Dinno Kuwaenzi Waliopoteza Maisha Mv Nyerere.

Msanii mpya Katika game la bongo fleva anaejulikana kama Dinno ameamua kuwaenzi waliopoteza maisha katika kivuko cha maji cha Mv Nyerere huko Ukerewe ajali iliyotokea siku chache zilizopita na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 230

Msanii huyo pia a atazindua nyimbo yake mpya iliyoimbwa kwa ajili ya watu hao lakini pia atatambulisha nyimbo zake zingine mpya zilizoimbwa siku nyingi za nyuma zilizopita kwa mshabiki wake na kuongea na mashabiki wake ili wapokee vizuri katika game.

Mpango mzima utakuwa ni wikiendi hii ya October 6  ambapo  tukio hilo litafanyika mnazi mmoja katika jengo la ushirika ghorofa ya nne.Nawaomba  watu waniunge mkono .

Hata hivyo, Meneja wa msanii huyo anasema kuwa pamoja na kuwaenzi waliopoteza maisha na walipatwa na matatizo lakini pia watazindua rasmi lebo yao ya Nambiza siku hiyo na kuanza kufanya kazi na msanii wao Dinno.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.