareem

Alikuwa mshindi wa Miss Tanzania mwaka 2008,kwa sasa amejikita zaidi katika maswala ya urembo hasa wa asili akishirikia na wanawake wa jamii za kimasai katika utengenezaji wa bidhaa za shanga.Duka lake limekuwa ni moja ya maduka makubwa yanyotangaza bidhaa za asili.

7.Jackline Ntuyabaliwe

Ni mrembo aliyepitia vipaji vingi mpaka kufika hapa, alianza na kushirki U-misss mwaka 2000, na kuwakirisha Tanzania Miss World. Alishapita kwenye kuimba ,kwa sasa amejikita katika ubunifu.Ameshashinda tuzo ya designer bora wa vitu vya thamani.

 

Serikali Kuingilia Kati Swala La Mavazi Kwa Wasanii Hasa Wa Kike

Naibu waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na michezo Mh. Juliana  Shonza,ametangaza kuwa kuanzia sasa serikali itaanza kazi ya kuwabana wasanii ambao wamekuwa wakivaa vibaya katika kufanya kazi za za kisanii, na kutumia lugha mbaya zikiwemo lugha za matusi katika nyimbo zao.

Mh Juliana Shonza amesema kuwa kwa muda sasa wasanii wamekuwa na mchango mkubwa wa mmomonyoko wa maadili kutokana na nguo mbaya wanazovaa na lugha za matusi wanazotumia katika nyimbo zao.Akiongea alipokuwa akipokelewa ofisini hapo , Naibu Waziri huyo amesema kuwa moja ya vitu alivyoviona katika sanaa ni jinsi wasanii wanavyovaa vibaya katika kazi zao, na ilo ni swala analotaka kuanza kulishughulikia lakini pia lugha  mbaya zinazotumika katika nyimbo nalo inabidi kufuatiliwa.

“Nilipoteuliwa swala la kwanza kabisa kuliangalia lilikuwa ni mmomonyoko wa maadili kwakweli imekuwa ni changamoto kubwa sana nimeshuhudia saizi hata ukiangalia  kwenye nyimbo na kazi za wasnii  lugha ambayo inatumika  siyo nzuri,lakini kama haitoshi  kuna nyimbo zinaimbwa ukifuatalia kwa ndani unakuta  siyo mazuri,lakini hata ktika mavazi  nitawaambia wasanii wa kike  wajitahidi kuvaa vizuri,kwa sababu hatuwezi kuacha hivi vitu hivihivi vinaendelea tu , kila taifa lina  misingi yake na tamaduni zake”

Labda ni kutokana na utandazi na maendeleo yanayoendelea, wasanii hasa wa kike wamekuwa wanavaaa nguo  zinazowaacha nusu uchi swala ambalo limekuwa likichangia mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa, na baadhi  ya nyimbo zimekuwa na maneno makali ambayo inakuwa vigumu wazazi kusikiliza mbele ya watoto wake.

Lakini pia Naibu Waziri huyo amedai kuwa swala la kuulinda na kuutunza utamaduni wa taifa ni jukumu la viongozi na watu wote kwa ujumla.hivyo basi wasanii  wanapofanya kazi pia inabidi kuzingatia kuwa kazi zao zinalenga pia kutunza na kutangaza utamaduni wa taifa lakini pia lugha wanazotumika katika kazi zao zilenge kusikilzwa na watu wa rika zote na sio kubagua kundi fulani, kuna baadhi ya nyimbo zinaweza kuwa na maneno makali kiasi kwamba ni aibu mzazi kusikiliza na mtoto.

Picha 5 za Wasanii Na Watoto Wao

Wasanii wa filamu na wanamuziki wa Bongo movies kama ilivyo watu wengine wana familia na wana watoto kupitia mitandao ya kijamii mashabiki wanapenda kuangalia na kuwafatilia watoto wao na familia zao.

Leo tutaangalia wasanii watano wakiwa na watoto wao:

1. Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba ana watoto watatu wanaoitwa Kiba junior, Amiya na Sameera ambao anapenda kuwaweka kwenye kurasa yake ya instagram , hizi ni baadhi ya picha za watoto.

.

