Hakuna Ninaemwamini Tangu Ninyweshe Madawa ya Kulevya:-Esther kiama

Mwanadada anaefanya vizuri katika anga za bongo movies Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake amejifunza kutokumuamini mtu yoyote kwa sababu hata waliompa dawa za kulevya hakuwahi kuwadhania kama wataweza kumfanyia  hivyo.

Ester anasema kuwa maruweruwe ya kuweka madawa ya kulevya bado hayajamuisha  na kwamba pamoja na kwamba  alikwenda hospitali na kutibiwa lakini amekuwa muoga mpaka vitu vingine ninaogopa kununua dukani.Ester anasema kuwa amekuwa akiogopa sana vitu vya maji maji kwa sasa.

Huwezi amini kabisa nimekuwa muoga hata kutoka nyumbani kwangu kwa sababu hiyo,nimekuwa muoga kupitiliza kabisa  sijui huu ugonjwa utaishaje , naona nimepata ugonjwa wa kuwa na wasiwasi.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.