Naibu Waziri Apigilia Msumari Wa Moto Kauli ya Mh. Rais

Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Mh. Juliana Daniel Shonza  amesema kuwa wizara yake haitasita kutoa adhabu au kumchukulia hatua msanii yeyote yule atakae kiuka agizo la kuvaa nguo nusu uchi kwa kisingizio cha kuwa msanii.mh shonz aliyasema hayo katika uzinduzi wa tamasha la tukuza Utalii wa Tanzania Festival  lenye lengo la kukuza utalii wa Tanzania lilikuwa limeandaliwa na  shirikisho la waimbaji wa injili Tanzania.

Wasanii wote ambao watakuwa wanakaidi agizo alikuwa ametoa Mh.raisi wa tanzania  la kuvaa mavazi yenye staha na hshima, wizara yangu wala haitavulimia na kuwaacha kwa kutokuwachukulia hatua watu hao, hii haitajali nafasi yake katika jamii wala umaarufu wake .naomba kabla dhoruba haijawakumba naoma wabadilike  kwenye kupiga rungu wala sitaangalia usoni.

Maneno ya Mh.Naibu WaMiri ni mkazo wa maneno yaMh. raisi aliyokuwa ameyasema mapema mwezi Desemba mwaka 2017 alikuwa katika mkutano wa umoja wa wazazi wa CCM Taifa uliofanyika Dodoma , ambapo Mh.Magufuli alisema kuwa amekuwa akisikitishwa sana na tabia ya wasanii hasa wa kike kuwa wanatokea katika video na tv wakiwa uchi , Mh .raisi alisema kuwa kitendo hicho ni ukosefu wa maadili na imekuwa ikisambaa kwa kasi sana kufanya kuchafuka kwa maadili n kufa kwa utamaduni.

Hata hivyo kauli ya M.rais iliendena na agizo kwa mamlaka husika kushughulikia swala hilo ili kuondoa kusambaa kwa picha na video zinazowacha watu wazi.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.