Steve Nyerere Aingilia Kati Ugomvi wa Gabo na Duma

Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, ameingilia kati ugomvi baina ya Duma na Gabo Zigamba huku akimtaka Duma kuachana na masuala hayo kwa kuwa anaetaka kushindana naye yupo juu yake zaidi kwa kila kitu.

Steve ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha eNewz
huku akionekana kukerwa na kitendo hicho ambacho kimedumu kwa muda mrefu kwa wawili hao na kupelekea Steve kuwafananisha na wanyama aina ya mbuzi na kuku kutokana na tabia zao. “Hapa katikati kuna mbuzi na kuku, lazima tuheshimiane kutokana na urefu na hata jinsi mbuzi anapochinjwa kilo zake huwa kubwa na kilo za kuku ni ndogo. Kwa hiyo lazima waheshimiane hata kwa kilo, ukuaji. Wasifikilie kwamba ugomvi wanapokuwa wanagombana ulaya basi nasi Afrika tufanye ili tuuze sokoni maana wengine wanasema kugombana ni kiki, na kataa hilo muda mwingine ni kudhalilishana tu“, amesema Steve.

Pamoja na hayo, Steve Nyerere ameendelea kwa kusema “heshima sio lazima uwe umetoka nayo nyumbani kwenu hata unapokuwa heshima unakuwa nayo ili upate kumuheshimu kila mmoja upate connection na maisha ya kesho na kesho kutwa”.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.