Niva Aomba Kuzikwa na Steve Nyerere

Msanii wa bongo movies Niva amefunguka na kutoa wosia wake na kusema kuwa anaomba endapo atakufa basi msanii Steve Nyerere ashughulikie mazishi yake,Niva ambae siku hizi ameonekana kujigamba na kuongea kwa kujiamini mbele za watu amesema kuwa kwake haina shida na anatamani sana katika mazishi yake yasimamiwe na Steve Nyerere.

Niva anasema kuwa hata  kuna watu wanamsema vibaya na kusema anakula rambi rambi kwake wala hakuna shida ilimradi azikwe kwa heshima kama vile ambavyo Steve amekuwa akijituma kufanya kazi hiyo.

Hata hivyo niva amelaani vikali wale wanaomwita na kumsema Steve nyerere vibaya  na kuwaita wapuuuzi na hawajui wanachokiongea.

Kumekuwa na maneno ya kejeli ya muda mrefu , baadhi ya wasanii wanamsema vibaya Steve Nyerere na kusema kuwa amekuwa akijihusisha katika misiba kwa ajili ya kula pesa za rambirambi.

 

 

 

 

Duma Kuja kivingine katika Sanaa,

Muigizaji maarufu hapa nchini kwa upande wa wanaume Daudi Michael Maarufu kama “Duma” anatarajia Kuachia Filamu yake Mpya mwanzoni mwa mwezi wa 8, ikiwa ni moja kati ya kazi zake kubwa ambazo alikuwa amepanga kuzitambulisha kwa mashabiki zake mwaka huu.

Amesema hayo leo kwenye mkutano na waandishi wa habari na kuonesha sehemu ya kipande cha Movie hiyo aliyoipa jina la NIPE CHANGU Ikiwa na Theme ya Mapenzi lakini pia sanaa ya uchekeshaji ikiwa imehusika ndani yake.

Filamu hiyo inatarajiwa kuachiwa Tarehe 18 mwezi August na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wageni kutoka Rwanda Pamoja na Nchi ya Kenya.

Utofauti mwingine uliopo katika Movie hiyo ni waigizaji ambao wameshirikishwa ndani yake kama vile, Asha Boko, Shamsa Ford, Mboto, Q Boy Msafi, Meneja Maneno, huku ikiongozwa na Waandaaji wa Filamu wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza Movie Hapa Nchini.

Davina Akiolewa Tena Naandamana:-Mayasa

mwanadada kutoka bongo movie Mayasa Mrisho amewashangaza  watu baada ya kusema kuwa rafiki yake kipenzi davina akiolewa basi yeye ataandamana kwa sababu  davina ameshazaa watoto watatu huku wakiwa wa baba tofauti na wanaume hao wamekuwa wakimuumiza sana kiasi kwamba amekuwa na machungu sana na  kuumizwa na mapenzi .

Mayasa anasema kuwa wa upand wa rafiki yake huyo Davina ameshaona kuwa hakuna haja tena ya kuendelea kuwaza maswala ya ndoa au mapenzi  kwa sasa anwaza sana maswala ya pesa kwa ajili ya kuweza kuwalea watoto wake.

Yaani siku Davina akiolewa tena naandamana  kwa maana wanuame wamemtenda sana jamani,sasa hivi ni muda wa kutafuta pesa tu kwa ajili ya kufanya mabo mbalimbali ya kimaisha kama anavyofanya ili aweze kuwalea watoto wake.

Hata alipoulizwa Davina mwenyewe alisema kuwa kwa sasa hana mpango wa ndoa tena zaidi ya kutafuta ela kwa ajili ya kulea watoto wake na ndio maana amekuwa akisafiri nje ya nchi ili kuweza kufanya baishara zake.

Neema Ndepanya Amchana Live Uwoya , ni Baada ya Wema Kushinda Tuzo

Wasani wa kike wa bongo movie Uwoya, Wema na Neema Ndepanya wameingia katika ugomvi mzito baada ya Neema kuamua kumuanika Irene Uwoya live na kusema kuwa amekuwa akimuonea wivu sana Wema sepetu wakati sio saizi yake.

Maneno ya Neema yanakuja baada ya siku ya jumanne Irene Uwoya kuweka picha na kuandika caption ya majungu huku ikiwa haionyeshi ni  nani alikuwa akisemwa katika post hiyo alindika “maumivu yakizidi muone daktari”

Neema Ndepanya ndipo alipoamua kumjibu kwa kumwambia”sarafu queen , maumivu yameshazidi tumemuona daktari na dozi tumeipata na tunaileta kwako kama ifuatavyo…wengi wanaijua sarafu series inayoruka DSTV na series hiyo ilisababbishwa na wema sepetu na  kuandikwa na mimi hapa na demo yake ikachezwa na wema,…..wema sio saizi yako na dau la wema lilikuwa kubwa sana na ndio maana waliamua kukufuata wewe hapa.kutokana na bajeti yao kubana ikabidi wakufuate wewe hapa  na kukupa ela ya kuosha gari la kubebea nyama..hivi wakati wanamfuata wema hawakukuona wewe, sanaa yako ya kutoa macho kama umebanwana gari la budege..”

Neema anaendelea na kusema kuwa nafasi za wema nyingi anacheza Uwoya kutokana na kuwa Wema amekuwa akikataa kulipwa ela ndogo, hata hivyo  neema anamwambia iren kuwa amekuwa akijifanya anajua kingerza kumbe hakuna kitu na wala hawezi sanaa ya kujipambanisha na Wema.

Neema ndepanya ameamua kumshauri Irene kwa kumwambia kuwa inabidi ajifunze kusifia kazi za wenzake ili aweze kusonga mbele sio kuwa na chuki na mafanikio ya watu wengine.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.