Amber Lulu awajibu wanaomsingizia kuwa anatumia ‘unga

Hakuna kitu ambacho kinachomkera Lulu Amber kama watu wanaodai kuwa anatumia madawa ya kulevya! Amber Lulu ambaye ni msanii na mrembo wa video za bongo amewakanya watu hawa akiwaambia waje basi wampeleke ‘sober house’ (rehab).

 

Msanii huyu alifunguka kuhusu maneno haya akizungumza na 3-Tamu ya Tanzania. Amber Lulu aliendelea kuwa wanaomsema wanapaswa kumpeleka apate tiba badala ya kumsema.

“Nimekuwa nikisemwa kila siku kuwa ninatumia unga, sasa nasema kama kuna mtu ana uhakika na hilo, basi anipeleke sober house nikatibiwe. Ni vyema watu wakajua kuwa hata mimi ni binadamu, ninaumizwa na kuse­mwasemwa,”

Hata hivyo alisema kuwa mtumiaji wa Unga hujulikana, kwa hivyo wampe muda waone ikiwa yeye anatumia madawa haya ya kulevya.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.