Daimond na Tanasha Waonyesha Kuwa Hawajaachana

Baada ya taarifa katika mitandao ya kijamii kuenea kwamba penzi la Diamond na mrembo wa Kenya, Tanasha lipo juu ya mawe. Mrembo huyo ambaye alitoa ahadi ya kuliweka penzi lake hilo private wiki hii ameibuka upya.

Wiki hii katika mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa kwamba Diamond na Tanasha wameachana baada ya muimbaji huyo kutamka katika moja ya interview zake kwamba hata funga ndoa tena mwezi ujao.

Jana Tanasha ambaye ni mtangazaji wa la NRG alipost picha ya Diamond Instagram na kuandika ujumbe wa upendo.

Baada ya post hiyo Diamond alimjibu mrembo huyo kwa kuandika ujumbe kwa amemkumbuka sana.

Katika hatua nyingine Natasha alitumia Insta Story kukanusha uvumi wa kwamba ameachana na Diamond baada ya kuona Rais huyo wa WCB anampotezea muda.

Bob junior Asema Hana Matatizo na Diamond, Wao ni Ndugu.

Baada ya muda mrefu kuonekana wasanii hawa wawili kuwa na bifu yaan Bob Junior na Diamond Platinumz,lakini baadae msanii Bob Junior alikuja na kujirudi na kusema kuwa hakuna matatizo yoyote kati yao huku akisema kuwa inawezekana kusingekuwa na WCB kama yeye asingeweza kufanya kazi na Diamond kwa mara ya kwanza.

Wiki iliyopita alipokuwa akiongea na Wasafi tv, Bob Juniour  alisema anajivunia sana Diamond kwa sababu anajua wapi wametoka na wapi aligundua kipaji cha msanii huyo.

Ikiwa jana ni siku ya kuzaliwa na tiffah ambae ni mtoto wa Diamond Platinumz, watu wengi walijitokeza kuwapongeza wazazi lakini pia kumpongeza mtoto wao, na mmoja kati yao alikuwa ni Bob Juniour na kuandika yafuatayao.

NAJUAMNAONGEAMENGI LAAKINI HAMJUI CHOCHOTE KUHUSU SISI,BASI LEO NAWAAMBIA KUWA HATUGOMBANAGI NA WALA HATUNA UGOMVI  NA HATUKUWA NA MATATIZO YOYOTE TULIPOTOKEA TUNAJUA MIMI NA NDUGU YANGU.TUKO PAMOJA LEO HAD KESHO AKHERA  NA NIKIWA KAMA BABA MDOGO WA TIFA NASEMA IVI HAPPY BIRTHDAY DAUGHTER  WE LOVE YOU SOOO MUCH TOTO YETU , THE QUEEN OF AFRICA TIFAH TIFANI.

Baada ya kuandika hivyo katika ukurasa wak wa instagram, diamnd nae aliweza kujibu kwa kuandika “shukrani sana ndugu yangu….”

Diamond Amuomba Mama yake Kuwapenda Wajukuu Wote,

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platinumz amefunguka na kumuomba mama yake kuwapenda wajukuu zake wote bila kuwabagua kama vile ambavyo amekuwa akimpenda yeye.Diamond ambae kila siku amekuwa muwazi kwa kila wanachofanya ndugu zake hakusita kuyasema hayo katika siku ya kuzaliwa ya mama yake.

Akiandika ujumbe mzito wenye kumtakia kheri ya sikukuu ya kuzaliwa mama yake mpenzi, Diamond pamoja na kumshukuru na kumuhaidi vitu vingi lakini hakusita kusema kuwa kama vile ambavyo anajua mama yake amekuwa akimpenda sana na anajua bado anampend basi pia awapende wajukuu zake wote bila kuchagua yupi wa kumpenda zaidi kwa sababu wale ni watoto na hawana hatia ya kuchukiwa kwa sababu hawana makosa.

katika ukurasa wake wa instagram, Diamond aliandika “……kama vile unipendavyo mimi mama pia uwapende wajukuu zako wote kwani ni wadogo sana na hawana hatia na hawaju chochote ingawa kuna muda wazazi wao wanakukwaza sana kutokana na isssue zetu bibafsi….’

Kwa muda mrefu kumekuwa kukionekana majibizano kati ya bi Sandra na   mama wa watoto waDiamond huku mama huyo akionekana kuwapenda sana watoto wa Zari kuliko yule aliyepo kwa Mobeto.hata hivyo hii sio mara ya kwanza Diamond kuwataka ndugu zake kuwa na upendo na watoto wake kwa sababu yeye tayari ameshakubali kuwa ni wa kwake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.