Siwezi Kukosa Mwaliko wa Harusi ya Lulu :-Juma Lokole

Kijana maarufu mtandaoni  juma lokole maarufu kama kichefuchefu amefunguka na kuongelea harusi ya rafiki yake kipenzi Lulu Elizabeth Michael na kusema kuwa amekuwa akisikia katika mitandao wakiongelea swala hilo alkini hata kama harusi ipo hata siku moja hatokosa katika sherehe hiyo.

Nani kasema kuwa kuna harusi (huku anacheka) harusi kifika mtaambiwa tu lakini jua mimi  siwezi kukosa harusi ya lulu hata siku moja na ikifika tu mtajua kuwa imefika na lisemwalo lipo na kama halipo linakuja kwaio tuake tusubiri ingawa hata mimi hzi habari ninazisikia tu.

Juma anasema kuwa harusi lazia itakuwepo kwa sababu pezni kati ya lulu na majizo sio la kinafiki kama watu wanavyofikiria lakini ni penzi kutoka moyoni.

penzi lao sio la kinafiki ni mapenzi kutoka moyoni, majizo anampenda Lulu na Lulu  anampenda Majizo na kama rc katangaza maswala ya ndoa basi rc atakuwa anajua.

Kesi Ya Lulu Yahairishwa Tena ,Mke Wa Dk.Slaa Haitajika.

Kesi ya msanii wa bongo movie iliyokuwa ikiendelea leo mahakamani , imehairishwa tena baada ya kukosekana kwa shaidi aliyekuwa moja wa madaktari. Shaidi huyo aliyetajwa kwa jina la Dk. Josephine Mushumbusi  inaesemekana kuwa ni mke wa Dk.Slaa ,ambae yuko nje ya nchi, ushaidi wake ulikataliwa kukubaliwa na kupokelewa na mahakama hadi pale atakapowakilisha  na daktari huyo mwenyewe au askari aliyeandika maelezo ya daktari huyo.

Hapo jana, wakili wa mshtakiwa anaejulikana kama Peter Kibatala  aliiomba mahakama kukubali kuupokea ushahidi wa shahidi huyo  uliotumwa na Dk. Mushumbusi akiwa nje ya nchi, lakini mahakama ilikataa kupokea ushahidi huo na kudai kuwa  upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo, na kutoa maamuzi hadi pale shahidi halali wa kesi hiyo awepo au askari aliyekuwepo wakati wa kutolewa kwa maelezo hayo.

“Josephine Mushumbusi, huyu ni mke wa Dk.slaa,lakini kwa bahati mbaya hayuko nchini na juhudi za kumpata zimeshindikana,kwaio wakawa wanaomba maelezo yake alioandikishwa na polisi yaweze kupokelewa mahakamani, bila ya yeye kuwepo” aliongea mmoja wa wataalamu wa mashtaka mahakamani hapo.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ulikataa kuwa Kibatala hapaswi kujivika kofia mbili(wakili na shahidi kwa wakati mmoja), hivyo kesi hiyo imehairishwa tena mpaka tarehe 25 Oktoba , ambapo askari wa daktari huyo anapaswa kuwepo mahakamani hapo kwa ajili ya kusoma ushahidi huo.

Wakati wa kuondoka mahakamani hapo msanii wa maigizo Lulu Michael alionekana kutimua mbio kwa lengo la kuogopa waandishi wa habari huu baba yake mzazi akiwa anamkingia kifua ili kukwepa picha hizo.

Lulu akiwa mahakamani leo Oktoba 24

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.