Gigy Money kuwachia wimbo mpya – papa

 

Gigy Money ambaye ni video vixen amefunguka kudai kuwa anamipango ya kuachia wimbo wake wa pili unaoitwa ‘Nampa Papa’. Hii inakuja mwaka mmoja baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Supu’ uliompa umaarufu Tanzania.

Mrembo huyu aliambia Bongo 5 kuwa wimbo huu ulitayarishwa na procuder Kimambo Touches. Aliendelea kwa kusema kuwa wimbo huu unasifia urembo wa wanawake na kuwa wengi wataufurahia.

“Nampa Papa ni wimbo fulani kama nyimbo zangu zilizopita, ni kama Supu nilikuwa najivunia maumbile yangu. Kwahiyo kwenye ‘Nampa Papa’ ni wimbo fulani ambao bila shaka kila mtu ataufurahia,”

 

Aliongeza,

“Kwahiyo mabibi na mabwana tukae mkao wakula Gigy kaleta balaa jingine jipya tuoneshe ushirikiano na thamini vya nyumbani. Pia wimbo huu sijaandika mwenyewe nimeandikiwa na mwanangu mmoja anaitwa Marioo,”

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.