Alichofanya Diamond na Davido ni Love, Hatujalipwa:-Babu Tale

Meneja wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakisema kuwa inawezekana show ya Davido ilikuwa imeshapngwa ili Diamond atokee kwa suprise  katika ukumbi wa Nextdoor, Babu tale anasema kuwa kufanya hivyo kwa  Diamond hakuna malipo yoyote kwa sababu wale tu ni marafiki na walikuwa wamekweisha ongea.

ile ni love tunaita, wale wawili wanazungumza, kama angekuwa anamtaka diamond na kunifuata mimi basi angekuwa amefuata sheria lakini ameongea nane yeye na wakakubaliana  ule ni urafiki wao waliongea kwaio sisi tukatoa blessings tu tukamwambia nenda.

Ingawa hapo awali pia iliwahi kusikika kuwa wasanii hao wana bifu kubwa lakini maneno hayo yamethibitika kuwa hayana ukweli owowte kwa sababu waliwahi kutoa wimbo uliofanya vizuri sana wa ONE ONE REMIX.

Diamond na Davido Ndani ya Jukwaa Moja, Afanya ‘Suprise’ ya Ajabu

Muimbaji kutokea Nigeria Davido alifanya show katika Ukumbiwa Next Door Arena ulipo Dar es Salaam ambapo aliambata na wasanii wanao fanya muziki wa bongofleva ambao ni Ruby, Nandy, The Mafik, Aslay na wegine.
Lakini Moja ya Jambo ambalo halikutegemewa na mashabiki ni kumuona msanii Diamond Platnumz akipanda kwenye stage moja na Davido tena waki-perform wimbo wa Number one Remix, wimbo ambao Diamond aliwai kumshiirikisha Davido kipindi cha Nyuma.
Ikumbukwe kuwa Kumekuwa na mgogoro wa chini kwa chini baina ya Diamond na uongozi wa Clouds Media, huku mashabiki wa muziki nchini wakiachwa na sintofahamu. Ngoma za msanii huyo maarufu barani Afrika ni kama zimepigwa marufuku kusikika ndani ya redio ama kuonekana katika televisheni inayomilikiwa na Clouds Media.
Mara kadhaa, msanii huyo amekuwa akisikika akitoa vijembe dhidi ya redio na televisheni hiyo maarufu nchini.
   Ukiuliza urafiki wao umeisha vipi hakuna anayejibu sawa sawa, ndio maana Edwini Senzaba amesema mambo ya ‘Ngoswe muachie Ngoswe’.
    Mchongo uko hivi, Davido alikuwa na show hapo ambapo imeandaliwa na Uongozi wa Clouds.
Diamond alifanya show huko Dar Live na baada ya kumaliza aliondoka haraka na kwenda Next Door na kuruka na Davido kwenye ‘My Number One Remix’ huku shangwe likiwa kubwa kwa mashabiki waliojazana hapo.
Baada ya kumaliza show hiyo ya kama dakika 8 hivi, Diamond alisikika akisema kuwa “Nimekuja kumpasupport rafiki yangu tukutane Wasafi Festival,” amesema.
Baada ya maneno hayo alitoka jukwaani na kuondoka akiwaacha watu wakipiga shangwe kubwa sana.
Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.