Madee atisha baada ya kuonyesha gari ‘yake’ mpya

Msanii wa Bongo Madee ni mmoja wa watu ambao wanapenda kuonyesha vitu vyao vya thamana mitandaoni. Kama sio saa ni viatu ama kitu kingine.

Lakini hivi karibuni aliwaacha mashabiki wake kama wameduwaa baada ya kuonyesha gari ambalo lina jina lake kwenye number plate.

Hata hivyo Madee hakudhibitisha kuwa gari hilo ni lake lakini aliandika kusema, “Gangster paradise!!! #WinoMweusi,” huku akiwapa mashabiki wake nafasi ya kubashiri ikiwa amenunua gari.

Kama kawaida wengi walimpongeza na wengine wakimsomea kwa kuwaringia na gari ambalo wanajua sio lake. Madee hata hivyo hakuwajibu kwani yeye anaishi maisha ya super star.

Tazama gari hilo hapa.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.