 

2. Diamond Platnumz

Mwanamuziki Diamond ni moja Kati ya wasanii ambao ni kivutio kwa watu, Ana watoto watatu wawili aliozaa na Zari ambao ni Nillan na Tiffah na mtoto mmoja aliyezaa na Hamisa Mobetto anayeitwa Dyllan.

 

3. Master Jay

Mtayarishaji wa muziki Master Jay ni moja kati ya staa mwenye watoto watatu ambao ni Catherine, Nuru na Silvia.

 

4. Aunty Ezekiel

Mwigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amezaa mtoto na mcheza shoo wa Diamond Moses Iyobo, cookie ana miaka miwili.

5. Hamisa Mobetto

Mwigizaji Hamisa Mobetto ana watoto wawili binti yake Fantansy aliyezaa na Majizo mkurugenzi wa EFM na Diamond Platnumz aliyezaa nae mtoto mdogo Dylan.

 

 

 

Mastaa Wa Kike Maarufu Na Muonekano Wa Nywele Fupi

Imekuwa fashion kwa  wanadada wengi kuwa na muonekano wa nywele fupi , tena wakionekana maridadi kabisa kuliko hata nywele za bandia wanazosuka wakati mwingine.Hawa ni baadhi ya mastaa na watu maarufu  wa kike bongo wenye muonekano wa nywele fupi na bado wanaonekana maridadi na kupendeza vizuri kabisa.

1.Nancy sumary.

Amekuwa akionekana na muonekano huu kwa muda mrefu sasa, ni mwanadada mjasirimali, muandishi wa vitabu lakini pia ni meneja wa Bongo5 Media.Ni mama wa familia lakini muonekano wake siku zote umfanya kuonekana mrembo bila kuchuja.

2.Elizabeth Lulu Michael

Amekuwa na muonekano wa kubadilika badilika katika nywele , lakini akiwa na nywele fupi uonekana vizuri zaid.ni mmmoja wa mastaa wa bongo movies anaeongozwa kwa kupendeza na kuvaa nguo ikamkaa vizuri kabisa.Huyu ndio Lulu Michael.

3.Jackline wolper

Jacky ni mmoja wa wasichana wanaovaa sana katika mastaa wa  bongo, amekuwa ni mtu anaejipenda.Kuwa na duka la mavazi pia linazidi kumfanya aonekane maridadi.yeye pia anamuonekeano wa nywele fupi ila za kwake amezitia nakshi, hii inamfanya azidi kung’ara kwa sababu ya rangi yake pia.

3.Faraja Nyalandu

Ingawa ni muda sasa tangu ashiriki mashindano ya ulimwende, lakini amekuwa ni mmoja wa wanawake wanaotunza umaridadi wao sana.Akiwa kama  mama wa familia pia Faraja amekuwa akivaa nguo za heshima, zenye kumfanya haonekane binti muda wote na kuonekana nadhifu na muonekano wake wa nywele fupi.She is always perfect!!!!!

5.Jackline Ntuyabaliwe

Ni moja wa mwanadada mwenye vipaji vingi, alianza na urembo, baadae akaingia kwenye muziki lakini sasa amejikita katika ubunifu zaidi na kampuni yake ya kutengeza vitu vya thamani chini ya kampuni ya Amorette.amekuwa na muonekano mzuri sana hasa katika nywele fupi. Huvaa simple but always looks stunning!!!

6.Shamimu Mwasha(8020 Fashion)

Inawezekana labda na kazi yake inamfanya aonekane maridani zaidi, amekuwa mwanamitindo na pia mtu ameweza kushauri wengine na kutoka kimaisha.shamimu ni mama wa familia,Mwanamitindo na mjasiriamali pia  lakini hii haifanyi yeye kuonekana toauti na wasichana warembo na wanaojipenda.

 

 

Mastaa Wakongwe Waliokataa Kuchuja Katika Muziki

Kuna baadhi ya wasanii wa Bongo fleva ambao tangu waanze muziki mpaka sana ni zaid ya miaka ishirini lakini bado wanafanya vizuri katika  muziki na wamekuwa chachu kwa wasnii wadogo ambao ndio wanachipuka.Hawa wamekuwa mchango mkubwa sana katika kuukuza muziki huu.

