Ferooz Atangaza Kujipanga Upya.

Msanii ferooz amekiri kuwa katika  game la muziki kwa sasa kuna utofauti mkubwa sio kama ilivyokuwa zamani kutokana na ukweli kuwa kumekuwa na wasanii wengi chipukizi ambao wanafanya vizuri sana katika muziki.

Ferooz anasema kuwa kwa sasa anataka kurudi katika game lakini kitu cha kwanza anataka kukifanya ni kujipanga na kuangalia ni jinsi gani anaweza kuwa sawa na wale waliopo katika game kwa sasa kwa kuisoma ramani ya muziki wa sasa na sio kurudi kama walivyozoea hapo awali,

Ferooz ambae aliwahi kutamba sana miaka ya nyuma hasa kwa wimbo wake wa starehe anasema kuwa muziki ni kama maisha kuna sehemu utapanda sana na kuna sehemu unaweza kushuka kabisa lakini swala la muhimu ni kuangalia ulipojikwaa na kurekebisha tena.

muziki uko kama maisha ya kawaida kuna kupanda na kushuka, ila kwa sasa niko napmabana ili niweze kupanda tena .

Ferooz anasema kuwa ana nyimbo mbili ambazo ataziachia mfululizo hivi karibuni na anaomba mashabiki wakae mkao wa burudani zaidi.

Ferooz Ataja Sababu Zilizopelekea Ukimya Kwenye Muziki

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Ferooz aliyewahi kutengeneza hits kama Starehe, Barua na Bosi na myinginezo amefunguka na kuongelea ukimya wake Kwenye gemu ya Bongo fleva.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ferooz amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na miaka mingi kupita bila kusikika lakini bado anapambana na gemu na mwili kukata tamaa:

Nipo napambana maana game ya muziki ni kama maisha mengine ambayo ni mzunguko unaweza ukawa juu au ukashuka. Napambana kupanda juu upya kwani Sijaachana na muziki na siwezi kwa sababu muziki ndio maisha yangu ila ni changamoto tu zilinipitia ndio maana nikawa kimya”.

Lakini pia Ferooz amefunguka na kukataa tetesi za k amna kundi lao la Daz Nundaz lilivurugika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya:

Hapana hatukujiingiza kwenye madawa ya kulevya kwa sababu kuna vitu ambavyo vinatokea kwenye kundi kama migogoro mara huyu anasema hivi, mara vile nikaamua kuhama kwenye menejimenti kuna kipindi nilikuwa kwa Mkubwa Fela, unajua mkishaanza migogoro lazima mshuke kwenye kazi mkiwa kundi na kikubwa ni kwenye mgawanyo wa fedha ndio ilikuwa shida na si kweli kwamba madawa ya kulevya ndio yaliua kundi ni maneno tu ya watu wakiona unashuka wanazungumza yao lakini mimi nipo safi ukiniangalia na hata sauti yangu pia iko safi.

Nashindwa Kuacha Muziki Upo Kwenye Damu.

Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva FEROOZ  amefunguka na kusema kuwa anatamani sana kuacha muziki lakini anashindwa kwa sababu muziki kwa sababu upo kwenye damu.Ferooz anasema hayo na kusema kwamba uamuzi huo aliamua kuuchukua kwa sababu anaona kuwa anaonekana kama sio kitu wakati yeye ameotoa muziki mbali.

Kikubwa ninachokiangalia sana ni wapi nilipotoka na muziki huu nilipotoka mpka hapa nilipofika halafu bado naonekana kama mimi ndio nimekosea,game limenisahau kwa kifupi, lakini pia mpaka nafikiria ku-quit muziki najikuta niache muziki lakini nawaza niktangaza kuacha muziki siwezi maana muzii upo kwenye damu.

Lakini pia Ferooz ansema kuwa pamoja na hayo yote lakini pia amekuwa akifanya mambo mengi lakini mwisho wa siku ninajikuta ninarudi kwenye muziki.

 

 

Ferooz: Biashara Ya Madini Ilinipoteza Kimziki

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Ferooz aliyetamba na vibao vyake ‘starehe’ na ‘boss’ amefunguka na kudai kitu kilichomfanya akae kimya mda mrefu kimziki ni kuingia kwenye biashara ya madini.

Baada ya kupotea kimuziki kwa zaidi ya miaka saba na kutajwa kama miongoni mwa wasanii waliofilisika na kufulia kabisa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa, kupitia kipindi cha Enews Ferooz amefunfuka kuhusiana na biashara ya madini ilivyo mfilisi na uamuzi wake wa kurusi kwenye muziki mazima:

Biashara za madini kwa sasa nimeachana nazo sahivi nimeamua kurudi totaly kwenye mziki wangu , nilifanya fanya biashara ya madini lakini mwisho wa siku nikapoteza pesa zangu nyingi zikapotea ila sasa nimeamua tu kurudi kufanya music full package kama Ferooz nina kazi zangu mpya nimetoa mashabiki zangu wazipokee, nimeshatoa wimbo wangu mpya unaoitwa ‘nakaza roho’ kwa sasa nina timu yangu mpya ambayo tuna endeleza gemu”.

Pia kutokana na ujuzi alioupata kwenye biashara ya madini aliyofanya kwa miaka yote hii Ferooz kafunguka nini hasa ilikuwa sababu ya kupoteza pesa zote alizozipata kipindi anaimba madini:

Unajua kila biashara ina experience zake sasa mimi kwa kuwa nilikuwa nimeshazea kifanya muziki nikaingia tu bilakujua lolote na kuna vitu vingi sikuvijua nikaja kujikuta vitu vimeenda vibaya mwisho wa siku nikajikuta nimepoteza pesa nyingi basi mwishoni ndio nimeamua nirudi kwenye muziki 

 

Msanii Mkongwe Ferooz Amekana Tuhuma Za Kutumia Madawa Ya Kulevya

Msanii mkongwe wa bongo fleva aliyetamba miaka ya nyuma kidogo na nyimbo yake ya ‘Starehe’ iliyofanya vizuri sana amefunguka na kudai tuhuma zinazomkabili kuwa anatumia madawa ya kulevya sio za kweli hata kidogo.

Wasanii wengi waliokuwa wanafanya vizuri siku za nyuma huishia kuchukua njia mbaya na hivyo kuishia kujiingiza katika matendo maovu kama kuuza na kutumia madawa ya kulevya na hivyo kupelekea vipaji vyao kufa wengi wao hudai hujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu ya ugumu kwenye gemu mfano wa wasanii waliojiingiza kwenye madawa ya kulevya ni pamoja na Ray C, Chiddi Benzi.

Ferooz ni moja Kati ya wasanii ambaye kwa kipindi kirefu ametuhumiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya Kulevya ambayo ndio yamepelekea kupotea katika ramani na kuzidi kuwa kimya tuhuma ambaxo Ferooz amezikana kwa nguvu shutuma hizo na kudai kuwa taarifa hizo hazifai kuaminiwa na watu wanaozisambaza ni wale wenye nia ya kumchafua na wasio mtakia mema.

Sijawahi kutumia dawa za kulevya na kama kuna mtu anayeshupalia kitu hicho tunaweza tukaweka dau tuende tukaangalie tuhakikishe na kama natumia sawa atakua ameshinda na jamii itakuwa imejua na kama nitaonekana situmii basi niondoke na dau langu na jamii itakuwa imeshajua situmii kitu kama hicho”.

Pia msanii huyo alielezea nia yake ya dhati ya kutaka kurudi kufanya muziki hivi karibuni kwa kutangaza kuwa anategemea kutoa ngoma yake hivi karibuni.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.