Penzi la Casto na Tunda Lasemwa Kuwa Matatani

Pamoja na kujitapa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kutokuachana kwao , wasanii maarufu Tunda na Casto dickson wameripotiwa  kuwa katika hali ngumu ya kimahusiano kutokana na penzi lao kuonekana kuyumba kwa sasa.

Wawili hao ambao pezni lao lilikuwa gumzo katika mitandao wanaonekana kuwa mbalimbali kwa sasa na kwamba kuna kidudu mtu kaingilia kati swala lao na kwamba haijulikani kama litaweza kukaa kama zamani.

Moja ya vyanzo makini vilisema kuwa kwa sasa wawili hao hata hawaonekani kuwa pamoja kutokana na ukweli kuwa penzi hilo limeisha kabisa na hata kuweka picha katika mitandao imefika kikomo kwa Casto.

Baada ya hapo GPL, waliamu kumtafuta tunda hili kumuuliza kuhusu swala hilo na ndipo aliposema kuwa kwa sasa yeye hana mchumba  na yuko bize sana na maisha yake na ana vitu vingi sana vya kufanya kwaio anaombwa aachwe.

Baada ya kutafutwa kwa Casto alishangaa kuambiwa kuwa tunda amejibu kuwa hana mpenzi na kusema kuwa kwa sasa wameamua kuweka mambo yao kuwa ya siri na hakuna kitu kitakacho watenganisha.

Casto Dickson Akana Kuitwa Mario kwa Tunda.

Mtangazaji wa kipindi cha siz kitaa kinachorushwa na Clouds media Casto dickson amekana tuhuma za mashabiki kumuita yeye kiben ten na kwamba maisha yake ya mapenzi tangu yameanza na Tunda amekuwa akilelewa na Tunda hivyo kwa vijana wa mjini wanaitwa mario.

Casto anasema kuwa alichofata kwa tunda ni mapenzi lakini pia yeye na Tunda kila mtu anakaa kwake hivyo unawezaje kumuita yeye kiben ten ilhali yeye anafanya kazi yake na anakaa kwake na pia tunda anakaa kwake.

akiongea na Dizzim online tv, Casto anawazjibu waandishi na kusema ”  how can you call mimi kibenten wakati mimi nakaa kwangu na yeye anakaa kwake na kila mtu anajitegemea

Lakini pia Casto ametoa siri ya maisha yake ya mapenzi na kusema kuwa mapenzi yamemuhathiri sana kiasi kwamba endapo atakaa muda mrefu bila kuwa katika mahusiano basi anakuwa too rough.

Casto Athibitisha , Tunda Amepokelewa Kwao.

Mtangazaji wa Clouds tv, Casto Dickson amesema kuwa kwa upande wa wazazi wake hakuna mwenye shida na maamuzi yake ya kuwa na mahusiano na mwanadada tunda kama watu wanavyokuwa wakiwatukana katika mitandao ya kijamii.

Akiongea na mwandishi mmoja wa habari casto anasema kuwa “uzuri mimi baba yangu huwa anaheshimu kile nilichoamua, ukijumlisha na kile nilichoamua na ushauri anaoutoa yeye kila kitu kipo sawa tu,my father hana wasiwasi na nilichokiamua na my mom alishafariki muda mrefu lakini naamini huko alipo anaona kuwa nilichokiamua ni sahihi.

Casto na tunda wapo katika mahusiano kwa muda mrefu sasa na kumekuwa na maneno mengi ya kuwashambulia kutokana  na kuamua kwao kuwa katika mahusiano huku wengi wakijaribu kuangalia maisha ya nyuma ya mwanadada Tunda.

For The First Time Tatoo Zetu Zitakuwa na Maana Tofauti:-Casto

Mtangazaji Casto Dickson amefunguka na kuongelea swala la yeye kuchora tatoo ya jina la mpenzi wake huku akiongelea swala mpezni wake huyo pia kuchora tatoo kama  yake huku akisema kuwa swala la wao kuchra tatoo lina maana tofauti na zile watu walizozoea kuziona katika mitandao na watu wakiangaika kuzifuta baada ya hapo.

Casto anasema kuwa kufikia hatua yake ya kuchora tatoo kuna maana kubwa tofauti na sio kama watu wanavyodhani,”utamuona akichora kama atachora wala huja haja ya kuangaika kama atachora utamuona,kwa sababu na yeye ana maamuzi yake pia tattoo sio kama pete kwa mba lazima tuwe nazo wote, na sisi tumeanza hivi tuna sababu zetu.”sisi tuna amaana yetu ambayo mtaiona iko tofauti kabisa, for the first time in afrika mtakuja kuona yeah,”

Casto anasema kuwa kwa sasa hajali kuhusu kuachana kwa sababu hata wakiachana hatakuja kufuta tatoo hiyo.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.