‘Mastaa Wengi Wanataka Mapenzi Ya Kweli na Sio Pesa”- Esther Kiama

Msanii wa filamu za Bongo movie Esther Kiama ameibuka na kusema kuwa mapedeshee wa mjini hivi sasa hawana dili kama zamani kwani wasanii wengi wa kike hawaangalii pesa bali wanataka mapenzi ya kweli.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Ester alisema mastaa wengi wameg­undua mapenzi ya kweli hayapo kwa mapedeshee ambao walikuwa wana­watumia tu kupitia hela zao.

Unajua zamani mapedeshee walikuwa wakitumia mifuko yao kuwarubuni mastaa mbalimbali lakini sasa mambo yamebadilika, wengi wa wasichana sasa hawatazami pesa bali mapenzi ya kweli na ndio maana ukichunguza utaona mastaa wanatoka na wanaume wa kawaida sana ambapo wakati mwingine si rahisi kuamini“.

Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakitajwa kuwa na mahusiano na wanaume wenye pesa wanaojulikana kama mapedeshee.

Esther Kiama Agoma Kuanika Mipango Yake Kuhofia Wanga

Muigizaji wa Filamu za Bongo movie Esther Kiama ameibuka na kudai anahofia kuanika mipango yake ya mwaka 2019 kwa kuhofia wanga wataweza kumkwamisha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Ester alisema mwaka ujao anatarajia kufanya kitu kikubwa, lakini hawezi kukitaja kwa kuwa wanga watampiga juju na kushindwa kufikia malengo yake.

Nimejifunza kwamba kwa mwaka huo unaoanza ni vyema nikafanya vitu kimyakimya hadi vikamilike maana nikianza kutangaza, wanga wasiopenda maendeleo yangu, wataya-katisha fasta na kujikuta nashindwa kusonga mbele”.

Esther Kiama ameigiza sinema nyingi za Bongo movie lakini filamu moja ambayo imempa umaarufu zaidi ni ‘Muhanga’.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.