Wasanii Watajwa kuwa Waathirika Wakubwa wa Madawa ya Kulevya.

Wasanii wa muziki na filamu nchi , watajwa kuwa dio kundi kubwa sana linaloathirika na matumizi ya madawa ya kulevya kuliko kundi lingine la watu wowote nchini.Hii imesema na Kamishna mkuu wa kupambana na kuzuia rushwa jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,

Kamishna huyo anasema kuwa , hata hivyo kiais cha kusafirisha na kuuza madawa hayo kwa sasa imepungua sana sio kama hapo awali  lakini wanaoongoza kwa kasi katika kufanya shugfhuli hizo ni wasanii.

Kmaishna huo anasema kuwa baaada ya kugundua kundi hilo ndilo linaloathirika sana wameamua kupanga mkutana na wasanii nchini utakao fanyika febraury 13 mwaka huu kwa ajili ya kuongea na wasanii huku mgeni rasmi akiwa ni mama Samia  ( makamo wa Rais ). ili kuongea nao kuhusu tatizo hilo.

 

Wasanii Walionja Selo Mwaka 2017.

Ni majaribu mengi binadamu wanakutana nayo, mengine Mungu anampa mtu ili kumpima na kuona kama anaweza kuyahimili kwa kishindo gani, lengo kubwa hapa ni kumuhaibisha shetani na njia zake,wakiwa kama wasanii yapo mengi hutokea kwao lakini haifanyi kuacha kuendelea kukonga nyogo ya mashabiki kwa sababu wao dfio wanakuwa wamekuweka hapo ulipo.

Mwaka 2017, unakaribia kuisha  na kila mtu anaweza kusema lake kwa kumshuuru Mungu kuumaliza salama punde mwaka utakapokuwa umeisha lakini hakuna anekosa cha kusimulia tena hasa anapokutana na tukio kubwa ambalo labda kwa namna moja ama nyingien imeweza kubadili maisha yake kwa ujumla au kwa kiasi fulani.

Hawa wafuatao ni baadhi ya wasanii ambao endapo watapata fursa ya kuongelea yaliyowakuta 2017, basi hawatasita kuongelea kitendo cha wao kulala selo kwa mwaka 2017, hii inaweza kuwa ni historia yAo isiyo weza kufutika kamwe.

NEY WA MITEGO

.

Ney wa mitego alikamatwa na kuwekwa ndani mwanzoni mwa mwaka huu baaada ya kuachi wimbo wake wa wapo ambao ulitafsiriwa kuwa ulikuwa unalengo la kuwakasfu viongozi waliopo serikalini.alikaa ndani kwa muda wa siku mbili.

ELIZABETH LULU MICHAEL.

Mpaka muda huu bado yupo gerezani, kesi yake ya mauaji ndio iliompeleka huko, lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuua  bila kukusudia.Akiwa msanii mwenye umri mdogo laini amepitia meng magumu, hakika mwaka huu ni mwaka mgumu kwake na familia yake.

WEMA SEPETU.

Alijikuta akiingia matatani baada ya pilika pilika z akutafut watumiaji wa madawa ya kulevya mkumbo ambao uliwanasa wasanii wengi sana katika tasnia ya filamu na muziki pia.alitok selo lakini kesi yake bado inasikilzwa mahakamani.

VANNESA MDEE

Ni moja ya wasanii wakubwa wakikie na wanaofanya vizuri tanzania na nje ya tanzania, alijikuta lock-up baada ya kutajwa katika list ya wasanii wanaotumia unga mapema mwaka huu katika kampeni iliyoanzishwa na mkuu wa mkoa.

Wasanii wengine ni pamoja na Recho, T.I.D,Petit man, na video quen Tunda.tunaamini mpaka mwaka unaisha hakuna atakaekutana na tukio baya tena.

 

 

 

Wasanii Wamshauri Lulu Kukaa Jela Atumikie Kifungo Chake.

Sio muda mrefu umepita tangu mwanadada wa bongo movies Lulu Michael kuhukumuiwa jela kwa miaka miwili jela ili kutumikia kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia  kwa msanii mwenzie  Steven Kanumba mwaka 2012.Baadhi ya wasanii katika tasnia ya muziki na filamu wameibuka na kuongea katika nyakati tofauti tofauti ushauri wao kwa msanii huyo kuhusu swala la yeye kukata rufaa.

Hata hivyo  wasanii wanaonekana kumuhurumia msanii huyo lakini  bado wanamshauri kuwa ni bora zaidi akatumikia kifungo chake chote na kumaliza kuliko kukata rufaa.Na kwa sababu kukata rufaa bila kujua hatma yako ni sawa na kukaa kifungoni bil kujua adhabu itaisha lini.

Lulu Diva.

Nikipata nafasi ya  kumshauri au kuzungumza na lulu  ningemshauri bora tu atumikie kifungo chake na akimalize tu  ili awe huru.ana kila sababu ya kutumikia kifungo icho ili kuupoza  machungu ya mashabiki wa kanumba na familia yake pia.baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo tofauti baada ya kifo hicho kuhusu yeye.

Snura:

Japo uwezekana wa  kukata rufaa inawezekana ila mimi ninamshauri sana amuachie Mungu tu  kwa kila jambao na anaejua kesho yake ni Mungu pekee.

Sandra.

Wala hasikate rufaa kwakweli kwasababu kesi ya mauaji ni kesi kubwa sana,na hata kama ataamua kukata rufaa ni mlorongo mrefu sana atapitia mpaka afanikiwe kile anachokitaka  na uwezekano wa kutokufanikiwa kwa rufaa yake ni mkubwa sana .Ni bora tu atumikie kifungo chake ili akimaliza awe huru na maisha yake mapya baada ya kifungo.

Davina;

Asikate tamaa maana kuna watu wanaona kabisa alilofanya kuwa ni kosa, hivyo ni bora zaidi akatumikia kifungo chake  kwa hiyo miaka miwili tu na baada ya hapo awe huru  na maisha yake ya kawaida yaendele kama mungu alivyopanga kuyasimamia.wala asikate ili mambo yaishe na atengenze usawa kwa watu.

Mlela.

Mimi ninamshauri tu  akabiliane na jaribu hilo ili awe huru.japokuwa jela sio mahali pazuri lakini midomo ya watu na maneno ya watu ni mabaya na yanakera zaidi .Kila linatolotokea kwa binadamu ni mungu ndie anapanga litokee na atampitisha ili awe kufika pale anapopataka yeye.

Pretty kindy:

Ni bora tu akatumikia kifungo chake, maana kwakweli baadhi ya mitazamo ya watu  katika jambo ilo ni tofauti sana.Amalize kifungo chake ili akimaliza kifungo  hakuna mtu hatakuwa na kinyongo na yeye tena.

Mary Mawigi:

Kwa upande wangu mimi naona bora tu amuombe mungu  amfanyie wepesi tu mbona miezi 18 tu.asikate tamaa  mungu yu pamoja nae.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.