Rayvanny Agoma Kufuta Wimbo wa Mwanza Kwenye Mitandao

Licha ya kwamba msanii Rayvanny alitakiwa kuufuta wimbo wake wa mwanza ambao umetangazwa na BASATA kuwa hauna maadili yoyote katika jamii na kuamuliwa kufutwa katika mitandao ya kijamii lakini bado msanii huyo mpaka muda huo wa saa moja hakuwa amefuta wimbo ho zaidi ya kutoa shukrani kwa mashabiki wake kuufanya wimbo huo kuwa namba moja katika trending ya mtandao wa you tube.

Rayvanny na Diamond walitakiwa kuufuta wimbo huo uliotoka siku chache baada ya Basata kuhakikisha kuwa wimbo huo haupaswi kusikiliza katika eneo lolote kwa sababu una hamasisha maswala ya kingono ambayo ni kinyume na maadili ya kitanzania.

Wimbo wa Mwanza mpaka sasa umeingia katika trending na kuwa -viewed na watu zaidi ya milioni 1 ndani ya siku mbili.

Rayvanny Aongelea Mahusiano yake Ya Kazi na Bosi wake Diamond

Msanii anaefanya vizuri na ngoma yake ya makulusa rayvanny amefunguka na kusema kuwa ,tangu ameanza kufanya kazi na bosi wake diamond platinumz hawajawahi kugombana au kupishana katika swala la kazi hata mara moja.

Rayvanny anasema kuwa vitu vinavyokuwa vinatokea huwa ni vya kawaida ingawa pia vipo ambavyo huonekana kutopendezwa navyo lakini haijawahi kutokea wakagombana kabisa na kushindwa kuelewana.

Nikikosea lazima anikoromee, lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye sio mtu wa kufoka foka lakini ikitokea umekosea lazima atakwambia na utajua kuwa kitu hicho hajakipenda kwaio mtu mwenyewe hapo inabidi tu ujiongeze.-Akifunguka Rayvanny alipokuwa akiongea na funiko base ya Radio Five.

 

Maneno ya Rayvanny kwa bosi wake Diamond.

msanii Rayvanny amefunguka na kuzungumzia yale anayoyapitia bosi wake  ( DIAMON PLATINUMZ )  na kumwambia kuwa hakuna mafanikio ambayo hayana changamoto wala kukosa maadui.katika ukurasa wake wa instagram Rayvanny aliandika:-

Kuna vitu pengine unaweza kuwa unapatia au unakosea , sitaki kuongelea hiloswala kwa sababu wewe pia ni binadamu.ILA KWNYE KUSEMA UKWELI NITASEMA sio kwa sababu wewe ni boss wangu hapana !!ila mara nyingi thamani ya mtu  na umuhimu wa mtu watu huwa wanajua pale ambapo anakuwa amondoka.MUZIKI NI KAZI NA NI AJIRA  namaanisha kuwa kuna familia nyingi tu zinaishi kupitia huu mziki.

DIAMOND KATIKA WASANII WOTE  wewe umekuwa ni msanii wa kuongeza chachu kwa wasanii wengine, na kupitia wewe naamini kuwa wengi wamefanikiwa , KUJITOA KWAKO NA KUAMINI KATIKA UMOJA  NA PIA KUTHUBUTU ndipo kulikokufanya  unafanikiwa….USHAAMBIWA KUWA HAUJUI KUIMBA lakini uliimba na ukafanikiwa, ULISHAAMBIWA UNAVIMBA UNAIGIZA  MAISHA lakini sasa unayaishi hayo maisha ..hakuna aliyefanikiwa akakosa maadui ndivyo dunia ilivyo…

MIMI ULINISAIDIA ULIJUA SHIDA ZANGU naaminikuwa mungu alikutumia  wewe ukawe mkombozi wangu  KWAIO KUMBUKA KUWA ILI MBEGU ITE LAZIMA IOZE…. SINA MUDA  WA KUMSMA MTU ILA FANYA KAZI SIMBA

Hivi karibuni diamond aliingia katika vita na Naibu waziri kwa sababu ya kufungiwa kwa nyimbo zake mbili , na pia hivi karibuni alifunguka na kusema kuna watu na md=edia zipo kwa ajili ya kuua muziki wake na lebel yake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.