Mr. Nice- Dudubaya Hajaacha Pombe Hana hela

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, aliyetamba miaka ya nyuma na style yake ya TAKEU ameanza kumchokonoa upya hasidi wake namba moja Dudubaya kwa kudai ukata unamsumbua.

Mwanzoni mwa huu Dudubaya aliutangazia uma amemuomba Mungu na amefanikiwa kuacha kunywa Pombe ambazo aliamini zilikuwa ni kikwazo kwake na maendelea yake kimaisha hivyo alisema hatokunywa Tena Pombe.

Mr. Nice ameibuka na kusema kuwa anaamini kuwa sababu pekee inayomfanya mpaka Dudubaya aseme ameacha Pombe ni kwa sababu hana hela amefulia hana chochote kitu hivyo hana uwezo wa kununua lakini hajaacha sababu za kiafya wala kimaendeleo kama anavyodai.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Mr. Nice alifunguka yafuatayo:

Mimi nampongeza kwa sababu sina sababu ya kumsikitikia sababu ni maamuzi yake mwenyewe lakini pia tusikae kumpongeza inawezekana ni tatizo la kiuchumi limempeleka huko kuacha pombe na inawezekana ametuambia ameacha pombe lakini akikaa chobingo anagonga mzigo kama kawaida au pia inawezekana ankara ya kununua imetetereka kidogo lazima aache”.

Mr. Nice amejisifia kuwa anaendelea na maisha yake kwani kuburudika ni sehemu ya maisha yake kwaiyo anapiga pombe kama kawaida

Dudubaya- Mr. Nice ni Kunguru, Young Dee Amemuokota

Msanii mkongwe wa mziki wa Bongo fleva Dudubaya ameibuka tena na kumpa maneno hasimu wake namba moja msanii mwenzake mkongwe wa Bongo fleva Mr. Nice.

Bifu kati ya Dudubaya na Mr. Nice halikuanza leo wala juzi bali nila miaka ya nyuma sana ambapo walikuwa na ugomvi mkali hadi kupelekea kupigana hadi kuvunjana mikono. Lakini bifu hilo limeelekea kuibuka upya hivi karibuni baada ya wawili hao kuanza kurushiana maneno kwenye vyombo vya habari.

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa Young Dee alitoa wimbo wake mpya siku chache zilizopita unaoitwa ‘Kiben-10’ ambapo kwenye nyimbo hiyo ameingiza melody na maneno na mistari kutoka kwenye nyimbo ya Mr. Nice na nyimbo ya Dudubaya lakini tatizo lilianza baada ya Mr. Nice kumtolea povu Young Dee kuwa kamuibia nyimbo yake na kumtishia kumchukulia hatua za kisheria.

Dudubaya kwa upande mwingine amekuwa na mtazamo tofauti kwani kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv amefunguka yafuatayo;

Mimi moyo wangu ulivyoumbwa ni wa kusaidia sipendi kuona mwenzangu anakwama kwa kitu fulani kwaiyo hiyo imenipelekea kufikiria kuwa alichofanya Young Dee kuchukua mistari yangu kwangu mimi sio ishu wala sio dili ya kwenda kuhitaji malipo ya aina yoyote kwani kazi aliyofanya Young Dee ni nzuri na ubora wa kazi yake ni wa hali ya juu”.

Lakini Dudubaya amefunguka kuhusu Mr. Nice kukasirishwa na Young Dee kuimba nyimbo yake bila ruhusa;

Mimi naona Mr. Nice asilalame sana kwa sababu hawa ni wadogo zetu kam hawaja kupigia simu basi aidha simu yako ilikuwa haipatikani kwanza anavyolalama asiwe kama kumbi kumbi aliyekatwa mabawa sasa Young Dee kafanya wema kumuokota ili arudi kupaa sasa anaanza kupiga makelele ili watu wajue kuwa Young Dee ndio kamkata mabawa lakini mimi naona Mr. Nice anataka alipwe tu kwa sababu kiuchumi yupo kwenye hali mbaya”.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.