1.Farid Kubanda -Fid q

Fid q alianza musiki miaka ya 200,akifanya vizuri huku akiwakilisha wasanii wanaotka Mwanza.aina ya muziki anaofanya ni HipHop.Nyimbo nzake ambazo zimeshafanya vizuri hadi sasa ni pamoja na Fid q, Mwanza Mwanza,Sihitaji Marafiki, I Am a Proffessional , Roho aliyomshirikisha Christian Bella ambao kidogo alifanya totauti na vile watu walivyomzoea na hivi sana anafanya vizuri na wimbo wake wa Fresh.

2.Mr.Blue

Mr.blue alianza kazi ya muziki akiwa mdogo sana na alifikia hatua ya kugombana hata na familia yake kwa sababu ya kazi ya muziki.Wimbo wa ‘tabasamu’ ni moja ya nyimbo zilizotamba sana enzi zake, nyimbo nyingine ni pamoja na Mapozi,Tilalila,Baki na mimi, Pamoja na Pesa .Mr blue mpaka sasa ni msanii anaependwa na amekuwa mfano wa wasanii wengine wengi.

3.Proffesa Jay

Jina lake halisi ni joseph haule,  alianza muziki mnamo mwaka 1994.kwa sasa anajihusisha na siasa na ni mbunge wa Mikumi kupitia chama cha upinzani Chadema,,lakini kazi ya ubunge haijamfanya kusimama kazi za muziki.Baadhi ya nyimbo zake zilizofanya vizuri ni pamoja na Zari la Mentali, Hapo vipi, Nikusaidiaje, Mtazamo.na Aluta Kontinua.Kwa bongo alikuwa akijulikana kama kaka mkuu wa muziki wa Bongo.

4.Dully Syskes

Miaka ya 1999 dully alianza musiki , ni moja kati ya wasanii waliokuwa wanapendwa sana Tanzani ana mpaka sasa Dully bado anafanya vizuri,wimbo wake wa hi! ndio uliomtambulisha zaidi katika muziki, baadae akaja na nyimbo kama Salome,Baby Candy, na Dhahabu.Hivi karibuni aliimba wimbo aliomshirkisha Harmonize kutoa Wcb uliitwa Inde.Bado yupo katika game na anafanya vizuri.

5.Ambwene Yesaya-AY

AY amekuwa akifanya vizuri sana katika rap tangu miaka ya 1996, huyu ni mmoja wa wasanii ambao kwa sasa wanafanya muziki lakin pia ni wajasiriamali wakubwa.Unapomuongelea AY basi uwezi kumuacha Mwana FA pia.

Nyimbo kama Habari ndo iyo, Nangoja ageuke, Yule, na Usije mjini zilifanya vizuri sana katika muziki kipindi icho.Ay pia aliimba nyimbo aliyomshirikisha msanii Diamond inayojulikana kama ‘zigo remix’.Hivi karibuni AY alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake anaetarajia kufunga nae ndoa.

6.Mwana FA

Mashabiki wanamwita Binamu, alianza muziki miaka kama  15 nyuma iliyopita,Mwana FA amekuwa karibu sana na AY , na ni marafiki wanaofanya kazi pamoja kwa muda mrefu, ameshatoa nyimbo kama Habari ndo iyo, Unanitega,Nangoja ageuke, Kiboko yangu aliyoimba na Ali Kiba pamoja na Dume Suruali aliomshirkisha Vannesa Mdee.

7.Lady Jay Dee

7

Wamekuwa wakimwita dada mkuu maana ndie msanii wa kike alieduumu muda mrefu katika game, alijulikana kama Anakonda, Binti machozi, Komando Jide,na mengine mengi.Alijulikana sana kwa nyimbo zake zenye kuibua hisia kama Machozi, Siwema, Usiuseme Moyo,Siku Hazigandi,hivi karibuni amekuja na nyimbo kama Ndi Ndi Ndi na I Miss U baadaa  ya kukaa kimya kidogo.Jay Dee alifunga ndoa lakini baadaye aliachana na mume wake huyo aliejulikana kama Gadner G Habash,Ana band pia ya muziki inayoitwa Machozi Band.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.