Dayna :Sifikirii Kutoa Album Sasa Hivi kwa Sababu Wengine Wametoa

Mwanadada ambae hivi juzi amekuja na  wimbo mpya huku mitaa mbalimbali katika mitandao wakimzushia kuwa yeye ni mama kijacho amefunguka na kuelezea kuwa hata kama kuna watu wengi kwa sasa wamekuwa wakitoa album  lakini kwa upande wake hajafikiria kufanya album kwa sasa hivi kwa sababu anaona kwamba bado hajaitaji kutoa album ya muziki wake.

Dayna Nyange anasema kuwa mashabiki wengi wanakuwa wanawashinikiza sana wasanii kuiga wasanii wenine kufanya kile walichofanya wenzao kwa sababu tu fulani kafanya , bila kujua kuwa kila kitu kina kuwa na wakati wake katika kazi.

sijafikiria kutoa album kwa sasa hivi  kwa sababu wenzangu wametoa album,mimi ni mtu ambae ninafanya kitu kwa muda wangu sahihi na muafaka na sio kufuata mkumbo kwa sababu tu fulani amefanya kitu hicho.siwezi kufanya ili nionekane kuwa tu nina album hapana, bali nahitaji kufanya album ambayo itakubalika.Alisema Dayna Nyange.

Hivi karibuni wasanii wa tanzania wameanza kuachia album zao akiwepo msanii pekee wa kike Vannesa Mdee ambae hata bada ya kuachia album yake ya money monday alikuja na kutoa mrejesho kuwa mashabiki wake wameipokea album hiyo vizuri na mauzo yanakwenda vizuri.

Nikki Wa Pili Alinifanya Niache Kurap – Dayna Nyange

Msanii wa muzuki wa Bongo Fleva  ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha Chovya mwanadada Dayna Nyange amefunguka na kusema kuwa kabla ajaanza  muziki alikuwa ni msanii wa kurap na alikuwa akimudu kufanya hivyo lakini alitokea mtu akamshauri kuachana na muziki huo kuwa haulipi ivyo afanye aina nyingine ya muziki.Mwanadada huyo anasema kuwa kwa kipindi cha mwanzoni alikuwa yupo vizuri katika kurap sana lakini alitokea Nikki wa Pili na kumwambia kuwa muziki wa aina iyo haulipi kabisa hivyo aachane nao.

“nakumbuka zamani nilikuwa nipo vizuri sana kwenye kurap  hadi nilitaka kusainiwa katika lebel ya Hermy B, B-hits kipindi icho tulikuwa tukifanya kazi pamoja na wakina AY , nakumbuka AY alikuwa akinisaidia hadi baadhi ya vitu vya kumuziki.Kipindi icho mtu kama AY ananisikiliza na kunionyesha nguvu yake katika muziki,najiona ukubwa wangu ulikuwa sehemu gani” anasema Dayna Nyange

Dayna anaendelea kusema kuwa lakini Nikki wa Pili ndio msanii aliemtoa katika kurap na kunipeleka katika kuimba, anasema ‘Nikki Wa Pili alimwambia atakuwa hapati ela endapo ataendelea kurap”Nikki wa Pili ndiye alinitoaa katika kurap na kunileta katika kuimba, aliniambia Dayna acha kurap utakuwa haupati ela aisee,, basi Nikki nakushuru,nikaaacha  na kurap kabisa na  nikaanza kuwa mwimbaji ” anafunguka Dayna

Dayna anaendlea kusema kuwa anashukuru kwa ushauri alioupata kutoka kwa Nikki kwa sababu umempa mafanikio makubwa sana, kwa sasa anatuzo kutokana na muziki huohuo”sasa hivi nina tuzo za BAE,AFRIMMA, so ninachoamini kila jambo lina wakati wake” aliongezea Dayna.

Mwanadada huyo ambae anafanya vizuri sana katika muziki amekuwa akitoa nyimbo nzuri pia , baadhi ya vibao vyake ni pamoja na ‘komela’ aliomshiriksha Billnass, ‘angejua’, ‘I do’, ‘Nivute kwako’ alioimba na Barnaba , ‘mimi na wewe’ na huu mpya unaojulikana kama ‘chovya’.

Dayna Nyange pia ni mama wa mtoto mmoja wa kike na amekuwa mama bora kimalezii, lakini pia Dayna ni mmoja kati ya wasanii wa kike wasiokuwa na scandal katika mitandao

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.