Penzi la Gigy Money na Mo-jay Larudi Upya.

Mwanadada Gigy money na baba wa mtoto wake Mo -Jay wameonekana kuwa watu wenye furaha tena licha ya wawili hao kukumbwa na skendo nyingi ikiwepo ile ya kugombana mpaka Gigy Money kupigwa na baba wa mtoto huyo.

Wakionekana wenye furaha hasa msimu huu wa sikukuu , wawili hao wameonekana kufurahia penzi lao hilo ambalo linaonekana kuwa kama jipya huku wakiungwanishwa na mtoto wao

Ikumbukwe kwamba, gigy moneya aliwahi kuoekana akiwa na mwanaume mwingine na pia Mo-Jay vivyo hivyo huku gigy money akisema kuwa hajaumia kabisa kumuona mo-jaya akiwa na mwanamke mwingine huku akitoa baraka nyingi kama kuna ndoa itafuata.

Hata hivyo wawili hao wanasemwa sana katika mitandao kuwa wamekuwa wakipendana na kwamba ni vigumu kwao kuachana inganwa kumekuwa na hiyo misukosuko ya kila mara.

Penzi la Gigy Money na Mo j Lafika Mwisho.

Penzi la mwanadada Gigy Money pamoja na mpezni wake ambae ni mtangazaji wa Choice Fm limesambaratika mara bada ya dada huyo kujifungu amtoto wa kike siku chache zilizopita na kutokea malumbanio kati yao na kusabababisha kusambaratika kwao.

Akiongea ndani ya Clouds Media , Gigy Money amesema kuwa yeye na Mo J wameachana rasmi huku akitoa sababu kubwa ya kuachana kwao ikiwa ni kutokana na kutoheshimika kwake kwa mwanaume huyo na amekuwa akimtolea maneno machafu ndani kipindi yupo mjmzito lakini aliyavumilia na sasa naona bora kuachana nae.

kweli kwa sasa ni ex wangu,baba wa mtoto wangu  mzazi mwenzangu lakini inafika sehemu inabidi ukue kiakili  na ukubaliane na hali halisi , huwezi kuishi na mtu kila siku hakuna tofauti kati ya mwaka jana na mwaka juzi ni yaleyale na wanaume wote hawa duniani.

Hata hivyo Clouds media ilimau kumtafuta mo j kwa ajili ya kumuuliza kuhusu swala hilo na ndipo alipokubali na kusema kuwa ni kweli lakini mtoto atabaki kuwa  wake na hata iweje hayo maswala mengine anamuachia mama mwenyewe.

Mo-Jay Akiri Kumpiga Gigy Money Akiwa Kwenye Hali ya Ujauzito.

Siku za nyuma hivi  msanii wa kike bongo Gigy Money, aliandika post kubwa katika ukurasa wake wa instagram huku akilalamika kuwa mwanaume aliyempa ujauzito amekuwa akimtesa na kumpiga .Gigy alilalamika na kusema kuwa mwanaume huyo amekuwa hajali sana hali yake ya ujauzito na kumpiga sana akiwa katika hali kama ile.

Hata hivyo wakizungumza walipokuwa pamoja katika red kapeti ya usiku wa Nandy,Aslay na marafiki , Gigy Money alianza kwa kusema kuwa walishayazungumza mambo hayo na sasa hivi wako sawa kabisa ingawa mara nyingi amekuwa akimshatika mpenzi wake huyo kwa wazazi wake lakini siku hiyo ilikuwa ni too much ndio maana aliamua kumpost instagram kwa sababu anajua kabisa kuwa mpenzi wake sio mtu wa  kupenda kuwekwa katika mitandao.

Ilikuwa ni lazima tupatane  ndio maana sikumponda wala kumtukana lakini niliandika na kuongea kwa wote  sio mo pekee yake huwa nakosega kuna muda mwanaume anakuwa na hasira moaka anaamua kumpiga mwanamke wake.lakini ameniomba msamaha na yameisha ingawa mara nyingi nikiwa na hasira huw aninamwambia mama yake au mama yangu lakini siku ile ilikuwa too much.

Alipoulizwa kuhusu habari hizo za kumpiga mzazi mwenzie Mo-jay alikiri kuwa ni kweli alimpiga lakini sio kipigo kikubwa kama wanavyodhani na hiyo yote ilisababishwa na hasira za Gigy Money mwenyewe.

Unajua wakina mama wanapokuwa katika hali aliyonayo gigy wanakuwa ni vigumu sana kuwaelewa,unaweza ukafanya kitu kidogo yeye akachukulia kuwa ni kikubwa na honestry kuna kitu alikiwa amefanya ambacho kilikuwa kinahatarisha maisha ya mtoto hivyo  na alinikera na sio mara moja mara mbili amekuwa akikifanya kwaiyo sikumpiga insuch lakini hakikuwa sawa kwaio nilipata hasira kama mzazi na tukakwazana nae na kwa sababu yuko kwenye hali kama ile anakuwa anafikiria mengi sana.

lakini sio kipigo ambacho watu wanasema nimempiga lakini ni ile tu kukwazana na kurekebishana na ndio maana hata mkikwazana na akigeuka mara moja mara mbili hakuoni wala haupigi simu basi anakuwa anapata hasira sana.

Hata hivyo Gigy Money na mzazi mwenzie Mo-Jay wanasema wanategemea kupata mtoto wa kike na tayari walishapata jina la kumwita atakuwa akiitwa Candy ambapo wanategemea kuanzia mwezi ujao siku yoyote wanatarajia kupokea mtoto wao.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.