BASATA Wapiga Kufuli Wimbo mpya wa Rayvanny na Diamond

Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.
Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema  kuwa wameufungia wimbo huo ambao amemshirikisha Diamond Platnumz na kupiga marufuku kuchezwa mahali popote.
Ameongeza kuwa wanawasiliana na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni.
Kuhusu kupigwa katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24 mwaka huu amesema nalo watalifungia iwapo watautumia.
Ameainisha kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanahamasisha ngono kinyume na maumbile na matusi mengine yanayobomoa maadili.
Wimbo huo ambao hauna siku nyingi tangu umeanza kusambaa katika mitandao  umeonekana kukisa sifa za kimaadili hata kusababushwa kufungiwa katika sehemu mbalimbali.
Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.